Thursday, September 29, 2011

WAKATI WA WATU KUNUNA UNAKARIBIA, VICHEKO VYOTE NA TABASAMU VYA SUMMER VYAFIKIA UKINGONI!!!/HÖST/AUTUMN = MAJIRA YA BARIDI YA KUPUKUTIKA MAJANI BRRRR!

Mmmmh! Kazi inaanza sasa. Kaziiiii kwelikweli, maana mtu unavaa nguo na mwisho unaonekana kama una kilo elfu kumi. Haya ngoja niache.

Ila pia ni wakati mzuri sana hasa miti inapopata rangi nzuri kama huu hapo juu inapendeza kusema kweli...Tatizo humwoni mtu ...pia ni kipindi kizuri kwenda mstuni kuchuma uyoga ila unatakiwa kujisitiri kweli .... huu mti rangi zake nipezipenda sana ila muda si mrefu majani yote yatapukutika na kuuacha na vijiti tu au mti unakuwa "uchi":-(


8 comments:

nyahbingi worrior. said...

Dada habari za siku.

Dada Yasinta,niko katika mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya http://blogutanzania.blogspot.com/ kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.

Luiham Ringo.

nyahbingi worrior. said...

Habari za siku.
Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
http://blogutanzania.blogspot.com/
kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
Ahsante
Luiham Ringo.

ray njau said...

AFYA NJEMA NA BARAKA TELE!!

Bennet said...

kwa hiyo baada ya muda mtakuwa kama mpo kwenye friza

John Fisher said...

Inaonekana hali nzuri kwa sasa halafu muda mfupi baadaye barafu na theluji. Kwa kweli Mola kaibariki bara letu la Afrika.....

John Fisher Kanene

Bennet said...

Hivi Dada Yasinta unawezaje kutambua uyoga wenye sumu na ule ambao hauna sumu, maana nishasikia kesi nyingi tu za watu kula uyoga wenye sumu baada ya kuuchuma msituni

Yasinta Ngonyani said...

Wote asanteni kwa kutochoka kipita hapa na kuacha kitu.----Kaka Bennet niwapo mstuni kwa ville najua aina tatu tu basi nachuma hizo ni "Chantarelle" ni ule uyoga wa njano au orenji, karl johan, sijui jina la kiswahili na pia kuna jamii ya "chantarelle" ambao ni blauni na upo kama mrija vile. Zaidi ya hapo sichumi uyogo mwingine. Ahsante kwa kutujali.

Simon Kitururu said...

Mtoto Mzuri wewe! Bado naangalia picha! kwa hiyo usiniulize umeandika nini!:-(