Tuesday, February 3, 2015

JUMANNE YA LEO TUANZE NA:- HADITHI YA WAPENDANAO!!!

Katika pitapita zangu nikakutana na hadithi hii na nimeona si vibaya kama nikiweka hapa ili wengi tupata faida...karibu
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mdada mmoja alitaka kujua anapendwa kiasi gani na mumewe. Hivyo akataka kujua mumewe atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha. Mwanamke akaamua kuandika barua inayosema"Samahani mume wangu nimeamua kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya mbali na wewe. Barua akaiweka juu ya meza iliyochumbani .Baadae jioni, muda wa mumewe kurudi akajificha chini ya uvungu wa kitanda chumbani. Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma kisha akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua, halafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga miluzi na akiwa anavua nguo. Akapiga simu na akasikika akisema"Mpenzi nina furaha sana leo ..yule mwanamke nuksi amesalenda mwenyewe kaondoka na kutuachia uwanja, jiandae nakuja "Muda huohuo akaondoka. Mwanamke alipotoka uvunguni alikuwa amenyong'onyea na ameloa mashavu kwa machozi, akasogea pale ilipo barua na kutaka kujua mumewe kaandika nini. Akakuta maneno haya. "Nimeona miguu yako uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia. NAKUPENDA SANA MKE WANGU".......

4 comments:

Anonymous said...

Ana bahati mwanamke. Hivi kama mume wake hakuona miguu si angeamini kuwa ameondoka! Si ajabu mume wake angekunywa sumu!By Salumu.

NN Mhango said...

Da Yasinta hii kali ya mwaka. Du! Umeniacha hoi. Maana ukianza ukisoma unapata mfadhaiko kwa jinsi mtu anaweza kufanya hivyo. Kiburudisho ni pale unapomalizia na sentensi ya mwisho. Ila katika mazingira ya kweli au tuseme orijinali hali inaweza kuwa tofauti na inavyoonekana kirahisi.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu...unafikiri kweli angekunywa sumu?

Kaka Mhango .....ni kweli sentensi ya mwisho ni tamu. Ila sijui mke alijisikiaje?

Anonymous said...

nimeipenda hiyo.nami nitajaribu one day.