Tuesday, April 21, 2009

MASUALA YA UBAKAJI NA KUPIGA WANAWAKE LINAZIDI KUWA KUBWA

Dunia imeharibika watu wanazidi kupotoka, angalieni haya mambo yanavyozidi kuenea. Mambo kama vile unyanyasaji, kuna ukatili mwingi sana hapa duniani ambao zaidi ni juu ya wanawake na watoto. Hao ndio wanaopata shida zaidi. Ukatili ni kinyume na haki za binadamu na uko ukatili wa aina mbalimbali. Kuna vipigo, matusi, kulazimishwa kufanya mapenzi, kuna baadhi ya mila potofu kama vila ndoa za lazima, kuolewa ukiwa na umri mdogo, kurithi wajane nk.

Bado sijaelewa ni kitu gani kinawafanya wanaume wengine wawapige wanawake. Kwanini umpegi mwenzi wako? Je usipompiga uanaume wako utapotea? Na kuna raha gani kumpiga mwenzako kama mnyama? Na hata mnyama hairuhusiwi kumpiga. Hili suala la kubaka utasikia raha gani wakati mwenzako anapata maumivu yasiyo kifani. Na pia hajapenda.

Je? Mnafikiri hii inaweza kutokana na wengi wanaume wanafikiri wao ndio waamuzi wa kila kitu ndani ya nyumba? Na kwa nini watu wawili waliooana wasikaa chini na kujadiliana na kuona kosa liko wapi. Je? Ingekuwa kinyume ingakuwa sawa?

Au labda wengi wanafuata maandishi haya:- Mwanzo 3:16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako, kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumea, naye atakutawala.

Ndugu wasomaji/wanablog naomba mnisaidie kunipa jibu.

22 comments:

Mwanasosholojia said...

Dada Yasinta na Baraza zima la MAISHA, nimevutiwa na mada hii, na hongera sana kwa kuitundika barazani!Binafsi nachukulia suala la kupiga mwanamke/ wanawake kama upungufu wa fikra na ubugikwaji mkubwa wa "mawazo mgando" kuwa wanawake labda ni chombo tu cha starehe, wasaidizi, vijakazi, watwana etc. Jambo hili siliamini kamwe pamoja na kwamba mimi ni mwanaume. Wanawake, kwa mtazamo wangu, wanapaswa kuheshimiwa na kuchukuliwa katika nafasi mahsusi kwenye jamii yetu. Hili litasaidia pia hata kubadilisha mitazamo katika mila nyingi (pamoja na dini yenyewe)ambapo mwanamke huchukuliwa kama mtu aliye nyuma ya mwanaume. Sidhani kama kuna raha yeyote ambayo mtu anaweza kuipata kwa kumtwanga mke au mchumba wake, halafu kesho anamtambulisha mbele ya rafiki zake! Sio kumdhalilisha yeye, ni kujidhalilisha wewe. Ni kama vile wewe uwe na mwanamke au mchumba ambaye imetokea ana nguvu kukushinda wewe, siku ukichokoza tu, anakutwangaaa!Inaleta picha gani hii? Binafsi nafikiri naweza kuwa mfano (sijifagilii hapa jamani, naiongelea nafsi yangu), nimeishi na mke wangu toka 2003 hadi leo sijawahi kunyanyua mkono wangu na kumchapa hata kibao!Hasira huwa zinakuja, lakini daima naamini mazungumzo ndiyo njia ya kutatua matatizo na si vipigo! Ni kweli wanaume tunapaswa kubadilika, lakini pia tuziongelee hizi mila na dini zinazowaona wanawake kama vyombo!Hapo ndipo hali hii itabadilika. Roma yenyewe haikujengwa kwa siku moja!

Fadhy Mtanga said...

Kwanini?
Inapigwa ngoma siyo mwanamke.
Hao wanaowachapa wanawake ama kuwabaka lazima wanayo matatizo kisaikolojia.

Anonymous said...

Du hii mada ni nzuri sana kujadiliwa, lakini kabla ya kuijadili hii mada mie nimpe pongezi mkuu Mwanasosholojia (Mathew Agripinus Asenga). Mhh ningeshangaa Mathew umpige yule shemeji yetu, kwanza jinsi alivyo mrembo, kaka umenikumbusha mbali sana Mzumbe, mabibo hostel.

Unknown said...

Mambo ya kupiga mwanamke yamepitwa na wakati. Ingawa wapo wanaume nao huambulia kipigo kutoka kwa wake zao pia.
Mwanaume mstaarabu hapigi mke kwa mangumu kwa kumshushia mazawadi ya uhakika.

Upendo daima

Koero Mkundi said...

Ndio maana naogopa kuolewa........
wanaume wa siku hizi washari shariiii......

Anonymous said...

mhh Koero una hakika na unachokisema? ukianza kuogopa ogopa mambo utashindwa kufanya mambo kwani kila jambo/mtu ni tofauti. sina hakika kama wanaume wa siku hizi ni washari au wanawake wa siku hizi ni wasumbufu!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

koero ukijiandaa kupigwa utapigwa tu!

mbona matatizo ya wanaume hayaongelewi? tunakuwa kama mijitu ya hatari jamani na wakati ni lazima wanawake waishi nasi hata tusipowatongoza watatutongoza sisi!

thats life

Anonymous said...

Mkuu Kamala umesema, kila siku ni wanawake tu wanaongelewa utadhani wanaume hatuna matatizo vile. du hiyo kali ya "tusipowatongoza watatutongoza sisi" huwa wajanja wa mjini wanasema "watajigonga" ua watajileta! Koero wewe endelea kuogopa kuelewa, lakini sisi tunakusubiri ufikishe 33 na mambo yawe hayaeleweki, kama usipomtafuta hata mume wa mtu!! teheteheteh

Mwanasosholojia said...

Mheshimiwa Kamala na mkuu Anonymous wa April 22, 2009 2:31 PM, mimi sidhani kama ni suala la kutoongelea matatizo ya wanaume. Ni kweli nasisi tuna matatizo, lakini ndio tutumie kigezo hiki kama njia ya kujustify kutoongelea matatizo ya msingi yanayowakabili wanawake? La hasha! Nafikiri tunapaswa kubadilisha mtazamo wetu (tena sisi tulio na nafasi ya kutoa nuru kwa wengine). Leo Mheshimiwa Kamala pamoja na Anonymous wa April 22, 2009 2:31 PM kama sisi tunakuwa na mtazamo huu (sipendi kuuita hasi, labda mtazamo wa kutoona hili kama moja ya matatizo ya msingi kujadiliwa), yule mwanakijiji wa kule Epanko, Mahenge- Morogoro, au yule wa kule Kamachumu vijijini Bukoba atakuwa na mtazamo gani. Mimi naona hapa kuna tatizo, na tatizo hili lina vyanzo mbalimbali. Masuala ya Gender ni magumu kuyapatia ufumbuzi kwa kuwa gender yenyewe haina maana ya biological/ physical difference, rather gender ni social construction. Mitazamo kama hii ndiyo inayopelekea ugumu tunaouona katika kuona umuhimu wa wanawake kufanyiwa yale yalio na haki kama binadamu wenzetu.

Sikatai kuwa kuna wanawake wengine wakorofi (kutokana na socialization na any other socio- economic attributes), lakini ukweli unabaki pale pale, ipi ni njia nzuri ya kutatua migogoro ndani ya nyumba au kati ya wapendanao?kudundana?kuumuana uso?hapana ndugu zangu. Ukisikia watu wanasema ametimiza jubilei katika ndoa zao ujue wamefanya kazi, ikiwa ni pamoja na busara katika utatuzi wa migogoro ndani ya nyumba. Kama nilivyosema katika mchango wangu wa awali, kugombana na kukwaruzana na hatimaye kuingiwa na hasira ni jambo lisilokwepeka katika ndoa, lakini mnalichukuliaje linapotokea? Hilo ndiyo suala kubwa.

Nashukuru Ananymous wa April 21, 2009 8:17 PM kwa kunipongeza (na kunifagilia, teh!teh!), naomba nikwambie kuwa mimi ni yule yule, na natumaini na wewe pia hutumii mabavu unapokabiliana na mke/mchumba wako, teh!big up sana!

Koero dada yangu, usiogope kuolewa
Katika ulimwengu, Mume Mungu atowa
Kwa mtazamo wangu,lazima tu utapewa
Kubwa dada yangu, mapenzi hupaliliwa!

Nawasilisha!

Anonymous said...

Mwanasosholojia, nianze tu kutumia mabavu kupiga ubavu wangu, si nitaumia mwenyewe!! endeleza hizo tabia njema ndugu yangu, mie nakufahamu fahamu vizuri tu, mwanakwaya wetu pale Mzumbe,Yombo kama sikosei, na sasa hivi nadhani majuu!

Mwanasosholojia said...

Teh, ahsante tena Anonymous wa April 23, 2009 12:25 AM, nafurahi kuona "unanifahamu fahamu" kama ulivyosema. Ni kweli huwezi kutumia mababu kupiga ubavu wako, nafikiri ukifanya hivyo si tu utaumia mwenyewe, bali unaweza hata kuwa na kovu la maisha! Hongera ndg yangu, tuendelee kuwa nuru kwa wengine, siku moja (hata kama itakuwa mamia ya miaka, wakati hatupo tena duniani), mambo yatabadilika, na dunia itakuwa sehemu nzuri ya kuishi kwa kila mmoja wetu, awe mwanamke au mwanaume!

Mwanasosholojia said...

Kunradhi wadau, mkono uliteleza nikaandika neno mababu badala ya mabavu. Naomba neno mababu lisomeke mabavu katika mchango wangu uliopita!

Koero Mkundi said...

Hivi kumbe kuolewa ni lazima eee?
Mie sikujua......

Mwanasosholojia said...

Mmh dada Koero huishi vijambo
Hoja mpya hii unaileta sasa, ndani ya hoja mama, kuolewa ni lazima au hiyari? labda Kibaraza cha Maisha au hata ukumbi wa VUKANI ulipachike hii waziwazi ili tuanze kuijadili baada ya kupata mahitimisho ya hoja hii ya "mangumi" iliyo mbele yetu

Christian Bwaya said...

Tunaweza kabisa kukwepa kuwadunda akina mama.

Hata kama wengine wanayachukulia mapigo kama tendo la upendo.

Zipo jamii zetu zimewaaminisha wanawake kuwa wasipodundwa ama kugombezwa gombezwa hawapendeki. Kwa hiyo unakuta tatizo linakubwa kubwa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tatizo sio wanaume bali tatizo ni la kimfumo. tunashindwa kubadili ya kale na ya sasa. tukiliweza hilo, wanawake watapumua na wanaume. hata hivyo unyanyasaji wa kijinsia ni dili kwa kiasi fulani ndio maana tuna TGNP, mewata, wama, gender clubs nk. waajiriwa wa mashirika hayo wote wanalipwa vizuri na kuendeleza familia zao. idumu midundo

Mwanasosholojia said...

Kumbe mheshimiwa Kamala unajua tatizo ni la kimfumo!tufanyaje sasa?tuendelee kuliangalia tu kwa sababu wanaharakati uliowataja watakosa "uhakika wa maisha"?Sidhani ndg yangu! Hata tukiiangalia kihistoria, babu zetu sio kwamba walikuwa wanadunda tu wanawake kama mangoma!nafikiri wengi walikuwa na utu, ambao siku hizi nafikiri unatoweka kwa kiasi kikubwa miongoni mwetu!Sisemi kuwa zamani hakukuwa na unyanyasaji kwa bibi zetu, hapana,unyanyasaji ulikuwepo pia, lakini Mheshimiwa Kamala, angalia huo mfumo ulioutaja unatupeleka wapi sasa, jaribu kuangalia historically, hasa baada ya kuingia kwa wakoloni, maisha ya watu yalivyokuwa yakibadilika kwa kasi. Haya ingia katika zama hizi za utandawazi, si tunaiga vitu kutoka kwa wenzetu wazungu?Wao wanapiga wake/ wachumba zao kama sisi?na ikitokea mwanamke anadundwa, na hata mume wake, jamii ya ulaya inalichukuliaje hilo? Tunasoma na kuona kila wakati, mwanaume lazima ashughulikiwe! Sidhani kama ni vyema kusema IDUMU MIDUNDO, nafikiri tuseme zidumu fikra za mabadiliko chanya ya kupinga unyanyasaji wa wanawake!

Anonymous said...

yes but is that a blackman thing? ie you do as your told woman type of thing?

ps i am not racist

just things i see and yes i am a man

Mwanasosholojia said...

Mr Anonymous (April 23, 2009 3:20 PM), the issue here is not basing on race! I just gave an example within parameters of my explanation and the problem at hand. If you caught me correctly, I started by saying we have the tendency of copying things from Europe or America (perhaps following the generalization that they are points of reference!, I then asked should/shouldn't we copy their approaches towards women, especially physical/social abuse? I didn't mean that we blacks are the only people on earth who normally beat our fellow humans, I have just exposed the other side of the coin, it is a matter of decision here, as there is no universal reality!always we have multiple realities!

Koero Mkundi said...

Kule Nchini Kenya Wanawake Wanasheria waliobobea wameungana na kuanzisha kitu kinachoitwa FIDA...
jamani hiyo muisikie ikija Bongo wanaume wote mtashika adabu, yaani hakutakuwa na mwanaume atakayethubutu kumwambia mwanamke Shhhhh!!!!....wewe anajipenda au....
FIDA inawahenyesha wanaume wakorofi nchini Kenya usiseme.
Sio hii TAMWA yetu au TAWLA hakuna kitu....wenzetu wame advance...hawataki mchezo kabisa

Simon Kitururu said...

Hili swal MMhh!:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

niombe radhi kwa kuchelewa kujibu. niko mikoani safari kibao na net ndo hivyo.

tunahitaji kujitambua na kurudi kwenye utu na sio sheria za kukomeshana na kutambuana. sisi kama wanaume, tunahitaji wanawake na wanawake hivyo hivyo. tukijitambua migogoro itaisha.

sio kukimbilia utamaduni wa wazungu wa biblia na bikra maria, bali tuuone uhalisia ili tuishi maisha mema.

kwa mfano, wengi tunafanya ngono na hatujawahi kufundishwa ngono wala kujifunza, kwa maana hiyo hatuijui na hatuifurahii na hivyo ni chanzo cha matatizo na kumbuka ni msingi wa ndoa.

ni lazima tujadilianna tujifuze maisha ya ndo na jinsi ya kubebeana na faida zake.

tuwe na vittuo vingi vya ushauri kama kile cha kwetu cha jitambue, bahatimbaya hatujulikani, hii ndilo suruhisho