Ndiyo, ndiyo! Ndugu wasomaji wa blog ya Maisha na Mafanikio kile KIPENGELE chetu cha marudio ya mada, picha, au nisema MATUKIO MBALIMBALI ambayo huwa kila JUMATANO...leo nimeona tuangalie picha hizi za huyo madada. Ambazo tulishawahi kuziona hapa. Ila leo ana swali moja maana si mnajua huyu ni Kapulya...Je ni picha gani wewe imekupendeza? unaweza kutoa sababu pia.:-)
Hapa mwanadada ametinga kimgolole/kimasai.
Hapa nilikuwa nafikiria nifunge mtindo upi? Kabla sijaamua picha ikapigwa...kaaziii kwelikweli!!!
Hapa nikaona nikumbuke nilipokuwa mdogo maana nilikuwa napenda sana kufunga nguo (Lubega) shingoni. Lubega na ndala si mbaya au mnasemaje.... Ahsanteni wote TUONANE TENA JUMATANO NYINGI /IJAYO KATIKA KIPENGELE CHETU HIKI CHA MARUDIO YA MATUKIO MBALIMBALI!!!!!
19 comments:
Mie nimeipenda zaidi hiyo ya kwanza na na bado najiuliza ni kwanini ingawa moja ya kilichonipitia mukichwa ni jinsi pozi lako lilivyo naupole wa kibikira kiinosenti fulani.
Ila pia nasikia Ukijipenda mwenyewe sana kuna wahitimishao MTU unajidai au angalau wengine kwako sio MUHIMU.:-(
simon mhhh!!!
mimi nimeizimikia picha ya pili. kwa sababu ina uhalisia, yaani haina kujiandaa ama wengine wanasema haina mapozi. inahusisha matukio mawili. mosi ni kama ulivhyosema kuwa ulikuwa unafikiria mtindo gani wa kuifunga hiyo nguo. pili ni mkono wa kushoto ulikuwa unafikiria nywele uzitupie wapi. hakia wadada mna kazi
sifa ya mgolole Da Yasinta watu wanasema huvai na kitu ndani!!,kama wamasai sijuwi nawewe nihivyo hivyo au ume ongezea kautaalam kako ka kuwa na kajinguo fulani, halafu juu ndo mgolole? siyo mbaya kuji penda ila kujipenda huko kusiwe kero kwa watu wengine.kiukweli wewe ni mrembo asilia. kaka S
Zote nzuri lakini mimi nimeichagua hiyo ya kufunga shingoni, sababu imekutoa kiutoto/mwali haswa pia umenikumbusha mbali sana.Sikuwa napenda kufunga kanga/kitenge kiunoni, nilikuwa napenda kufunga hivyo kwa sababu zangu, Mhhhh nitawaeleza sikunyingine.....
Dada, wa swahili na waswahili,umenikumbusha,na mimi enzi za utoto,mchezo wa baba na mama,au kujipikilisha.wakati tukicheza wasichana wengi wali funga sana lubega halafu mkicheza mchezo wa baba na mama , walikuwa wana shikilia hizo lubega zao huoni ndani. kaka S.
Simon! nanukuu "moja ya kilichonipitia mukichwa ni jinsi pozi lako lilivyo naupole wa kibikira kiinosenti fulani." mwisho wa kunukuu una hakika huo ni upole wa ....
Na kuhusu kjipenda sana mwenyewe...miminaamini kuwa usipojipenda kwanza mwenyewe basi hakuna atakayekupenda...Lakini asante kwa hilo ulilolisema ntapunguza kujipenda ili MTU asifikiri najidai...LOL
Kaka John! Umenichekesha kweli:-) wadada tuna kazi ila si wote...
Kaka S! Kaazi kwelikweli hiyo itakuwa siri yangu:-) Halafu nasema ahsante kwa wasifa ulonipa.
Rachel: wewe huachi vituko...nasubiri kwa hamu kweli kujua kwa nini ulikuwa hupendi kufunga kanga/kitenge kiunoni...
Kaka S. hakika kuna kitu kinaniambia wewe ni ....hapo jaza wewe . Eti tulikuwa hatuoni ndani duh! kazi kwelikweli..nawasifu hao wasichana kwa kukamatia huo mgolole.Mambo ya utoto safi sana...
@Kapulya: Inawezekana nimechanganya sura ya huzuni na UPOLE aisee mdada!
Sijahitimisha lakini kwani ni hiyo picha yakwanza ndio fulu sumaku kimnaso.
Na hilo swala la kujipenda,...
... nadhani hata akina YESU labda walikuwa wanafanya kupenda wengine kabla ya kujipenda ukifikiria ,...
.... labda ilikuwa ni kimpindo fulani ambao ni kinyume na usemacho ingawa kuna wanukuuo mpaka BIBLIA kwamba penda gwaguro lako kabla ya kupenda gwagulo la mwenzio,...
... na wanasababisha hata kwenye ndege wanadai kitu ikidata jiokoe hata kihewa kabla haujamsaidia mwenzio kupata kipumulio hata kama huyo ni mwanao!:-(
Ukweli mie nilipopitia mara ya kwanza blog yako na kuona picha yako hiyo ya kwanza juu nilipatwa na mshtuko wa kuona kama Adamu alipomuona Eva kwa mara ya kwanza, baada ya kusoma profile yako,oh nikajihurumia, kumbe tayari Adamu keshakuona. Ni mrembo halisi wa Songea wanapenda kuvaa kanga pia kama huku kwetu Unyamwezini madada zetu wanavyopenda kanga.
Zote nzuri umependeza sana my dear
Mımı mbona sıku nyingı nımeshakukubalı
Ile ya kwanza imenikumbusha mbali sna kwani home watoto wa kike wakiwa wadogo ndo hufunga hivyo.Ndu umbunifu sana.
Bigup kwa kuenzi hayo mavazi.
Na kujipamba kwenu kusiwe kule kusuka nywele kwa nje na kule kujivika mapambo ya dhahabu au kuvaa mavazi ya nje, 4 bali kuwe yule mtu wa siri wa moyoni katika vazi lisiloharibika la roho ya utulivu na ya upole, ambayo ni ya thamani kubwa machoni pa Mungu.
--------------------
R.Njau
Mimi hiyo ya Lubega naipa asilimia 100.. jamani utasema una 16..?!!
duh..imbombo ngavu!
HAYA CHE JIAH NASEMA HIVI.
Nahitimisha kuwa piha ya kwanza ndo illiyileta mjadala huu kisa cha picha,hivyo najuwa mwafrika huwa anapojipanga kwakweli anapendeza hata kama ungevaa ile kanini wewe kapulya unaijua ungependeza tuuuuuuu sasa basi unataka kuleta tatizo la picha kwani umetasikia maneno ya kaka yako mbogo kama angesema mmakonde ungekuja mbogo sana ila kwavile wa kunyumba ahaa singilii kwamaana hiyo picha ya kwanza nami nimeshinda
asante mchango wangu ni huo PICHA YA KWANZA Habari no hiyoooo
Mfungo wa hiyo picha ya chini pia kulikuwa na wakati nilikuwa nashuhudia ukiwa ni maarufu sana kwa watoto wa kiume waliokatwa jando !
R. Njau unamfahamu huyu mwenye blog? unamfahamu kiasi cha kumshurutisha kufuatilia maoni yako? ha ha ha ha ha una nakisi weye ndiyo maana ukachangia nje ya mada kama mie niliyevutiwa na maoni yako bwana kijeba. ha ha ha ha
Ndg Markus;
Asante sana kwa maandishi yako.Madokezo hayo ya biblia yanawapongeza wanawake wote kwa jinsi wanavyojipamba lakini inawaelekeza kuwa wasisahau kuipamba mioyo yao kulingana na kanuni za kimungu.Kama mwenye blogu hakupendezwa na hii mistari ya biblia namsihi awe mvumilivu kwa kuwa kila mdau anatoa mchango wake kulingana uwezo wake wa kuifahamu mada iliyopo mezani.
------------------
R.Njau
Umependeza, mimi kwangu hata ukivaaje naona unapendeza sana tu
Post a Comment