Friday, September 19, 2008

RUHUWIKO


Ruhuwiko ipo baina ya Songea na Peramiho. Ruhuwiko ni mtaa, mtaa huu una sifa za kuvutia. Kwanza mwaka 1990 alifika papa, baba mtakatifu pale kanisani wakati huu halikuwepo kanisa kilikuwa kiwanja tu. Alitoa misa, pia wengine walibahatika kupata kipaimara. Siku ile hata mimi nilikwenda kumwona papa, kuhudhuria misa. Kwa hiyo mwenzenu nimebarikiwa kubarikiwa na papa. mtajiju msiobarikiwa.

Ruhuwiko kuna shule ya viziwi na bubu, pia kuna shirika la masista wa ndanina nje, Pia, Ruhuwiko kuna kiwanja cha ndege. Kwa hiyo msipate tabu. Ni sehemu nzuri imekaa katikati kwenda Songea mjini na pia kwenda Hospitali Peramiho.

10 comments:

Kibunango said...

Ooh.. Kwa hiyo ukitoka mfaranyaki unaingia lisbon kabla ya kufika londoni then ruhuwiko? ile kambi ya jeshi katika njia ya kwenda peramiho inaitwaje? nafikili ipo baada ya ruhuwiko

Yasinta Ngonyani said...

Aise inaonekana unaijua kweli Songea/Ruhuwiko. Kwani mie sikujua kuna Londoni. haya ile kambi ya jashi inaitwa chabruma nadhani

mchayano Ngonyani G said...

hata chabruma ni kitongoji cha lizaboni,vingine ni Mjimwema na Mwenge mshindo

mchayano Ngonyani G said...

Jamani mkitaka habari za Lizaboni ndio mimi muhusika hapa.Wakazi wengi wa Lizaboni wana mashamba yao katka kitongoji cha Mwenge mshindo. Basi huko kuna mihogo ile wacha.Wakati wa kifuku basi yale mambo ya uyoga ndio usinene.Kama dada Yasinta unaujua ulelema na kilembese basi huko ndio mahali pake. Hata wale walaji wa mawongo na mangatungu basi kule utavipata.
Jamni mangatungu ni matamu, lakini mpaka yawe na chumvi. aahhhahahahah!

mchayano Ngonyani G said...

Dada Yasinta, kumbe shida ilikuwa ni mimi mwenyewe, nilipotesa password. Imebidi nireset upya, na naona sasa mamby yanakwenda kama kula ugali wa mayau na lidelele,menga kutyelela tu pa singu, pa mulomo wiwezalepa kumemena.

Anonymous said...

LUHUWIKO: Yaonekana we Yasinta hukufahamu vizuri songea bana..Ukitoka pale mjini Mfaranyaki, Matalawe, Lizaboni. Londoni ni Kitonji cha Lizaboni lakini hakipo barabarani, kabla ya kufika Ruhuwiko kuna hiyo kambi ya Jeshi baada ya kutoka Lizaboni inaitwa "HUDUMA" au (Service) opposite na National Millings (NMC) ya zamani, then unaelekea Ruhuwiko..Namanditi na ukiwa Lilambo kama unakwenda Peramiho au Mbinga/ Mambabay kwa upande wa Kushoto yako ndio eneo la hiyo Kambi ya jeshi la Chabruma...

Kibunango said...

Anony..
Hiyo kambi ya Chabruma ndio karibu na Airport?

Damn missing Songea so much!

Anonymous said...

Samahani dada Yasinta au yeyote humu kuna anaejua information zozote kuhusiana na shirika la waklara fukara hapo Ruhuwiko? Nahisi kuvutiwa nalo nijiunge.

Na Mpangala said...

Mlongo kwa mala nyingine tena umeitakasha roho yangu enzi za Papa mimi nilikuwepo uko, na hizo baraka tulizipata wote nakumbuka hii siku kama ilikuwa jana. ni siku yakutokusahaulika.
usengwili.
weekend njema kwa wote.

ray njau said...

Ruhuwiko,Ruhuwiko sema tena Ruhuwiko.Sawasawa kabisa.