Wednesday, November 19, 2014

LEO NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA PRO. JOSEPH MBELE---


 NI KITABU CHA METHALI KATIKA  HADITHI ZA KINGONI  AMBACHO KIMETAFSIRIWA KWA KISWAHILI.
Ndiyo Profesa Mbele si mchoyo wa elimu ..kwa upendo wake wote kanitumia hicho kitabu. Nasema tena AHSANTE  SANA na shukrani nyingi zikufikia najua nimekushukuru.Nilikuwa sijui kuhusu hiki kitabu. Hapa ni moja ya methali zilizopo katika kitabu hiki:- YU NDUGU MACHONI...Kingoni ni Chihali chaku.....Tutaendelea siku nyingine na methali leo leongo ni kutoa shukrani.  ENDELEA NA MOYO HUO WA UKARIMU.

7 comments:

Christian Bwaya said...

Naweza kuelewa furaha uliyonayo dada Yasinta.

Kwa hakika Profesa Mbele ni aina ya wasomi wasio na uchoyo na maarifa. Hutamani kuona maarifa yanaenea na kutawanyika kumfikia kila mwenye kiu ya kuyapokea.

Tunalo jema kubwa la kujifunza kwake.

Christian Bwaya said...

Naweza kuelewa furaha uliyonayo dada Yasinta.

Kwa hakika Profesa Mbele ni aina ya wasomi wasio na uchoyo na maarifa. Hutamani kuona maarifa yanaenea na kutawanyika kumfikia kila mwenye kiu ya kuyapokea.

Tunalo jema kubwa la kujifunza kwake.

Ester Ulaya said...

abarikiwe sana sana...lazima ufurahi dada.....na mimi niombee cha kifipa hehe

ray njau said...

Katika uga wa elimu hakuna fursa kwa uchoyo.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Bwaya! yaani ni furaha hasa..si watu wengi wanaweza kujitolea hivi...

Ester ! nadhani kama atakuwa nacho cha kifipi atakutumia tu kwa jinsi ninavyomfahamu mimi.
Kaka Ray! hakika hakuna haja ya kunyimani elimu na ingekuwa vizuri kama nasi tungeiga mfano wake Pro.

Anonymous said...

Tanzania inashindwa kuwatumia wasomi wake kama profesa Mbele hapa angendeleza gurudumu la Elimu Nchini kwake, kwa kukosa kutambua michango ya Elimu na wasomi wake

Mbele said...

Ndugu Anonymous uliyeandika November 20, 2014 at 7:13PM, kwa bahati nzuri, utandawazi wa leo na tekinolojia, kama zile za mawasiliano, zinazidi kurahisisha mambo, kiasi kwamba mipaka ya nchi sio tena kikwazo kama zamani. Mtu unaweza kuchangia elimu na taaluma popote ulipo hapa duniani, na unaweza kufaidika popote ulipo hapa duniani.

Kama m-Tanzania au mtu mwingine yeyote ambaye anaamini kuwa nina lolote la kumfundisha, napenda kumwarifu kuwa vitabu vyangu vinapatikana katika duka la mtandaoni, hili hapa.

Mtu akishasoma, nitakuwa radhi kuendeleza mawasiliano naye ili kutoa maelezo Zaidi kuhusu mambo atakayohitaji. Mawasiliano haya tunaweza kufanya kwa kutumia tekinolojia za mawasiliano kama vile barua pepe blogu.

Na kama mtu hana uwezo au namna ya kuvipata vitabu hivi, anaweza kunianikia ujumbe, tukafanya mkakati nimpelekee vipi na wapi, na alipie wapi, hata kama yuko Tanzania.

Narudia, huu ni ushauri kwa yule anayetaka kujifunza angalau yale ya msingi ninayoyajua. Katika dunia ya utandawazi na tekinolojia ya leo, hili gurudumu la elimu mtu unaweza kulisukuma kutokea popote ulipo hapa duniani.