Friday, September 12, 2014

TUMALIZA WIKI KWA UJUMBE HUU UKIWA DUNIANI USIHUZUNIKE NA USIWE MNYONGE HATA KAMA UNA UMASKINI KIASI GANI!!!!

Ukiwa DUNIANI USIHUZUNIKE  na usiwe MNYONGE hata kama una UMASKINI kiasi gani, Mungu yuko pamoja nawe, na unatakiwa kizingatia haya;.

1. Usijilaumu kwa lolote lililokutokea.
2. Usihofu kuhusu hali uliyo nayo sasa.
3. Usijilinganishe na mtu yeyote duniani.
4. Usifikirie sana yaliyopita katika maisha yako
5. Kumbuka Mungu ndiye mpangaji wa kila linalokutokea.
6. Usiwaze sana kuhusu kesho waza kuhusu leo.
7. kukikosa ulicholikusudia yote ni mipango ya Mungu.
MUWE NA SIKU  PIA IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA JUMA.

7 comments:

Amina said...

Usipowaza kuhusu kesho si hutakuwa na malengo endelevu?

Yasinta Ngonyani said...

Amina...leo ni leo na kesho ni kesho.....

Mama Wane. said...

ahsante dada Yasinta ni ujumbe mzuri.ila kuwaza kesho ni lazima mwenzangu.

Yasinta Ngonyani said...

Kwanini mama wane?

Anonymous said...

Tunaangalia tulipotoka, tulipo, na kusonga mbele. By Salumu.

Salehe Msanda said...


Asante kwa ujumbe murua
Wengi tunakosa furaha na amani kwa kutokana na kuwaza na kufikiria vitu ambavyo
hatuna uwezo wa kuvibadili mfano hutuna uwezo wa kuibadili jinsi kesho itakavyokuwa kabla haijaifika hiyo kesho
Kila la kheri na weekend njema

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu! umenena...
kaka salehe! ni kweli..ahsante kwa mchango wako.