Friday, April 17, 2009

GHAFLA SIKU MOJA TULIINGILIWA NA HAWA WAGENI "SIAFU"

Ruhuwiko/Songea 2009 mwezi wa pili . Siku hii ghafla tulifikiwa na wageni bila kutegemea. Ni wadudu hatari sana lakini bahati nzuri tuliwashtukia na kuwasaidia waendelee na safari yao. Ila wangeingia ndani basi leo tungeongea mengine.

5 comments:

Anonymous said...

na wanavyojua kuchagua sehemu za kung'ata hao, mbona mngekoma!! wao wanagusa sehemu muhimu tu (wanang'ata sehemu zinazouma)

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo tulikuwa na bahati. Ni kweli ni wadudu wabaya sana. Na wao wanapenda sana mida ya usiku tu wakati watu wamelala

Anonymous said...

yep, usiku ni muda mzuri wa kuwaingilia watu!!

Bennet said...

Faida za siafu ni kwamba wakiingia kwenye nyumba wanaua wadudu wote hasa wale waharibifu kama mchwa, tandu, buibui na wengine, kama wameingia sehemu moja tu ya nyumba labda chumbani, mnaweza kuhama kwa siku moja mlale chumba kigine au sebuleni ili wasafishe chumba, kesho yake kama nyumba ina mchwa lazima watahamia chumba kingine na wao mpaka wanamaliza kusafisha nyumba nzima.
Kama unawaona kero mwaga majivu wataondoka wenyewe.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kule Usukumani hawa ni kawaida sana. Kama alivyosema Bennet, ni wazuri kwani kama una panya au mende hawa watakusafishia. Lakini kama unafuga kuku au bata basi umekwisha!