Saturday, September 10, 2011

poleni sana ndugu zetu wa zanzibar kwa msiba huu mkubwa!!!

Meli ya Mv Spice iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja imezama usiku wa leo maeneo ya Nungwi ikiwa na abiria wanaokadiriwa kufikia zaidi 1000, wengi wao wanaofiwa kufa maji.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, vinasema meli ilikuwa imepakia mizigo na nabiria kuliko uwezo wake.
Poleni sana ndugu zetu wa Zanzibar, Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, zaidi tuzidi kumuomba yeye ili manusura wengi wapatikane. Ameeni
picha na maelezo toka hapa.

2 comments:

Rachel Siwa said...

Poleni sana Wapendwa wetu Zanzibar, Mungu awatie nguvu kwa wakati huu mgumu.

sam mbogo said...

Tukopamoja,mungu awape nguvu,wote waliofiwa,na moyo wa upendo,kwa kipind hikicha majonzi makubwa.pia tunaomba mungu awajalie,busara nahekima watakao shughulikia chanzo cha ajali. kaka S.