Thursday, September 22, 2011

WAZO LA LEO :- USIKIVU WA WANAUME NA WANAWAKE KATIKA MAISHA YA NDOA/ULIJUA KWAMBA...

...Kama unataka kupata usikivu wa mwanamme kitu muhimu ni kumgusa? na pia ulijua kama unataka usikivu wa mwanamke basi mnongóneze!!! TUTAKUTANA/ONANA TENA KESHO!!!!

6 comments:

Mija Shija Sayi said...

Kwa kweli sikuwahi kufikiria hili ila naona lina ukweli ndani yake... au Kitururu unasemaje?

Simon Kitururu said...

@Da Mija: Tatizo kwetu huku Uarabuni kuguswa na mwanamke kuna masharti na kumnong'oneza mwanamke iko kazi!

Halafu kwao waliombali na mtu, Kunong'ona kwenye simu inaweza kuwa ni usumbufu kwa msikilizaji na kugusana haiwezekani!

Ok tukiacha utani;
Mimi nadhani inategemea na ni nani unaongea naye na tamaduni zina nafasi yake hapo. Huwezi Da Mija kuanza kumgusa Rais Nyerere ili tu akusikilize kwa kuwa inaweza kuonekana hata kwa Nyerere mwenyewe kunadharau fulani.

Na kuna mambo huwa yanafaa kunong'ona kwa kuwa siwezi tu nikaanza kukunongoneza jambo lolote tu hata la kuwa SIMBA imemfunga YANGA halafu ukanielewa kweli nimaanishacho ni swala la mpira wa miguu.

Kwa hiyo inategemea tu katika hili ingawa naweza kuelewa kuna mazingira topiki fulani huweza kunogesha kastori katamu kenyekupandisha tamu nyingine kama mtu akinong'onezwa hugu akiguswa kiufundi.

Anonymous said...

Nimeipenda!!!unaona mwanadada huyo ailivyosisimka? inaashilia ndo anaelewa zaidi.

Anonymous said...

KUGUSA NA KUNON'GONEZA NI WONYESHO DHAHIRI WA HISIA MWENZI NA MAHABA
ENDELEVU KATIKA MCHAKATO WA KUBORESHA NA KUDUMISHA VIFUNGO VYA NDOA
KWA MUJIBU WA SHERIA NA KANUNI ZA KIMUNGU KWA WENZI WA NDOA.

Anonymous said...

-----WONYESHO DHAHIRI WA HISIA MWENZI NA MAHABA ENDELEVU KWA WENZI WA NDOA................!!
-----------Ndoa na iheshimiwe kati ya wote, na kitanda cha ndoa kiwe bila unajisi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi-------Waebrania 13.4---------------
===================================
R.Njau

Salehe Msanda said...

Habari.

Ni kweli unachosema na zaidi wanasema mnong'oneze kwa kutumia sikio la kushoto: