Thursday, April 16, 2009

MAISHA/KUTEMBELEANA NA KUTAKANA HALI

Haya sasa wasomaji hapa duniani watu tumeumbwa tofauti kwa kila kitu. Kwani mimi nilikuwa nadhani watu wote tuna mawazo sawa hasa katika jamii. Kama nilivyosema tangu mwanzo kabisa nilipoanza kublog, kama wote mmesoma tangu mwanzo. Vipi tunalea watoto wetu. Yaani haya maisha ya baba, mama na watoto inanisumbua sana akili yangu. Ukizingatia vipi sisi waafrika tunavyolelewa. Kwa kweli mimi inanipa shida sana, ni vigumu kuelewa kwa nini dunia nzima wasiishi kama sisi waafrika. yaani kuwatembelea wazazi, ndugu na marafiki mara kwa mara. Yaani huku watu wanathamini zaidi pesa/kazi kuliko jamii. Utakuta mtu anamwacha mama yake baba yake mzazi kwenye nyumba ya wazee ili atunzwe na watu wengine kwa sababu yeye ana shughuli nyingi. Nimewauliza mara nyingi je? wangeacha hao wazazi wako leo ungekuwa wapi? Lakini wao wanasema kila mtu na maisha yake. Na nimejiuliza je? hii ni haki au vipi? Kwani najua sisi Afrika tunaweza tukaishi pamoja ukoo mzima na tunatunzana. Ndugu wasomaji mnasemaje mnaonaje upi ni utaratibu mzuri?

Jambo jingine ni kwamba nina nusu mwaka sijaonana na majirani zangu lakini leo ghfla wakati nipo nje nafanya usafiwa mazingira. Amekuja jirani yangu na kunisalimia na pia nia yake kubwa ni kuonyesha ya kwamba amepata mjukuu. Yaani huyo tunaishi pua na mdomo lakini kuonana ni kasheshe. Inawezekana wakati mwingine jirani anakufa na usiwe na taarifa. Huwezi kujua, na pia kuna mila/tabia huwezi tu kwenda msibani bila kualikwa. Sasa kwa vile kajua kanaanza kujionyesha basi kuku wote wamefunguluwa. Ukizingatia wakati huu ndo kuna kuwa na ile michomo ya kitimoto na bila kusahau bia (ulanzi). Mmhh. Maisha haya kazi kwelikweli.

2 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Siku zote nimekuwa nikijaribu kuhoji utamduni wa nchi za ulaya kila mahali, nimejaribu kuangalia namna jamii zinavyoishi tangu kale hadi sasa, najikuta nikisema hali iliyopo ughaibuni kiutamduni siyo uhalisi wa maisha ya mwandamu. Ndiyo maana nakubali tofauti hizi katika msingi kwamba kwanini huyu mungu aliruhusu watu wabuni maisha ya kuishi peke yako na kujali sana pesa? kwani anaacha kizazi hicho kiendeeleze mambo ya mababu zao bila kuhoji ni kwanini wanaishi maisha ya aina hiyo?

lakini najua kwamba Yasinta ni mwathirika wa maisha ya tamaduni mbili, ninasema hivi kwasababu nimekuona na kukushuhudia mwelekeo wa maisha namna unavyoyachukulia kwa msingi wa tamaduni mbili. lakini pamoja na kumudu kutofautisha mambo bado unakibiliwa na mtihani wa kufanikiwa kwani bado naamni unaishi katika njia za wale wale wanaoshi njia ambazo unazihoji ingawa siyo kwa kukusduia.

unaweza kuona maisha ya ughaibuni kwa namna ambayo kwa wale waliozaliwa na kukulia vijijini halafu wakakazna kupata shule lakini hawakubalika, naweza kuwepo hapo na ndiyo maana nasona sana kitabu cha Song of Lawino maana ukweli uliopo utadumu miaka milioni ijayo.

inawezekana kuwa masiaha hayo waliyachagua au yalikuja baada ya mlundikano wa mambo. lakini tukumbuke hata maendeleo ya vitu yanweza kuchangia tamaduni kubadilika maana hata Joseph Schampeter anadokeza kwamba historia inaweza kubadilika tokana na muda,huu ni ule ambao watu wanaishi kwa njia mpya ambayo jamii nzima inaweza kuathiriwa na maendeleo ya vitu. maana tunatakiwa kutofautisha kati ya maendeleo ya vitu na maendeleo ya watu. kwahiyo tunaweza kuona majumba ya sinema na mambo mengi ughaibuni lakini tamadani zake ni ovyo watu wanaishi kwa fujo bila kujali thamni ya utu wa mwandamu sababu ya vitu. labda naweza kusema kwasbabu nimezaliwa afrika, lakini kwa msingi wa maendeleo ya vitu hakika yamebadilsiha mambo mengi.

USIJIULIZE SANA WEWE SOMA kitabu cha SONG OF LAWINO utaelewa, unakumbuka nilikuonyesha ile sehemu ya "i am ignorant of european dances" soma maneo ya Lawino uone uhalisia wake

Fadhy Mtanga said...

Duh.!