Friday, September 9, 2011

CHAKULA CHA MCHANA WA IJUMAA YA LEO...KARIBUNI TUJUMUIKE NDUGU ZANGUNI!!

Ni kawaida yetu kila Ijumaa kufanya manunuzi ya chakula kwa wiki nzima. leo nilipokuwa dukani nikakuta mahindi haya . Sikuweza kuyaacha nikayanunua ili yawe mlo wa mchana . Hapa nimeyaandaa tayari kwa kuyachemsha......


.....na hapa ndipo tayari nimeyapanga kwenye sufuria na yanachemka taratibu...
......dakika kumi baadaye walaaaa... mahindi tayari yameiva na sasa.......




.....mwanadada kwa raha zote anatengeneza barabara ya kwenda Afrika....nadhani wote mnakumbuka mchezo huu wa kula mahindi. Yaani enzi hizo miaka orobani na saba wakati wa utoto . Kaka, dada au hata baba au mama wakati wa msimu wa mahindi kulikwa na msemo au mchezo wakati mkila mahindi basi wanasema "leta muhindi wako nikutengenezee barabara ya kwenda LITUMBANDYOSI". Na kwa akili ya utoto basi unampa tu kumbe mwenzako yale mahindi anakula na anakuachia mistari miwili tu...hahaaaaaa!! leo nimekumbuka mbali kweli. KARIBUNI JAMANI NA IJUMAA NJEMA PIA:-)

5 comments:

Sam mbogo said...

Da,Yasinta,ilohindi kweli au basi tu,hindi ulaya!! lainikamanini,hata kutengeneza njia ya kwenda bagamoyo itashindikana,hayapukuchuliki hayo.I la hatamimi nayapenda sana kwa ulaini wake. ningekuwa najuwa jinsi ya kuruka na ungo ungeniona hapo sasa hivi lakini sayansi hii sikufanikiwa kuipata,inaniuma sana,inabana matumizi.kaka S.

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

EDNA said...

Natamani hayo mahindi mweee.

Rachel Siwa said...

Duhhh da'Yasinta kaka yangu alikuwa anapenda kweli mchezo huo wa kutengenezea wenzie njia, hahahhaa umenikumbusha mbali sana, sijui watoto waleo kama watakubali naona patachimbika.Bado hamu haijakuisha tuu, Nyumbani hukukuta msimu wa mahindi?.Kula kitu roho inapenda wangu nami nimeyatamani haswa.

Anonymous said...

Sisi haturii viakula via kulambala via hotelini,tukulya viakula via kusipa via kupika weniewe.



R.Njau