Friday, February 13, 2015

SWALI LETU LA IJUMAA YA LEO!!!

Swali letu la lau ni kama lifuatavyo:- Kwa nini wanawake wanaishi maisha mazuri, marefu na yenye amani ukilinganisha na wanauma?
NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA/MWISHO MWISHO MWEMA WA JUMA!!

10 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Naomba kutofautiana nawe. Ni wanawake wangapi, wapi na wa wapi? Kuna ukweli kuwa wanadamu wote wanaishi katika maisha mazuri na wengine magumu wengine kwa furaha wengine kwa uchungu. Nadhani ni mchanganyiko. Ni mawazo yangu tu.

Yasinta Ngonyani said...

kutofautina nami si vibaya kakangu ...na nakubaliana nawe ni kuwa ni wanawake wachache sana wana maisha hayo kila sehemu ...ila hapa jibu lake ni kwamba kwa sababu wanawake hawana wake/hawaoi.

Daniel Hhary said...

jibu ni rahisi tu bwana, WANAUME WANAWAHANGAIKIA WANAWAKE NDIO MAANA UNAONA WANAUME WANAPOTAFUTA HUTUMIA NGUVU NYINGI KULIKO WWANAWAKE

Yasinta Ngonyani said...

Daniel ...Unaweza kufafanua?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yasinta, bado sikubaliani na jibu lako. Hata kama wanawake hawana wake au hawaoi wanaolewa je hilo si tatizo?

Mama Wane said...

Mmmmh hapa mimi ngoja nipite kimya kimya tuu

Daniel Hhary said...

jibu ni rahisi tu bwana, WANAUME WANAWAHANGAIKIA WANAWAKE NDIO MAANA UNAONA WANAUME WANAPOTAFUTA HUTUMIA NGUVU NYINGI KULIKO WWANAWAKE

Penina Simon said...

Ni kwa sababu wanawake wanajipenda sana, wanaume shida yao ni moja inayowaharibia maisha na pension wanazokuwa wamepewa, wanapenda sifa na starehe za mwilini.

Rachel Siwa said...

Mmmhh hapa pakujifunza zaidi..

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! Nimekuelewa na pia naweza kusema si wanawake wote wana hayo maisha marefu na mazuri.

Mama Wana ! nashukuru kwa mchango wanko maana hujapita kimya kimya umeacha kitu Ahsante.

Daniel! Je unaona hilo ni jambo la busara kutumia nguvu? au nimekuelewa vibaya ?
Dada P: inawekana ikawa kweli.
Kachiki! si unajua ni raha kujifunza.