Friday, April 17, 2009

MNAONAJE?IJUMAA YA LEO TUCHEZE BAO/NCHUA AU KWA JINA UJUALO WEWE


Lakini hapa uchezi tu kuna kitu pia unajifunza natumai wato mmenielewa vizuri tu.

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Huu mchezo unafikirisha saana. Unafikirisha kwa kutaka ujue ukianzia wapi utaishia wapi na itakupa nafasi ya "kusafiri" mizunguko mingapi na mizunguko hiyo itakufanya "ule" mara ngapi na mwishoni waweza "kulala" wapi na hiyo itampa nafasi gani mpinzani wako katika uchezaji wake.
Ni mchezo mzuri ukichezwa kwa kiasi.
Naamini ndio maana Prof Matondo akaita njia bora ya kufunbza hesabu.
Ijumaa njema Dada

Albert Kissima said...

Kweli Mzee wa changamoto umesema kweli, mchezo huu unahitaji mahesabu makali.

Mchezo huu umenikumbusha mbali kwani sisi hatukuwa na vifaa maalumu vya kucheza mchezo huo.Tulikuwa tunachimba vishimo vidogo chini na kisha tunatumia ndulele(ngogwe chungu) sijui wengine wanaziitaje.Nimemkumbuka jamaa mmoja ambaye alikuwa akitufunga sana kwenye mchezo huu.