Thursday, September 22, 2011

PICHA YA WIKI:- CHUPA ZA MAJI NA MAANDISHI YA MAISHA .....

.....sikuweza kuacha kuzifotoa kwa vile zinalingana na jina la blog hii MAISHA NA MAFANIKIO
nadhani wote mnakumbuka mwanzoni blog hii ilikuwa ikiitwa MAISHA TU:-)

5 comments:

Simon Kitururu said...

Nimeulizwa kwanini jina chupa hutumika kwenye vidude kama hivyo vya plastiki na kuwa kama ni sahihii kutumia `` VYUPA VYA`` na sio ´´CHUPA ZA´´ sasa hivi wakati nakodolea bloguyo Yasinta!


Na nikaulizwa zaidi kuwa: SI chupa ni za kiglasigalasi?


Na bado nakuna kichwa!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Simon...unanifanya hata mie nikune kichwa sasa...unajua sikuwaza sana kwote huko ...nilijua chupa na umoja na vyupa ni uwingi...na labda ningeweza kusema chupa/vyupa vya plastiki....nadhani kuna mmoja lazima atajua...tusubiri...u tuendelee kukuna vichwa vyetu kidogo...

Anonymous said...

Katika Kiswahili mazungumzo Yasinta anapendeza na blogu yake inachapa mwendo.Lakini kama tunataka usanifu wa lugha ni tuwaachie wanazuoni wa lugha ya Kiswahili watoe semina elekezi.Maji ya maisha ni maarufu sana kutokana na wingi wake na bei nafuu.Maji haya yalijipatia umaarufu wakati wa kipindi cha maisha plus.Siku hizi maisha ya vijijini hujulikana kama maisha plus!!!
------------------------------
R.Njau

ISSACK JIAH said...

Leo nimechungulia blog nilijiuliza kwani mpaka saa sita hajabadili nilitumia njia nyingine ya kutaka kujua kwanini mada hajibadiliswa ila nadhani ni haraka ndo akaandika hilo neno CHUPA VYA MAJI ila ni kwavile aliandika habari nyingi wiki ile ya kule mbeya ndo akili ililemaa alijua bado yupo mbeya kwa vyupa nya maji pole vyuma vya leli hiyo ni poa hakuna msamiati wala wingi wa chupa,CHUPA NI CHUPA HATA ZIKAWA MILIONI POLE
Hayo kwani hutukupa pole na kaka yako aliyeunguliwa na banda la vyiatu kule kumbeya uwombile uli mkavu na loli ni pale alipoamwambia mzungu uli mkavu brayan ;;akasema ooo""" sitaki wali mkavu nataka wali na maharage" kuti vyiki brayan ... akajibu tena SITAKI WALII MKAVU NATAKA WALI NA MAHARAGE hoo naloi sikuja na loli nimekuja na train
jioni njema
che jiah

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo! ndugu zangu ..Labda nianza na kuwapa SAMAHANI kiswahili ni kigumu jamani...narudi na ntabadili hapo kwenye kichwa na habari badala ya VYUPA VYA nitaandika CHUPA ZA....kaazi kwelikweli...kweli kublog ni kuelimishana..Ahsanteni.