Tuesday, May 15, 2012

HAPA NI BAADHI YA MISEMO NA METHALI TOKA SEHEMU MBALIMBALI TANZANIA!!!

1.Alipo mtu mwenye dosari si vema kuzungumza habari hizo (Kibena)
Maana ya methali hii ni kwamba mtu mwenye dosari huwa na wasiwasi kila mara dosari yake igusapo, na huwa mkali kiasi cha kushangaza wazungumzaji. Kama dosari hiyo ni kilema huweza kuwafikiria vibaya wasemaji. Hutumika katika kuwaonya watu kuwa iwapo wanafahamu kwamba mtu mmoja kati yao ana dosari wajihadhari kugusia hiyo wakati wa mazungumzo yao.

2. Mzigo kichwani mwa mwenzio waweza kuwa wako (Kiiraqw)
Kila mtu ana matatizo yake na kuyatatua kwa kushirikiana na wenziwe. Kuna watu wenggine wanaokataa kutoa msaada wakidhani wanajitosheleza wenyewe. Methali hii inafundisha umuhimu wa ndugu na ushirikiano katika maisha nayo hutumika wakati inapotakiwa kuonyeshwa fundisho hilo.
PAMOJA DAIMA!!!!



10 comments:

emuthree said...

1.Ukiruka ukuta uagane na kiuno chako
2.Jana changa la mgomba usimcheke jani lilozeeka maana ni kesho au keshokuta na wewe utakuwa hivyo hivyo.
Hizi ni methali za Kipare,...natumai kila kabila wana methali zao, na zina maana nzuri tu, ina haja ya kuzihifadhi, kwa vizazi vijavyo

emuthree said...

2.Jani changa la mgomba....'nasahihisha hapo juu, kwa kipare huitwa `kidere'

Rachel Siwa said...

Hahhahh hehhhe tehethet kwikwiki oohh Sandee sana beeh Mlongo wangu a.k.a. KADALA!!! Uwii!!

@Ndudugu wa MIMI Asante pia za Kipare, nitakuuliza sikunyingine kuhusu wapare!!!!!

Wabena kwakujihami Duuhh hata wakitaka kusema kitu wamesikia sehemu, Wataanza kuna Tetesi ili akisutwa/kuulizwa ilikuwaje Nyeh Si Nilisema Tetesi?

Lakini nawapenda tuu!!!

Wenu Kachiki Muke ya Mubena!!!!

Yasinta Ngonyani said...

emu3! ahsante kwa kutupa methali za kipare ndio kujifunza huko.
Rachel we mlongo wangu! nilijua tu utasema unawapenda Wabena...Hata mie nawapenda sana naweza kusema ni nyumbani kwangu kwa pili Ubenani..
nimeipata hii methali katika kitabu cha hadithi za WANGONI INA SEMA HIVI:- Mdomo ukila pua haitaki na Fundisho laki ni: Watu wengine hawafurahii mafanikio ya wenzao. Ahsanteni ndugu zangu kwa kuwa nami...

Rachel Siwa said...

Pamoja da' Yasinta ipo siku tutakutana huko au vipi? kitabu cha hadithi za Wangoni nami natamani kukisoma,oohh usahau na wa............

Mtani said...

Nyeh! Muke ya Mubena leo amekumbusa mimi mbali sana, "wewe niangusage tu, sambi sako mwenyewe"! (lakini hawa ni binam za wabena maarufu kama wahehe).

Rachel umenikumbusha Kidugala na Ilembula. Halafu ukutane na Baba mtu mzima au Mama mtu mzima, wanaongea kwa mapozi hawana haraka.

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! Wala usikondo kuhusu vitabu vya hadithi za wangoni utavisoma tu..ila je unaweza kingoni?

Mtani! nimecheka kweli hapa hiyo ya "wewe niangusage tu, sambi sako mwenyewe" kaaazi kwelikweli....

ray njau said...

Jasiri haachi asili !!!

Rachel Siwa said...

Hahahhahah nyehh Mtani nitakuchapa wewe kuwaesema "niangusage" hahahaha Mtwangona kuendelea haahah kweli wewe unawajua huwa wasugua/fikicha Viganja kwa mapoziiiiii

Da'Yasinta amecheka sana ulipowata Wahehe tehteheteh.

Kujua kingoni itabidi nijue tu, kwasababu nakupenda, na Ukipenda Boga............

ray njau said...

@Yasinta;
Kwa wachaga hakuna misemo au Moshi na Songea ni mbali?