Saturday, April 11, 2009

UBUNIFU WA MICHEZO +KUWAFURAHISHA WATOTO


Tazama hapa mtoto alivyo na furaha kwa mchezo huu wa kukaa kwenye plastiki chakavu na kuvutwa na kamba kama yupo kwenye gari vile. Lisifuni jina lake kwa michezo, mwimbieni kwa ngoma na zeze. Zab 149:3

4 comments:

Bennet said...

Inanikumbusha sisi tuliokulia uswahilini kutokaqna na hali za maisha ya chini tulikuwa wabunifu sana. magari kuanzia ya mabati, makoa na mbao tulikuwa tunatengeneza, mipira tulikuwa tunafuma kwa manailon na kamba za manila, tulifinyanga sana kwa kutumia udongo tulioutoa buguruni malapa darajani. mabembea ya kufunga kamba kwenye miembe kwa kutumia matairi ya magari yaliyotumika, tuliangalia sinema za kuwapiganisha panzi (balangulu) na vuja jungu, manati tulizotengeneza wenyewe ilikuwa ni silaha muhimu ya kuwindia njiwa, ndege pori na kunguru

basi msinikumbushe enzi za utoto

Anonymous said...

YASINTA NAKUTAKIA GLAD PÅSK.YASINTA KUNA PICHA UMEPIGA NA KAKA ZAKO KUNA KAKAKO 1 PALE KAVAA SHATI LA NJANO KASIMAMA PEMBENI YAKO KAMA HAJAOA NAOMBA UTUUNGANISHE NAMI NIKO HAPA SWEDEN LABDA UTAKUA WIFI KANIVUTIA.sio lazima utoe hii coment in public but that ur choice.kama yuko single and intrested nambie nikutumie contact.

Unknown said...

Duh! Anonymous.... tumekusoma....Ha ha ha haaaaaaa
naomba niwe mshenga. dada Yasinta hongera kwa kupata wifi.

Ok kuhusu picha ya mtoto imenikumbusha mbali kama alivyosema mdau Bennet. watu tumepitia vitukop vingi sana utotoni....yaaani we acha tu

Mzee wa Changamoto said...

Huo ndio ubunifu Dada. Ni kama anavyozungumza rof Masangu Matondo mara kadhaa. Huu ndio ubunifu.
Asante