Monday, April 27, 2009

USAFIRISHAJI WA FANICHA MFARANYAKI-RUHUWIKO


Mambo ndio hayo!!!!

10 comments:

Anonymous said...

Hizi TOYOTA (Datsun) za aina hii zilikuwa imara kweli kweli. Hizo fenicha zimezidi vipimo lakini bora tufike ushukuru mungu hukutani na askari na huyo aliyeshikilia fenicha huko hatazidiwa na nguvu ya msukumo wa fenicha wakati wa kukata kona maana inaweza kuwa historia tena. Bora hivyo kuliko kubeba kichwani ama kwenye toroli au kusukuma kwenye mkokoto (mkokoteni).

Yasinta Ngonyani said...

Umesema kweli hapa ilizidi kipimo na ni kweli bahati siku hiyo askari walishiba na halafu si unajua Mfaranyaki-Ruhuwiko si mbali.

Anonymous said...

Sio mchezo huo mzigo. Dada Yasinta huo mzigo ulisafirishwa likizo hii au kabla, maana nimeona hilo gari ni TZC. kuhusu askari wa usalama barabarani hapo ni bahati sana, maana toka Mfaranyaki mpaka Ruhuwiko kuna vituo viwili vya askari wa usalama barabarani, tena kitu kimoja kipo jirani kabisa na hapo walipokata kona kuiacha nji kuu ya kwenda Mbinga.
Pia hongera sana kwa kujenga, naona kazi iliyobaki kwako ni kuingia mkataba wa ugomvi na Tanesco tu. ni ajabu sana hizi sheria zetu, kwani wakisharuhusu watu au mashirika binafsi kuuza umeme wao kwa raia naamini ofisi za Tanesco zinaweza kufungwa Songea kwani kuna umeme wa kutosha kabisa wa maji kule abasia ya Peramiho na pia shirika la masista wa Chipole na wao wanao umeme ambao unaweza kuhudumia mkoa mzima na mikoa ya jirani kama Ntwara na Lindi.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu usiye na jina hiyo ilikuwa likizo hii. Na asante kwa yote, yah hapo hiyo issue ya umeme ila tutafika tu

Mzee wa Changamoto said...

Wote washasema, ila mie nimekumbuka saana hizo Hilux. Yaani ni balaa. Zinapakia mzigo mpaka unaona kuna mwanya kati ya kichwa na bodi, na bado inapanga mlima kama tambarare.
Ama kweli bongo tambarare.

John Mwaipopo said...

safi sana. ila ingawaje mmesema kuwa kuna askari usalama wa barabarani lakini ni mashaka kuwa hilo gari halitumii tena njia rasmi. Linatumia njia za vichochoroni. kwa namba hiyo TZC tayari lingeshadakwa hilo. au 'miundombinu' inatumika kuwapoza askari kila siku?

Anonymous said...

Mkuu Mwaipopo, umesema vema kwamba huenda hilo gari linatumia njia zisizo rasmi aka njia za panya. lakini mimi nadhani hiyo hoja yako ya pili ikawa nzito zaidi ni hiyo ya kuwapoza askari, kwa maana hapo ziliponunuliwa hizo fenicha ni jirani kabisa na barabara kuu, halafu toka Mfaranyaki ili ufike Ruhuwiko ni lazima ukutane na "vijiwe" viliwi vya askari wa usalama barabarani tana kimoja nina hakika kipo hapo hapo ambapo hilo gari limekata kona kuacha njia kuu, na kingine kipo eneo amalo ni kituo cha askari wa JWTZ. hivyo kusema kwamba hilo gari litakwepa sana sidhani na kama mhusika ataamua kweli kupita njia za panya, hana jinsi sana ya kuweza kukwepa kwani njia pekee mbadala anayoweza kutumia inapita jirani kabisa na makao makuu ya ofisi za usalama barabarani mkoa, hivyo ni rahisi kukamatwa na pia hiyo njia ya panya inazunguka sana kiasi kwamba itamgharimu mafuta mengi na matokeo yake "itakula kwake". na jambo lingine ni kwamba mji wetu wa Songea ulivyo mdogo ni askari wanamfahamu mpaka mmiliki, huenda hilo gari linamilikiwa na mkuu wa kitengo fulani katika hizo ofisi muhimu, kwani hata kama linalipia bima,TRA sidhani kama watakubaliwa waendelee kutumia hiyo TZC

Bennet said...

Minimeona hicho kijani kibichi na ndio kimenivutia kwenye picha.
hayo makochi ya mbao ngumu ni mkataba maana siku hizi kuna makochi hata mtoto analisukuma, ukilinunua baada ya mwaka limevunjika

John Mwaipopo said...

usiye na jina unanitamanisha nitembelee songea siku moja. alafu huwa natamanigi sana kutembelea songea. ipo siku tu.

Anonymous said...

Kaka Mwipopo, karibu sana Songea. uje ujionee mji wetu ulivyo. sio mkubwa sana ila msafi, pia hali ya hawa imetulia. Njoo ujionee bombambili, Ruhuwiko, Lizaboni, London, mji mwema, matarawe, msamara, matogoro, majengo, mfaranyaki, Ruvuma, mateka na mitaa mingine mingi. karibu sana ndugu yangu.