Sunday, October 19, 2014

SAMAHANI KWA TATIZO LILILOTOKEA KATIKA BLOG YETU YA MAISHA NA MAFANIKIO..ILA SASA NATUMAINI ITAKUWA SWALI...

Hodi, hodi! ndugu zanguni. Mwenzeni ipo ila tu semeni nilitekwa ...kwanza niliona tarehe 14/10 Dada Ester Ulaya /mama Alvin aliniambia dada kuna shida hapa Maisha na Mafanikio vipi? Nikashtuka halafu nikaangalia ni kweli lakini baadae tatizo likatoweka na nikaweza kublog kidogo. Sasa 16/10 nikatumiwa na ujumbe wa barua pepe na Pro. Mhango naye akawa anaiambia dada Yasinta vipi naona umeteka  maana nimejaribu kuingia nimeshindwa  fanya hima na utufungulie . Nikawa sasa najiuliza mwanadada mimi nitafanya nini hapa. Nimehangainga weeee bila mafanikio  naamaka  leo asubuhi nakutana na ujumbe mwingine toka kwa kaka yangu Salumu naye anasema vipi dada ?..Mmmhh hapa kajasho kakaanza kunitoka maana nilijua lile swala limetoka. Sasa hivyo nimerudi nyumbani na nimefungua hili kopo kwa woga ...nikamwomba msaada baba watoto naye kwa vile ni mtaalamu kidogo wa komputer inaonekana amefaulu kuutoa ule ujinga. Shukrani nyingi sana kwake. Ahsante...Tuwe makini kutoweka link ambazo hazina sababu. TUPO PAMOJA DAIMA. NAWASHUKURU SANA WOTE WALIOIONA SHIDA HII NA KUNIPA USHAURI MAPEMA.

5 comments:

Anonymous said...

Asante da Yasinta. Naona mambo yamekuwa bambam. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

kaka Salumu Ahsante sana kwa kuwa bega kwa bega nami. Maana umenipa moyo na hasa nimshukuru sana Mr. bila hivyo peke yangu nisingeweza:-(

NN Mhango said...

Tunakukaribisha tena duniani da Yasinta. Tengeza backup kuepuka huu uhuni na usaka tonge wa kijinga. Je una habari za pro Matondo? Maana naona ameadimika sana.

Nicky Mwangoka said...

Karibu tena, Nilishangaa kidogo maana kila nikijaribu ku-access yalikuwa yanakuja "mashikoro mageni"

Yasinta Ngonyani said...

kaka Mhango! ahsante sana nitafuata ushauri wako. Alo sina habari na pro Matondo labda tumtangaze maana kweli kaadimika mno.
Kaka Nicky ...ahsante sana alo nashukuru shem wako kanisaidia kutoa yale "mashikoro mageni" :-)