Monday, April 6, 2009

HAPA JE? ANGALIENI JINSI WATOTO WALIVYO HODARI KWA KUBUNI MAMBO


Je? wenzangu mnaona nini katika ubunifu huu hapo juu?

11 comments:

Albert Kissima said...

Picha hii imenivutia sana.Mimi nauona mduara mruri uliojengwa na miguu ya watoto hawa.kuna ninaowaona wako kwenye tafakari fulani hivi, kama vile wanamsubiria mwenzao atakayekaa katikati ya mduara na kuongea nao.
Naomba kuhoji kitu fulani.
Huu ni ubunifu wao kweli au ni utamaduni ktk jamii watokako watoto hawa?

Anonymous said...

mimi naona volcano. watoto wametengeneza sura ya mduara unaotengenezwa na mlipuko wa volcano.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee. siku zote usimkemee mtoto, mwache ajaribu, mohoji anafikiri nini. wanesema ubunifu umejaa kwenye akili zao

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Wanafalsafa na wanahisabati wanasema kwamba duara ndiyo "perfect body". Zitazame sayari, zitazame mbingu, tazama. Falsafa ya Kiafrika pia inasema kwamba Mwafrika hafi bali daima yumo kwenye mduara ambao hauna kikomo. Kwa mantiki hii hakuna mwanzo na hakuna mwisho. Watoto hawa wanaweza kuwa hawana viatu, na kwa mtazamamo wa Kimagharibi wanaweza kuonekana masikini lakini kuna ujumbe mkubwa katika picha hii. Ngoja niachie hapo, pengine mwanafalsafa Kitururu atachanganua zaidi.

Fadhy Mtanga said...

Picha imenivutia sana da Yasinta. Watoto wameiweka miguu yao kwa namna ya kupendeza hata kutengeneza duara.

PASSION4FASHION.TZ said...

Kweli watoto huwa ni wabunifu sana,hii picha ni nzuri sana nimeipenda,ombi kwako Yasinta naomba niitumie kwenye blog yangu kama hutajali,imenivutia sana.

Nuru Shabani said...

Kweli watoto ni wabunifu.

Anonymous said...

watoto nimewapenda sana!Wamejitahidi sana kubuni!Kwani mduara ni mzuri kama ni wenyewe wamebuni basi nawapa pongezi!

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni wote, ngoja nami nitoe maneno mawili matatu. Ni kwamba watoto ni watu wabunifu sana.Ni wengi watoto kama wanafanya kitu basi wanawakatalia kwa kweli inabidi tuache tabia hii na kuwaacha na tuone nini kitatokea.Na pia ni kweli inawezekana ni utamaduni wanasubiri babu au bibi aje na kuwasimulia hadithi

Anonymous said...

usengwili sana, picha ya mwina sana.

NURU THE LIGHT said...

nimeipenda sanaaaaaaa