Saturday, May 5, 2012

HUU NDIO MLO WANGU WA JIONI HII YA LEO KARIBUNI!!!....

..NI kuku TANDORI kwa chips (viazi) pia kachumbali kwa mbaliiiii. Msiwe na wasiwasi kuna zaidi kwa hiyo anayejisikia kuja KARIBU SANA:-) JIONI NJEMA YA JUMAMOSI YA LEO!!!

9 comments:

Mtani said...

Yasinta kuna vitu nimeona hujataja, au ndo mambo ya "na kadhalika" (na kazalika). Hapo umetaja chips na kipaja cha kuku, lakini kwa mbaaaaaliiiiiii kuleeeeee naona kuna sahani.

Msosi wenyewe naona iko sahani moja tu, sasa wakija wageni 3 tena wanaume wa nguvu watashiba? Kule kwetu chips ni mboga, kwa hiyo hatuwezi kushiba.

Jioni njema!

Mtani said...

Swali la kizushi/kitaalam:

Kwa nchi za wenzetu, dinner huliwa kuanzia saa 11 jioni na aliyechelewa sana saa 1 jioni. Mtani wangu nimeona amebandika huu mtundiko saa 12:35 jioni (natumaini ni kwa saa za kwake). Hapa kwetu Tanzania dinner huanza kuliwa saa 2 usiku na waliochelewa sana hula saa tano usiku, japo wanaokula saa tano usiku ni wachache (msiniulize takwimu nilizipata wapi, ila dondoo fupi ni kwamba nimezowea kuzamia misosi).

Je, kuna madhara yoyote kiafya kula chakula cha usiku late? Kama yapo, ni yepi? Je, kula mapema kuna faida au madhara yoyote?

Yasinta Ngonyani said...

Ondoa shaka mtani kuna sahani nyingi hata ukitaka ugali utapata. Hiyo ilikuwa tu kama kuanzia na mwendelezo utachoka...kuhusu kula mapema muda nilikuwa nakula ni saa kumi na moja ya hapa ambayo nyumbani Tz ni saa kumi na mbili jioni...faida ya kula mapemna ni kwamba unapoenda kulala unakuwa huna chakula tumboni na unalala kwa raha zote...

mumyhery said...

Shukran tutakaribia

Mija Shija Sayi said...

Yaaani..

Rachel Siwa said...

Nimechelewa hamkunibakishia? nimezila/susa!!!

Interestedtips said...

yam yam, natamanije hapoooooooo

Yasinta Ngonyani said...

Dada M! karibu sana..wahi basi.
Mija! we acha tu yaani!!
Rachel! wala hujachelewa kipo kingi tu ila kama kweli umezila bathi bana!

Ester! yaani utamu mpaka nalamba vidole....

simba deo said...

Mateso hayo ... mie hapa mate yananitoka ... da ... sasa kuku huyo wa chenyeji au wa chichina? Mana du ... siku hizi hata wanaume wanakuwa na matiti makubwa ... nasikia sababu ya kula kuku wa chichina ... Wataalamu watujuze!