Friday, September 30, 2011

NIMEONA NISIWE MCHOYO:- KARIBUNI TUJUMUIKE MLO WA MCHANA HUU AMBAO NI SUPU YA SPINACHI!!!

Nimerudi toka kazini huku nikawa na hamu kweli kweli ya supu...baadaye nikakumbuka nina spinachi. Kwa hiyo hapa, ni supu ya spinachi ambayo ni:- spinachi, maji, na chumvi. Inaandaliwa kwa dakika 10...Kwa anayetaka anaweza kuweka nusu kikombe cha maziwa au cream. na katika kula unaweza kula na kipande cha mkate pia yai moja la kuchemsha. Ila Kapulya hapendelei sana vitu hivyo kwa hiyo anakula kama ilivyo. KARIBUNI SANA TUJUMUIKE!!!!

18 comments:

Simon Kitururu said...

Sijawahi kuonja hiyo kitu!

Ila imekaa kiafyaafya vile ingawa sina uhakika kama inatufaa siye walevi!:-(

isaackin said...

he hee,supu ya spinach na hang-over hii dada??
ngoja kidoogo ntarudi kunywa

EDNA said...

YAM YAM,NITAKUTAFUTA BAADAE DADA.

Yasinta Ngonyani said...

Simon! Basi nakushauri ujaribu au panga safari uje nitakutenezea utaacha kula vyakula vingine vyote. Ni kweli ina afyaafya...Hata kwa walezi ni inapanda:-)
Kaka isaackin! umenichekesha kwelikweli ...haya ukirudi utaikuta na utaifurahia...

Edna ni kweli YAM YAM, nitafurahi ukintafuta:-)

ISSACK CHE JIAH said...

MIE NIENGENEZEE SUPU YA MBELELE
HAPO TUNGEKUWA WOTE ILA NA HII KWAKWELI MIMI HUWA NATENGENEZA MWENYEWE KILA JUMAPILI NI SUPU MZURI SANA ILA MCHANA HAPANA INAWEZA ISIPANDE KAMA ALIVYONENA NDUGU YANGU ISAACKIN JUMAPILI HII NAFUATA FIGILI PALE SOKONI BUGURUNI NITAYARISHE KABISAA TENA UMENIKUMBUSHA
CHE JIAH ISSACK

Yasinta Ngonyani said...

Hivi ni jumapili leo? mie nilidhani ni IJUMAA? mmmhh sijui ni nani katingwa hapa...Hiyo figili usinnyime sijui italiwa na nini?

sam mbogo said...

umenikumbusha supu zaaina mbalimbali. kuna supu ya kongoro,supu ya utumbo wa mbuzi,supu ya mkia,supu ya kichwa,supu ya kuku wa kienyeji, supu ya ulimi, supu ya mapumbu ya ng'ombe/mbuzi, supu ya pweza,supu yasamaki wakuchemsha.katika hizi kiboko ni kongoro ikifuatiwa na supu ya nanii za ng'ombe na mbuzi,hasa kwa waonjaji wa pombe kama sisi.Kaka S

Yasinta Ngonyani said...

KakaS. Duh! ni kweli kuna supu nyingi zote hapo ziåpo juu ila hiyo ya nani hapana...nakumbuka siku moja nikiwa katika mizunguko yetu tukafika mpaka MTO WA MBWA na pale tukasimama na kupata supu ikaja hiyo supu ya nani we bwana weee bahati mbaya walikata vibaya basi harufu hiyo. Nakuambia nilipakua si mchezo na hamu ya supu yote ikaisha ....sema zaidi sasa!!

Simon Kitururu said...

Yasinta unataka kudai NANIHII zinanuka?

Yasinta Ngonyani said...

Simon! za hiyo supu ya huko mbwa wa mto yaani ya mbuzi ..ni kweli ilikuwa inanuka ..SAMAHANI LAKINI NI KWELI:-( Kwani wewe umewahi kula?

Simon Kitururu said...

Kwa walevi kama mimi wa KITANZANIA ni vigumu kuruka hiyo kitu!:-(

Ila labda KUNUKA na KUNUKIA ni pua ya mtu!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Oh! Simon unaposema mlevi una maanisha nini? ni kweli pua zetu zipo tofauti mwingine anaona inanuka na mwingine anaona inanukia.

Simon Kitururu said...

Si ulevi ni ulevi tu Yasinta?

Rachel Siwa said...

Asante da'Yasinta kwa Supu, kwangu naona bora hivyo kuliko na mathiwa tena, mmhh mimi si mpenzi wa maziwa. Jamani kaka S [Sam] mimi sikuwanajua kama kuna Supu ya nanihii, kumbe kaka Kitururu na da'Yasinta mmesha onja,nilitamani kuonja lakini da'Yasinta umenitisha.
@Kaka Isaac ukikuta tumemaliza itabidi unywe ya Maharage!!!!!!!!

isaackin said...

duh hiyo nikikuta mmemalizza ntafurahi wacha.
hizo supu za p*mbu za ngombe basi kipindi fulani nimepita mitaa ya suga ray nje nikakuta jamaa wanazichoma za nguruwe mbuzi na ngombe ebwana zilikuwa zimenona kweli kweli mi sikujua kitu gani nikaagiza sahani top mix na pilipili kibao baada ya kufakamia ndo nikauliza nini hiki ndo nikaambiwa ni mbupu za wanyama hao kutapika nikataka kumeza nikataka.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hapo sawa

Unknown said...

Ah! aH! ah!

Bennet said...

Hizo nani hii za ng'ombe na mbuzi kwa sie wazoefu tunaziita ASHUA, ISAACK kumbe unakuja suga ray siku hizi inaitwa KISUMA