Wednesday, May 9, 2012

JIONI NJEMA NA :-WANAWAKE WA SHOKA/ WANAWAKE NA VILEMBA ("WRAPS")

 Dada Mija wa http://damija.blogspot.se.
 Mama Ana Tibaijuka.
Na Winnie Mandela, aliyekuwa mke wa Mstaafu Rais Nelson Mandela.
JIONI NJEMA!!!

11 comments:

sam mbogo said...

Vilemba,! dada mija kilemba chako kiko powa sana,kwahakika umependeza,wewe na hawa wengine. ukiangalia kwa udadisi zaidi,vilemba kwa wanawake wengi ,hasa vya aina hii tunavyo viona,kuna ukweli ndani yake kwa mba ni dalili au ishara za mwana mke kujitambua.mara nyingi vilemba hivi havi valiwi bila sababu. mfano kwenye sherehe,au mkusanyiko wa watu kwe lengo la kupongezana,na utakuta maandalizi yake si mchezo,huwa kunakuwa nakusidio maalumu,katika uvaaji wake,hukurupuki tu na kusema leo navaa kilemaba,ndo maana huonekana kwa baadhi ya wanawake ambao ukiwafuatilia kwa karibu,maisha yao ni wana harakati. kisaikolojia kilemba,ni nguvu,ni kujiamini ni ,ushupavu, ni ujasiri na hata wakati mwingine ni kuthubutu nk. huo ni mtazamo wangu..kaka s

Mija Shija Sayi said...

Yasinta asnte kwa kunipa heshima hii dadangu.

Kaka Sam, una mawazo yenye nguvu sana unatakiwa uanze kuandika vitabu ili wengi wafaidike kwa mawazo na mtazamo wako.

Mbarikiwe wote.

Rachel Siwa said...

Kweli ni wanawake wa shoka,wamependeza sana.kaka Sam mwana wa Mbogo asante kwa shule.

emuthree said...

Yaah, imekaa vyema, huenda katika kutafakari kuhusu vazi la taifa, labdakilemba kina nafasi yake,maana kilemba, kwa mwanamke kina ashiria heshima.
Kwanini nasema hivyo, kwasababu mtu kasuka nywele zake vyema, au kaziweka kinamna atakavyo, ili watu wamuone, je anaweza kuweka kilemba?
Huyu aliyeweka kilemba hakujali hilo, alichojali ni heshima yake tu,...Hongereni nyie wanawake wa shoka.

Mtani said...

Kweli wanawake wa SHOKA na vilemba vya nguvu japo nimevutiwa zaidi ya kilemba cha dada yangu Mija.

Penina Simon said...

Wamependeza hawana mfano, Duh kweli mwanamke kilemba!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! hakika ulichoneno ni kweli kabisa mwenyewe hapa nilikuwa najiuliza kufunga hiki kilemba si unahitaji ufundi sana. Hata mie nimekipenda kilemba cha dada Mija.
Mija! Sisi ni wanandugu ni watoto wa baba mmoja...halafu kingine nimekipenda kilemba chako. Nilikuwa nakikodolea macho muda sasa.
Rachel! Yaani haswa wanawake wa shoka.
emu3! Itapendeza kama kutakuwa na kilemba cha taifa na nitakuwa wa kwanza kukifunga. Kusuka au kuweka nywelw kimtindo na kuvaa kilemba mimi naweza nikajibu kwamba inawezekana .
Mtani!Unaweza kusema kwanini umevutiwa zaidi na cha dada Mija?
Dada P. Yaani we acha tu. kwa maana hiyo wanawake inabidi tuvaa zaidi vilemba.

Mtani said...

Yasinta,

Nimevutiwa na kilemba cha Dada yangu Mija wa Sayi kwa kuwa rangi ya kitambaa imetulia na kwa mbali kale ka-ufito (mstari) kana match na rangi ya uso wake. Wakati mwingine choice ya rangi ya nguo matters a lot kwa kulingana na color ya ngozi ya mvaaji. Pia namna alivyofunga kuna ufundi wa aina fulani ambao unafanya kilemba kivutie zaidi.

Sam Mbogo amesema kwamba kufunga kilemba ni sign ya nguvu, kujiamini, ujasiri, ushupavu na uthubutu. Kwangu mimi hayo yote ninayaweka kwenye category moja kwamba ni USHOKA wenyewe. Nikienda mbali kidogo, kwa kutumia analogy ya Sam, kitambaa cha Da Mija kiko very firm (kimeshika hasa, amekifunga kwa kukaza). Hiyo ni dalili ya nguvu na kuonyesha kwamba yuko tayari kwa lolote lile hata kama amevaa vazi la heshima. Ile notion ya uana harakati inaingia hapo. Angalia picha za Winnie Mandela na Ellen Johnson Sirleaf (Rais wa Liberia) zama zao za harakati, vitambaa vyao vilikuwa viko firm ukilinganisha na wanavyofunga siku hizi.

Kwa hiyo u-shoka na uana harakati can be traced back kuanzia ujanani. There are ladies ambao wako ready kwa lolote wakati wowote na wako young ladies ambao wanafunga vilemba kama urembo, kukitokea saga rhumba kitu cha kwanza anafikiria, sijui kitambaa changu kitadondoka?

Nikirudi kulinganisha kilemba cha Da Mija na hao wamama wengine wa shoka:

Ukiangalia kilemba cha Winnie Madikizela kwa haraka kimekaa kama kofia, halafu ameweka wig ambalo lime-overflow nje ya kilemba na hivyo kupunguza utamu/uzuri wa kufunga kilemba. Kwa kawaida vilemba maalum kama hivi huwa vinafungwa kwa ku-match (kumechisha) na vazi la chini, sasa wig likishatokezea, hata ile matching inaharibika. Kwa sisi tulioenda JKT tutasema dressing ni zero.

Nikimalizia na kilemba cha mwalimu wangu Prof. Tibaijuka, amejitahidi kufunika nywele lakini kwa juu kimesambaa sana na hivyo ile dressing (mpangilio) unaharibika. Pia usipokaza kitambaa wakati unakifunga, ni rahisi kubadilisha muonekano pindi kukitokea mtikisiko wa aina yoyote na ndio maana unaona upande mmoja kwa mbaaaali nywele za Anna zinaonekana na upande mwingine nywele hazionekani.

Sijui kama nimejibu swali lako Yasinta.

Mija Shija Sayi said...

@Mtani..si ujitokeze jamani tukujue?

Bless you all..!!

Mtani said...

@Da Mija,

Nimekusikia dada yangu.

Yasinta Ngonyani said...

Haya mtani nimekusika na nimekuelewa. Ahsante sana kwa ufafanuzi. Ni ufafanuzi mzuri na mwenye kueleka.Pamoja daima.