Wednesday, September 10, 2014

NINA IMANI WENGI WETU TUNAKUMBUKA VIFAA HIVI....ZILIPENDWA-PICHA YA WIKI!!!

Bila redio kama hii ilikuwa hakuna kucheza disko,  bila pasi basi ni kuvaa shati la makunyanzi, bila kibatari/koroboi basi kulala kiza/giza na mwisho ni mpira huo ......

4 comments:

NN Mhango said...

We Yacinta wee! Kweli umeua. Umepata wapi picha za Tanesco, World Cup,Bwana Mtanashati na hiyo runinga ya zama zetu wakati wa viatu vya ghorofa au vistuli ngazi nne? Umenikumbusha mbali kipindi kile watu wa kiva buga bugaloo, pekosi, petty na vitu vingine. Zama zile kama mzee wako ana mtambo huo uitwao memory ujue nyie matajiri hakuna mfano. Kama ni kijana kaununua lazima jumamosi aandae disco kwenye ukumbi wa shule ya msingi huku akijinoma na usafiri wake wa pajero aina ya baiskeli. Ngoja niachie hapo.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango...utundu tu. Vya zamani bora jamani...yaani hiyo pasi nilipokuwa nyumbani baba akanionyeshe mpaka leo anayo aliinunua enzi zile za wakimbizi wa msumbuji walipokimbilia Lundo kwa bei ya shilingi tano...nilishangaa sana. Kwa kweli nimeamini atunzaye huwa nacho/akiba haiozi....nimecheka kweli leo umenikumbusha mbaaaali....ahsante!

George Olloo said...

bado yapo na yanatumika sanaaa kwa jamii ya kiafrika kwahiyo wala siyo
zamani hata leo

Yasinta Ngonyani said...

Kaka George! nimefurahi kusikia hili jambo:-)