Thursday, April 30, 2009

UCHUNGU NA FURAHA

Kwa nini ni rahisi kuwa na furaha?
Kwa nini uchungu ni mzito?
Kwa nini kuna furaha kidogo?
kwa nini kuna uchungu zaidi?

Au kwa sababu tunathamini/pendezwa na furaha wakati tunapofikiwa na furaha?
Au kwa vile tunayanyenyekea maisha?
Au kwa vile tunalazimika kucheka?
Au Labda kwa vile tunalazimika kulia?

SIKUNJEMA KWA WOTE

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

define uchungu.

define furaha

Fadhy Mtanga said...

Furaha kitu muhimu,
Si kwa awamu na zamu,
Maisha ya mwanadamu,
Yanahitaji furaha.

Uchungu huwa mgumu,
Ingawa yatulazimu,
Uchungu una wazimu,
Hatuwezi ukimbia.

Ni hayo tu!

Yasinta Ngonyani said...

Kamala, Naona mtani wangu Fadhy kakujibu nini maana ya maneno haya. Ila nami nita(difine) kwa kiswahili sanifu:- Ni hivi Furaha ni kuwa katika hali ya ukunjufu wa moyo, uchungumfu Changamnka,kuridhika na kuwa na hili ya kustarehe.

Na Uchungu:-
Ni hisi anazokuwa nazo mtu baada ya kufikwa na na jambo la kuumiza k.v. kujikata, kujigonga au jambo la kutia huzuni k.v. kufiwa n.k.

Fadhy uliyoyaandika ni kweli kabisa.

Mwanasosholojia said...
This comment has been removed by the author.
Mwanasosholojia said...

Furaha kuitafuta kazi,
Kuihifadhi pia kazi,
Uipatapo yaonekana wazi,
Kwa watu wote na vizazi!

Hatuutafuti uchungu,
Ni kama vile ukungu,
Hauvumiliki uchungu,
Ajuaye ni Mungu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee