Friday, April 3, 2009

NGOJA LEO TUANGALIE:- UGONJWA UNAOMALIZA WATU WENGI AFRIKA YETU MALARIA

Malaria ni moja ya magonjwa hatari yanayoambukizwa kwa haraka sana. Gonjwa hili linaenea zaidi kwenye nchi za tropiki na (subtropical) juu zaidi kwenye joto duniani, zaidi ya yote Afrika. Dalili kubwa kujua una malaria ni joto la kupita kiasi(homa), baridi ya nguvu, maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, kutokwa na jasho. Pia kinyaa, kutapika na kuhara inaweza kutokea pia.

Wasiliana na daktari kama umepata joto baada ya kusafiri nchi za joto ambazo kuna uwezekano wa kuambukizwa na malaria, hata kama ulikuwa unatumia kinga. Mimi na familia yangu hapa juzi tulipokuwa TZ wote tumeumwa malaria na wakati huo huo tulikuwa tunatumia kinga. Kwa hiyo kula/kunywa kinga si kuwa hutapata malaria.

Watu zaidi ya milioni 300 kila mwaka huambukizwa na malaria. Zaidi ya milioni moja wanakufa na vifo vingi ni watoto hasa Afrika. Hapa Sweden kuna ripoti watu kama 100 husumbuliwa na malaria kwa mwaka. Wengi wao wameambukizwa Afrika

Ugonjwa huu husababishwa na protozo ambazo ni seli moja kutoka mnyama/mdudu ambaye ni familia moja na plasmodium na kuingia ndani ya mwili wa binadamu kwa kuumwa na mbu wa malaria. Vimelea(parasiter) vinaingia ndani ya seli za maini na humu wanagawana kabla maambukizo ya seli za dawa nyekundu(corpuscle)

Dalili nyingine
Muda kutoka maambukizo mpaka homa kwa kawaida ni kati ya wiki mbili mpaka wiki nne. Lakini inawezekana ikachukua miezi mingi kwa yale malaria ambayo si hatari sana, au muda mrefu zaidi.

Kuna ile aina hatari ya malaria ambayo dalili zake ni ngumu na maambukizi yake hajatibiki kwa hiyo watu wengi wanaweza kuzimia au kufa.
Aina ya pili ya malaria ina dalili ambazo zinaweza kuzuilika ila zinarudiarudia “baada ya siku mbili” au baada ya siku tatu.

Kupinga/kuzuia
Kama unasafiri katika sehemu za malaria jaribu kujiepusha kuumwa na mbu kwa kutumia dawa (anti-mosquito), vaa nguo mbazo unajua zinafunika mwili mzima hasa wakati wa jioni na usiku na tumia chandalua.

Mbu mara nyingi wanauma jioni na wakati wa usiku. Kama unajua sehemu uendayo kuna mbu wa malaria ni lazima uwe na dawa kwa nia ya kuzuia malaria.

Hata kama matibabu ya kuzuia sio 100% yanakinga, ni muhimu kuzuia kwa kunywa dawa kwa sababu ukiacha inaweza kuhatarisha na kusabisha ugonjwa mwingine zidi ya malaria.

Uchunguzi
Utambuzi wa malaria unafanyika kwa kupima damu kwenye darubini.Lakini hapa nilipokuwa nyumbani nilishangaa sana nilipojisikia vibaya nilienda kupima. Nilikwenda kwenye kliniki ya mchina mmoja yeye hatoi damu anatumia komputa tu anaweka vifaa kwenye vidole na inachukua nusu dakika kugundua kuwa una wadudu wa malaria au sio.

Matibabu
Inasemekana kuna dawa nyingi zenye nguvu ambazo zinaweza kutibu malaria.
Kwa urahisi inabidi kunywa dawa mara mbili mpaka mara tatu kwa siku (usiku na mchana). Kama hali inakuwa mbaya sana ni lazima upewe dawa moja kwa moja kwenye mishipa ya damu.

Wengi wanaweza kutibiwa muda mrefu, wakati huohuo mgonjwa mwingine wa malaria anaweza kuhitaji matibabu ya uangalizi makini (intensive care) Muhimu ni kwamba matibabu yaanze mara moja uonapo dalili.

8 comments:

PASSION4FASHION.TZ said...

Nikweli malaria ni ugonjwa hatari sana na unauwa watu wengi sana,nazani kushinda hata ukimwi,kitu kingine ambacho kinachangia sana vifo ni hizo dawa za malaria wanazopewa wagonjwa jamani kwa Afrika ni tatizo kubwa sana.

Mtu anakwenda hospitali anapimwa anakutwa na malaria,haulizwi kama ana allergy yeyote ana andikiwa dawa za malaria na kupewa au kuchomwa sindano kwa dawa ambayo ana allergy nayo,hapo badala ya kumtibu ndio anaongezewa tatizo.

Nakumbuka niliwahi kwenda muhimbili kwa matatizo ya macho,wakati nikiwa kwenye foleni baada muda kidogo walikuja watu 4 wanaume wawili na wanawake,mmoja kambeba mgongoni mwanamke wamemfunika khanga mwili mzima kama vile mwali!kufika pale wakamtemlemsha mgongoni wakamkalisha kwenye benchi,huku wakijitahidi sana kumfunika asipate mwanga kabisa,sasa wote pale tukaki na mshangao kwakuwa ndio walikuwa nyuma yangu ilibidi nimuulize dada mmoja kati yao,nikamuuliza mbona mnamfunika kiasi hicho? yule dada akaniambia yule mgonjwa ni mdogo wake alikuwa anakisumbuliwa na malaria alipelekwa hospitali ya Amana akapewa dawa baada ya kuzitumia tu,kosa alivimba mwili mzima,na maumivu makali sana baada ya siku 3 akaanza kupoteza nywele zikawa zinatoka,nyusi zote kope nazo zikatoka zote,baadae ya nywele zikaanza kucha zikatoka zote za mikononi na miguuni zote! yule dada akasema alikuwa hawezi tena kuongea, haoni tena alilazwa muhimbili zaidi ya miezi 3,basi akamfunua kidogo kwa haraka tumuone, jamani nakumbuka siku hiyo hata kula sikuweza alikuwa anatisha!binadamu ni wazuri hivi una nywele una kope na nyusi lakini ukipoteza vyote mwili wake ulikuwa na mabaka mabaka meupe kama mtu aliebabuka au kuungua na moto,niliogopa sana dada yake akasema yaani hapo ndio wao wanaona kuna mafanikio makubwa sana tungemuona siku za nyuma ni muujiza mpaka kufikia hali ile tuliyomuona nayo.

Nikamuuliza yule dada alipewa dawa gani?akasema ni hizi za malaria ilikuwa na mchanganyiko na (surpher)sina hakika na hizo spelling, na yeye huwa hapatani na hizo dawa yeye alipoandikiwa na Doctor basi akaanza kuzitumia,nikamuuliza tena kwanini hakumwambia Doctor kuwa yeye hapatani na hizo dawa? akasema hajui kusoma na wala Doctor hakumuuliza kama alikuwa na allergy yeyote,nilisikitika sana nikabaki najiuliza maswali mengi sana hivi ni wangapi wanakutana na matatizo kama hayo? ni wangapi wanapoteza maisha yao kutokana tu na kutokuelewa au kutokujua kusoma?

Halafu kuna kundi la pili ambalo mtu anaumwa badala ya kwenda kupima kwanza kabla ya kuanza kutumia dawa,yeye anakwenda tu pharmacy kununua dawa za malaria na kuanza kuzitumia pengine wala sio malaria inamsumbua,sasa tatizo kubwa ni huko vijijini jamani unamkuta mtu anauza madawa kama anavyouza vyakula vya kawaida,na kuna wengine hana hata ujuzi wa aina yeyote eti watu wanakwenda kutibiwa kwake kama yeye ni Doctor na mpaka kuwachoma sindano na kuwawekea drip,huko ndio watu wanakufa kwa kulazimisha jamani inasikitisha sana,sababu kubwa ni kukosa huduma karibu na maeneo wanayoishi.


hakika kuna vifo vingi ambavyo ni vyakulazimisha, pamoja na matatizo yote hayo hakuna hatua zozote zinazochukuliwa,inasikitisha sana.

Yasinta Ngonyani said...

Nakubalina nawe hili ni tatizo kubwa sana. Au nisema sijui hakuna hii tabia ya kuuliza kama unatumia hizi dawa au vipi. Unaandikiwa tu, Lakini pia ni jukumu lako wewe mgonjwa kujua kama zile dawa zinakuzuru au vipi. Lakini sasa kama hujui kusoma wala kuandika hiyo sasa kasheshe.

Tatizo jingine ambali ni kubwa ni kwamba watu wengi wanapuuzia kumaliza dozi. Wao wanakunywa dawa wakishaona nafuu basi wanaacha na hapo ndio malaria (wadudu) wanapochukua nafasi na kufanya kazi yake na mwisho wake ni kifo. Kwa kweli inasikitisha sana

Mzee wa Changamoto said...

Juzi nilikuwa naongea na Dadangu mmoja nyumbani akanieleza juu ya mtoto wa ndugu yetu aliyefariki kwa ugonjwa huu. Iliniuma sana maana alikuwa mwana mwema na mwenye sfya. Well! Kila kitu kwa wakati wake lakini bado inauma na ni tatizo saana nyumbani

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa changamoto pole sana kwa msiba. Nahisi jinsi unavyojisikia.Ni kweli kama ulivyosema kila kitu na wakati wake.

Yohana Limbe Juma (Mtumishi) said...

Mzee wa Changamoto pole sana kwa msiba. Malaria ni ugonjwa hatari sana. Juzi hata nikapata habari kijana mmoja kijijini kwetu alikuwa ameehuka. Nilipowauliza kama kawaida walikuwa wanafikiri kwamba karogwa. Niliwaambia wampeleke Bugando. Walipokwenda iligundulika kwamba ilikuwa ni Malaria na ilikuwa imeanza kunyemelea ubongo na wangechelewa kidogo tu basi angeweza kufariki. Sasa amepona kabisa na yuko nyumbani. Tumekazania UKIMWI lakini Malaria ndiye number one killer!

Bennet said...

Yasinta hii maada ni nzito sana na tatizo ni kubwa kuliko tunayolifikiria, hizi dawa zinachagua sana maana dawa hiyo hiyo inaweza kutibu mtu mmoja na mwingine isitibu, matokeo yake kuna dawa lukuki madukani mpaka hujui utumie ipi.

Kwenye blogu yangu niliongelea dawa ya mmea wa Aloe vera kama kinga ya malaria na inaendelea kuwasaidia watu wengi na wameikubali, mpaka sasa nimewakinga watu 14 na wamekubali kwamba uwezo wao wa kuhimili malaria ni mkubwa (kinga).

Yasinta Ngonyani said...

Kaka matondo, ni kweli watu wengi wanakufa kwa sababu wanafikiri kuwa wamelogwa na pia wengine hawataki kwenda kupima mapema na kuanza kula dawa.

Kaka Bennet, Ahsante, naomba uniambia unafanyaja na huo mmea wa Aloe vera? kwani ninao hapa nyumbani

Bennet said...

Yasinta nashukuru kwa kutaka kufahamu jinsi ya tembelea blog yangu na utajifunza mengi