Thursday, May 10, 2012

JELA -NA HUSSEIN MACHOZI

Nimeupenda wimbo huu wa Hussein Machozi na hasa ujumbe wake kuhusu jela. Ukipata muda hebu jaribu kuusikiliza.


Maisha haya jamani kaaazi kwelikweli...Bora nirudi jela.....!!!

6 comments:

emu-three said...

Inasikitisha...hebu jiulize mtu kama Mandela, alifungwa akiwa kijana akatoka mtu mzima!

Yasinta Ngonyani said...

emu3! Yaani kweli inauma halafu ikiwa kosa ni la uongo halafu unarudi nyumbani wengine wamerith kila kitu kweli huu uungwana kweli?

sam mbogo said...

Jela simahali pazuri kwa hakika.Hasa jela zetu za Tanzania(Afrika).kitu ambacho kina nisumbua akili yangu, ni mfumo mzima wa magereza zetu,bila kusahau mahabusu pia. nafikiri tangia tupate uhuru au hata wakati wa mkoloni,mfumo wa magereza zetu bado ni ulele .majengo ni yaleyale,huduma kwa wafungwa ni mbaya,vitu kama vyoo,maji sehe za kulala,chakula havirdhishi,afya za wafungwa ni mbaya.hakuna mtu anaye tupia macho eneo hili na kuliboresha.adhabu wanazotoa zingine wala hazistahili mtu kufungwa.magereza zikipata kiongozi mbunifu zinaweza kujiendesha zenyewe,na kuboresha mazingira yake,wengi wafungwa wanataaluma zao na vipaji mbalimbali ambavyo vikitumika vizuri vitasaidia ,kwa wafungwa wenyewe na magereza kwa ujumla.piya wizara husika(mambo ya ndani) ikipata waziri mbunifu ,mchapakazi anaye jituma na kujiamini anaweza akafanya mabadiliko makubwa sana katika magereza zetu.kaka s

Unknown said...

hii inasikitisha sana...

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Emu-3 & Da Yasinta: fikiria kama Mandela angekuwa na mawazo kama ya huyu mwanamuziki mjinga ati bora nirudi jela...

akute Winnie wake amechukuliwa na vi-serengeti boys; nchi iko hoi... NIRUDI JELA!

kwangu mie nafurahia mdundo tu kwenye muziki huu na si ujumbe! Kwa kuwa hana uwezo wa kuyabadilisha hayo yanayotokea na hivo maisha lazima yaendeleee kama kawa!!

Labda kama alikuwa 'kaolewa' huko jela teh teh teh!

Kelkaf said...

Hussein machozi big up...mimi nafurahia wimbo wake kwasaabu kwanza amegusia suala la kutokuwepo haki kwenye mahakama zetu,na hata kwenye jamii,na hata katika suala la mapenzi nk lakini pia amegusia mfumko wa bei jinsi unavyoumiza wananchi na yote ni maswala ya muhimu kazi mzuri na ahsante yasinta kwa kupost huu mwimbo