Thursday, March 1, 2012

TAFAKARI YA LEO:-MILA NA DESTURI ZETU!

Nimekuwa nikiwaza jambo hili tangu nilipoanza kupata akili....Ni swali ambalo nimekuwa nimewauliza watu wengi nao hawajaweza kunijibu kwanini. Na leo nimeamka na naliona linazunguka kichwani mwangu na nimeshindwa kuacha kuuliza hapa kibarazani.
Ni hivi:- Hivi kwa nini msichana asimwombe kijana ampendaye kuwa anataka waoane? Najua ni mila na desturi zetu za kale kwamba ni mvulana/kijana /mwanaume afanye hivi. Je msichana/binti /mwanamke akifanya hivi kwa mvulana/kijana/mwanamume anayempenda itakuwa si sawa?

8 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

hatujambo wote ila kama ni mila na desturi basi kwanza tuanze na neno mila mila nijuavyo mimi ni utaratibu fulani wa kabila au jamii kwa kufuata mfumo wao wa maisha kama vile ngoma ,mavazi n.k yale yaambatanayo na jamii ile
desturi ni tabia ya watu fulani au kundi fulani na hata makabila au taifa ,hivyo vyote ukivichanganya utapata mfumo fulani wa hao watu au hiyo jamii ,kwahiyo kubadili ni ngumu kwani tangu hapo enzi hizo jambo la kupenda au kutamani aliachiwa mwanaume kwamaana hiyo mwanamke kumfuata mojakwamoja mwanaume na kumwambia nimekupenda au ninakuhitaji huo ni mtihani ila ataishia kumwonyesha ishara au atajitahidi kumletea mvulana au t6useme mwanume vibweka tuu ukweli labda mila za wenzetu wa mataifa ya huko ulaya na kwingineko ila afrika ukweli huwezi kuona wala kusikia mimi ni mtizamo wangu ila kumbuka kuwa yatafika kwani kwasasa maadili yote tanapotea kwani utandawazi unatumalizia mila zetu na desturi hivyo huko ulikohisia dada tutafika muda si mrefu hata mwaka 2020 ni mbali
asante dada KAPULYA
CHE JIAH

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hamna shida wawambie tu

Simon Kitururu said...

Kona zangu za maisha Tanzania na Duniani kwingine nimeshuhudia sana tendo hili. Kwa hiyo katika pitapita zangu kuanzia Bongo Nyoso maswala ya kimwana kumuomba vitu au mpaka NDOA njemba imekuwa kitu ya kawaida. Nahisi tu tunacheza viwanja tofauti kama katika kiwanja chako vimwana hawaombi.


NYONGEZA:

Na kumbuka kuomba ndoa sio lazima mtu aseme anataka kuolewa kwakuwa WADADA wajanja moja ya kukustua wanataka jumla jumla kwanza wana kuonjesha na kukunasa kiutamu halafu wanachokuambia baada ya kunasa ni kuwa wanakuacha kwa kuwa hawaoni mahusiano yanaelekea wapi.

Kumbuka kuomba embe si lazima EMBE litamkwe kuwa ndilo linaloombwa kwenye mila fulani kama za KIBONGO ambazo hata matusi yanatafutiwa diplomasia ili yasionekane ni matusi sana.

Na kwa hilo nasema WANAWAKE karibu asilimia zote WATAKAO KUOLEWA hutongoza na kuomba hata kuolewa kama unasikio zuri!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mbona wengine wanasemaga? 'Niangusage' ama si namna ya kusema 'nataka ndoa?'

ray njau said...

Hii ni changamoto kwa tamaduni zetu chakavu na zisizo na mashiko.

Anonymous said...

Seleman Awadh:
Nionavyo mimi kwa hali ilivyo sasa hakuna mila wala desturi kwa sababu
watu wameshaacha hivyo vitu mtu yeyote bila kujali umri/,rika,anaweza kumwambia mwenzake kuwa anamtaka kimapenzi au angependa kuwa nae/kuoana nae.

Salehe Msanda said...

Habari

Mila hiyo imeanza kubadilika kuna wanandoa wameoana kutokana na matokeo kua msichana kuanzisha suala hilo.



Kwa hali ilivyo sasa hivi haishangazi sana kuona msichana anamproach mvulana kwa lugha yao ya kileo.



Kila la kheri na hongera kwa kuleta suala hili kibarazani.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua fursa hii na kuwashukuruni wote kwa michango wenu. Baada ya kuandika hili likaja swali jingine je kama msichana akimwomba kijana uchumba ina maana ni yeye ndiye atoa posa? si mnajua kwetu Afrika kutoa posa ni kijana. sasa hapa itakuwaje?
Kwasababu wenzetu kule India huwa wanasaidiana nusunusu na kijana anachukua na kupeleka posa...Nikashika kicha na kusema kaaazi kwelikweli....