Thursday, April 30, 2009

SALAAM ZA MEI MOSI = SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI KOTE

Kufanya kazi si adhabu bali ni heshima, kwani kila mtu yampasa kuisha kwa jasho lake.

Kuwa na bidii kutampa mtu cheo, lakini uvivu utamfanya mtumwa.

Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhila.
Atafutaye madhara, hayo yatamjia.

Kazi ndiyo msingi wa maisha. Maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi, tujenge tabia kujiajiri. Badala ya kujibweteka na kushinda vijiweni.
Nadhani wote tunajua ya kwamba ujuzi hauzeeki. Tunapaswa kuiga mifano ya wengine tufanyapo kazi zetu. Hata zikiwa za kawaida.

“Tazameni maua ya pirini jinsi yanvyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini, nawaambieni, hata Solomon mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama au mojawapo. Ikiwa, basi, Mungu huvika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho hutupwa motoni, je, hatafanya zaidi kwenu niny? (Mt 6:28-30)

“Asiyefanya kazi na asile” (2Thes 3:10). Ili tupate maendeleo katika maisha ya jumuia na katika maisha binafsi kila mmoja inampasa kutumia vipawa vyake na kufanya kazi kwa ubunifu na bidii.

Kazi ni kazi. Hata kama ni kazi ya kutifua ardhi, cha msingi inampatia mtu riziki yake halali. Tufanye kazi kwa bidii na maarifa ili tujipatie mahitaji yetu kiuhalali.

3 comments:

Born 2 Suffer said...

Nakumbuka wakati nasoma shule tulikuwa tunasheherekea sikukuu ya mei mosi kwa nyimbo hii. (Mei mosi leo sikukuu kubwa Tanzania). Siku hazirudi nyuma jamani wapi zamani.

Mzee wa Changamoto said...

Siku njema kwako Da Yasinta. Kama nawe ni kati ya wale ambao huisherehekea kwa "off", basi hongera. Mimi naisherehekea KAZINI

Yasinta Ngonyani said...

Born 2Suffer ni kweli kumbukumbu ni kitu muhimu sana. Na nakubalia nawe zamani ilikuwa safi zaidi.

Mzee wa Changamoto hata mie nasharehekea kazini pia.