Friday, September 16, 2011

BREAKING NUUUUUUUUUUUUUUUUZ: SOKO KUU LA SIDO JIJINI MBEYA LINATEKETEA KWA MOTO HIVI SASA

Hii ni hatari jamani
Kaka Selafim Ngonyani akiwa kwenye ofisi yake na wajomba zake pia dada yake ilikuwa mwaka huu 2011 mwezi wa sita mwishoni

Nimepata na mstuko .Muda si mrefu nimepata habari kutoka kwa kaka yangu hapo kwenye picha mwenye shati nyeupa..kuwa ofisi yake imeungua moto...ila amebahatika kuokoa baadhi ya vitu. Na yeye mwenyewe yupo salama..Hapo ilikuwa mwaka huu nilipokuwa nyumbani tulipita Mbeya mpaka hapo Ofisini kwako yeye ni Fundi viatu...habari zaidi unaweza kusoma hapa na hapa

12 comments:

Simon Kitururu said...

Polenin sana!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

pole sana Kaka Serafim na Da Yasinta!

bila shaka tutajua chanzo cha moto kama ni hujuma ama 'mapenzi ya Mungu'!

Anonymous said...

"POLENI SANA NDUGU ZANGU NA MUNGU AWAPE MOYO MKUU NA USHUJAA WA KUKABILIANA NA UGUMU WA MAISHA KWA KUWA IBILISI HANA JEMA SIKU ZOTE.
--------------------------------
Ninajua vema, Ee Yehova, kwamba njia ya mtu wa udongo haimo katika uwezo wake. Mwanadamu anayetembea hana uwezo wa kuongoza hatua yake.-Yeremia 10:23.
--------------------------------
R.Njau

sam mbogo said...

Pole sana,kaka yake mtu. huo lazima ni mkono wa mtu!!! lazima twende kwa mganga,ama sumbawanga,bagamoyo,au tanga,inauma sana.(utani jamani kaah) kaka S

Mwanasosholojia said...

Pole nyingi kwa brother na kwako sisy. Nafikiri sasa umefika wakati wa kungalia kwa undani namna ya kuyadhibiti majanga haya kabla ya kutokea ikiwa sambamba na kuboresha idara za zimamoto..ni kama vile hazipo!Moto unatokea na kuunguza karibu vitu vyote kana kwamba zimamoto hawapo!

emuthree said...

Tunampa pole sana kwa mtihani huo wa kimaisha!

EDNA said...

Pole sana kaka, na wengine wote walioathirika na ajali hiyo ya moto.

Anonymous said...

Pole sana kaka, ila Yasinta ofisi ya kaka haijakaa vizuri, saidia basi kuboresha hiyo ofisi. Hata kama anashona viatu lakini pawe pasafi.

Anonymous said...

Bwana anajua njia ya kutoa na kumnyima mtu,siajabu Mungu alijua kuwa hayo yatatokea. Tujipe moyo Mungu ana namna ya kuwarudishia kile kilichopotea. Pengine na hilo ni janga kati ya majanga ya mwezi huu.wadau tuna budi ya kuwachangia chochote. Poleni sana

Mija Shija Sayi said...

Poleni sana, Mungu atawarudishia kile kilichopotea..

Pamoja daima.

John Mwaipopo said...

poleni sana wote (nikiwamo na mimi maana ndio shopping center yangu. naenda kwa mguu tu)

ama baada ya pole unazi kidogo. yasinta inaonyesha kaka yako na mimi tunaizimikia DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote kwa kuwa nasi katika kipindi hiki ..Na kikubwa hapa twamshukuru Mungu kuwa maafa hayajawa mengi..kwani ajali ikitokea basi kilichobaki kubangaiza tena na kuanza upya ..hata kama ni kwamba mwanzo mgumu lakini hakuna jinsi... ila duh! huu ni mwenzi wa majanga kwelikweli