Monday, February 23, 2015

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA SABA /7 LEO :-Mmmmhh! Miaka saba leo imefika kama mchezo!!!!

Hapa nipo nyumbani Songea/Ruhuwiko katika shughuli za kuandaa madikodiko nikiwa na wifi yangu tukisaidiana  na pembeni ni kakangu mdogo. Ilikuwa inakaribia mwaka mpya 2015.
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka saba (7) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!.......... HAYA JUMATATU IWE NJEMA SANA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE.

NIMEONA SI MBAYA TUKIMALIZIA NA BURUDANI KIDOGO YA KIODA/CHIYODA KUTOKA KWA NDUGU ZETU HUKO KIJIJINI MANDA.... KARIBUNI

TUPO PAMOJA DAIMA...KAPULYA/DADAMKUU.

12 comments:

Mbele said...

Hongera sana, na kila la heri. Tuko pamoja.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana..Maana bila ya uwepo wenu singefika hapa na tuzidi kutembeleana kwa mtindo huu.Pamoja daima

che guevara mwakanjuki said...

Hongera sana

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Che! Ahsante sana..

Anonymous said...

Hongera Da Yasinta. Tunakutakia mafanikio zaidi katika MAISHA NA MAFANIKIO. By Salumu.

NN Mhango said...

Hongera kapulya kutimiza miaka saba ya huduma si nchezo. Mungu akuongezee wasomaji na machapisho.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ! Ahsante sanakwa ushirikiano wako.
Kaka Mhango! Kama ulivyosema si mchezo ila uwepo wenu unanikakamua. Pamoja dsima.

Nicky Mwangoka said...

Hongera sana dada. Pamoja daima. Asante sana kwa kutuhabarisha kutufurahisha na kutuelimisha.

Ester Ulaya said...

hongera sana dada yangu...blog yetu nzuri iendelee kudumu zaidi na zaidi

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Nicky Ahsante nawe kwa vile pale upatapo wasaa hukosi kupita hapa na kuacha lako la moyoni.

Mama Alvin Ahsante sana pamoja daima!

mumyhery said...


Hongera sana

Yasinta Ngonyani said...

Dada M! Ahsante!