N imekuwa nikijiuliza kila siku na sijapata jibu, sasa leo nimeona niliweke hapa kwani palipo na wengi hapaharibiki neno, Ni hili hapa swali lenyewe:- Hivi kwa nini pilipili inamfanya/tufanya tupige chafya? Najua mtasema mbona kuna vingi vyatufanya kupiga chafya, lakini mimi naona pilipili ni zaidi.....naomba tujadili kwa kupamoja. JUMATANO NJEMA!!!
6 comments:
hahahah dada swali zuri sana...bora wanaofahamu waje wajibu nipate kujua pia...ingawa pili pili huwa sili na siipendi
Ester Basi ngoja tusubiri ....maana elimu hainyimwi..mie nakulaga ni tamu pia:-)
Wanasemaga pilipili huongeza hamu ya kula (appetizer)na wangine husema inasababisha ugonjwa wa bawasir/kifaduro, wahindi wanaipenda sana mpaka ipo juisi ya pilipili! Sifahaham kama inasababisha chafya. by Salumu.
Hapa nimeshindwa kujua, kwanza kabisa nini humsababisha mtu kupiga chafya?
Nikipata jibu la hilo ntaweza kujua kwn pilipili humsababishia mtu kupiga chafya
Japo hii si fani yangu, nadhani pilipili husababisha kupiga chafya tokana na ukweli kuwa zinaposagwa huwa chembechembe laini ambazo huingia si puani tu hata machoni. Kawaida chembechembe hizi laini zinapoingia puani lazima ziisisimue kiasi cha mwili kuzisukumia mbali kama kanuni asilia ya kujikinga na viingilizi. Hivyo si kwa pili pili tu. Hata petrol au vimiminika vikiingia puani lazima kutakuwa na mrejesho.,
Kaka Salum! ni kweli hilo la kuongeza hamu ya kula nimewahi kulisikia. Kuhusu huleta homa ya kifaduro sijawahi kusikia ila ugonjwa wa moyo nimesikia. Mmmhh hiyo juisi sidhani kama naitamani...
Usiye na jina wa 7:27 AM... Ni haswa wote tunatraka kujua nini hasa sababu kwa hiyo ukijua usikose kutojuza:-)
Kaka Mhango!Ahsante kwa mchango wako...
Post a Comment