Wednesday, April 29, 2009

BIKIRA

Mada hii nimeruhusiwa na http://mbilinyi.blogspot.com/ kwani nina imani wote tuna nia moja.
Mabinti wa kizulu huko Lamontville Afrika kusini wakisubiri kukaguliwa kama bado ni mabikira huku nyuso zikiwa zimepakwa udongo.
(Picha kwa hisani ya Ellen Emendorp wa NYT)

Kutokana na desturi za huko Sri Lanka bibi harusi ni lazima athibitishe kwamba ni bikira usiku wa harusi yake.
Kila bibi harusi hutakiwa kubeba kitambaa cheupe ambacho huwekwa chini wakati wa tendo la ndoa kwa mara ya kwanza usiku wa kwanza kwa maharusi ili kuthibitisha kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
Kitamba kuwa na damu ni certificate kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
Na wapo mabibi harusi hukutana na wakati mgumu baada ya kujikuta hawakutoa damu yoyote ingawa ni kweli wao ni mabikira.
Hii ni kwa sababu wasri Lanka kama jamii zingine duniani bado wanaamini bikira yeyote hutoa damu siku ya kwanza na Yule ambaye hakutoa damu huonekana alijihusisha na ngono kabla.

Hiki ni kipimo cha kitambaa kuwa na damu ni kipimo potofu kwani na unscientific, wanawake wengi innocent huumizwa na kuonekana hawana quality ya kuitwa bikira wakati ni bikira.
Ni vizuri watu kujua uhusiano uliopo kati ya kizinda (hymen) na ubikira (virginity)

Bikira ni nani?
Bikira ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi (penetrative sex) na si lazima awe mwanamke ambaye atatoa damu siku ya kwanza ya tendo la ndoa.
Ni vizuri kufahamu kwamba asilimia 20% - 25% ya mabikira huwa hawatoi damu yoyote kutokana na muundo wa kizinda (hymen)
Wakati mwingine kizinda huondolewa kwa kufanya mazoezi mazito, kupanda baiskeli, kukwea miti na ifahamike kwamba kufanya mazoezi hakuwezi kuondoa ubikira.
Kizinda ni nini?
Kizinda ni ngozi nyembamba sana (membrane) ambayo huziba entrance kwenye uke.
Ina matundu ambayo hutofautiana kwa size ambapo damu ya mwezi kwa mwanamke huweza kupita kila mwezi.

Kuna aina Nne za vizinda
1. Kizinda cha kawaida (normal hymen),
2. Kizinda kisicho na tundu lolote [huhitaji surgery wakati mwingine] (Imperforated hymen),
3. Kizinda chenye tundu dogo sana (Microperforated hymen)
4. Kizinda chenye tishu za ziada na kufanya matundu mawili (septate Hymen)

Bado haijajulikana kazi ya kizinda ni nini, kwani baada ya sex mara ya kwanza huchanika na kuachana na kubaki historia.

Kizinda kiligunduliwa mwaka 1544 na Daktari wa kiarabu Ibn Sinna hata hivyo kufika karne ya 16 watu walikuwa wana imani potofu kwamba kizinda ni ugonjwa na dawa yake ilikuwa ni sex inayofuatana na mwanamke kuolewa.

Kutokuwa na kizinda au kutokutoa damu siku ya kwanza ya sex si evidence kwamba mwanamke si bikira wapo wanazaliwa hawana wengine nyembamba sana na wengine huweza kutoka kutokana na aina ya mazoezi au accidentally.Damu ambayo hutoka siku ya kwanza ya sex ni kidogo sana linaweza kuwa tone hakuna mwanamke amewahi kutoa damu na kulazwa au kuhatarisha maisha yake kwa sex mara ya kwanza.
Pia ifahamike kwamba mwanamke huweza kujisikia maumivu kidogo au discomfort wakati wa tendo la ndoa.
Hata hivyo maumivu mengi huhusiana na woga na ignorance (knoweledge is power), wakati mwanamke anakuwa na hofu, woga wakati wa tendo la ndoa misuli ya uke hukaza na uke huwa tight na mwembamba na wakati mwingine hushindwa kutoa lubricants kwenye uke kutokana kuwa na hofu na matokeo yake ni kusikia maumivu wakati wa penetration.
Pia inawezekana mwanaume hakumuandaa vya kutosha na pia inawezekana wakati wa kumuandaa mwanamke mwenyewe hakuwa relaxed na kuwa tayari kupokea tendo zuri la sex akihofia kuumizwa.

Je, mwanamke kutunza bikira hadi wakati wa kuolewa kuna heshima au fahari yoyote?

Kwa nini suala la kuwa bikira kwa wanaume katika jamii zote linakuwa halina uzito bali wanawake tu?

Je, wakati wa kuoa au kuolewa karne hii ya 21 suala la bikira ni muhimu kuzingatiwa?

12 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Hapa kuna mengi ya kujifunza. Asante kwako na Kaka Mbilinyi.

Mzee wa Taratibu said...

Kama sisi hatujaoa na tusiojua mambo kama haya sasa tutayajua kabla ya kuoa, mada nzuri hii.

Mwanasosholojia said...

Imekaa vizuri, kinachotakiwa ni kutafakari na kuchukua hatua!

Christian Bwaya said...

Mada nzuri. Hebu niitafakari zaidi.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mimi hapa sina la kusema! Hata hivyo kila mara huwa najiuliza, kwa nini ubikra wa wanaume hautiliwi maanani? Ni yale yale, ukisikia watu wanazungumzia malaya aka dada poa aka CD n.k, n.k. mara nyingi anayebebeshwa mzingo wa lawama ni mwanamke utafikiri kwamba huo umalaya anaufanya peke yake. Ni matokeo ya mfumo dume au???

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa Changamoto ni kweli hapa kuna kujifunza mengi.

Mzee wa Taratibu mmh hapa utafaidika.

Mwanasosholojia ni kweli kinachotakiwa ni kutafakarri na kuchukua hatua.

Kaka Bwaya Bado unatafakari?

Prof. Matondo hilo swali nami nimekuwa najiuliza kwa nini wasichana/wanawake tu wanatakiwa kuwa BIKIRA na sio wavulana/wanaume. Je kuna mtu ana jibu?

Albert Kissima said...

Wanawake na wanaume wote wanatakiwa kuwa bikira.

Pengine ubikira wa wanaume hautiliwi maanani kwani ni vigumu sana kutambua kuwa ni bikira au la.


Ubikira kwa ulimwengu wa sasa ni muhimu sana.Mtu anayeweza kuwa katika hali hii anakuwa amejiepusha na hatari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa na mtu wa aina hii kwa asilimia kubwa atawezakuwa mwaminifu katika ndoa.,ni heshima, inaongeza uaminifu kwa mwenza wako, n.k

ANGALIZO: Kuna kina dada/wanawake ambao hutunza ubikira ili watakapokuja kuolewa waonekane hawakuwa viwembe wakati kwa upande mwingine walikuwa wanakosoa uumbaji wa Mungu.Kwa hali hii hakutakuwa na maana yoyote ya kutunza ubikira!

PASSION4FASHION.TZ said...

Safi sana Yasinta,kweli hapa kuna mengi hii mada imetulia na ukitafakari kwa undani mmmh,wanawake bado tunaonewa sana wanaume je?

Bennet said...

hilo linaitwa chenza ingawa kuna machungwa yanamenywa kama chenza, aliimba Suma lee, naendelea kumnukuu kuna walioolewa na machenza na ndoa zao walishindwa kuzitunza, lakini kuna walioolewa na machungwa na ndoa zao walizitunza
Kwa sisi wanaume kuna raha yake ukilikuta chenza, ingawa nasikia kuna ya kutengeneza (Tanga huko) sijui kweli? kwa wanaume naona kumjua au kumpima bikira ni ngumu sana

Anonymous said...

Well, wanawake hujitunza kwa kuitunza .... asiguswe,
sijaona wanaume wanapimwaje? au wao ni haki kutembea watakavyo?

Richard said...

dah... wakati wakutoa bikra unastaili kutumia nguvu na inatoka baada ya mda gan( dakika) ngapi

Ulimwengu Habari said...

Saf. Nimeipenda hii zuli sana yani