Friday, June 14, 2013

UJUMBE WA IJUMAA YA LEO:- NYUSO ZA MWANAMKE!!!

Unajua ya kwamba:- Mwanamke kama dutu la udongo wa mfinyanzi huumbwa na kuumbuliwa na jamii kwa namna mbalimbali. Kama kinyonga, uso wake unabeba rangi tofauti kulingana na mikondo ya maisha na mapigo ya wakati. Itakuwaje mwanamke awe wa kuozwa kama mwenye ugaga wa hisia za kujichagulia mwenyewe; au awe wa kuuzwa kama pakacha la maembe katika soko la umma? Uso wa mwanamke ni njia mbilimbili; ikiwa hazai analea, asipokuwa akirimbesha anarembeshwa, kama hatumbuizwa, ikiwa hajengi anabomoa; na kila mtu anamtazama na kumtarajia aonyeshe  uongofu wa malaika kama kwamba yeye si mtu. Haya yanapokolea ndipo mwanamke anaonyesha nyuso zake.....NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA..KAPULYA

3 comments:

Justin Kasyome said...

mewanamke ndio mhimili wa familia, akitetereka au kuyumba, familia haina mwelekeo maana mwanaume mwenye mafanikio, nyuma yake yuko mwanamke mwerevu...

Yasinta Ngonyani said...

Justin...N kweli. Ila wapo wengi wanaofikiri mwanamke ni pambo lenye nyuso nyingi au pia ni pambo lisilokuwa na uso hata mmoja.

ray njau said...

Sheria Inayoonyesha Maoni ya Mungu Kuwaelekea Wanawake
===================================
1. Walikuwa na uhuru wa kibinafsi. Tofauti na wanawake katika mataifa mengine mengi ya zamani, wanawake Waisraeli walifurahia uhuru mwingi sana. Ingawa mume alipewa daraka la kuwa kichwa cha familia, mke, akiwa na kibali cha mume wake, ‘angefikiria shamba na kulinunua’ na ‘kupanda shamba la mizabibu.’ Ikiwa alikuwa na ujuzi wa kusokota na kufuma, angeweza hata kufanya biashara yake. (Methali 31:11, 16-19) Chini ya Sheria ya Musa, wanawake walionwa kuwa watu wenye haki za kibinafsi.
Katika Israeli la kale, wanawake walikuwa pia na uhuru wa kuwa na uhusiano wa kibinafsi pamoja na Mungu. Biblia inazungumza kumhusu Hana, ambaye alisali kwa Mungu kuhusu jambo la kibinafsi na akaweka nadhiri kisiri. (1 Samweli 1:11, 24-28) Mwanamke fulani katika jiji la Shunemu alikuwa akizungumza na nabii Elisha siku za Sabato. (2 Wafalme 4:22-25) Mungu aliwatumia wanawake, kama vile Debora na Hulda ili wamwakilishe. Inapendeza kuona kwamba wanaume wenye vyeo na makuhani walikuwa tayari kutafuta mashauri kutoka kwa wanawake hao.—Waamuzi 4:4-8; 2 Wafalme 22:14-16, 20.
2. Waliruhusiwa kupata elimu. Kwa sababu walikuwa sehemu ya agano la Sheria, wanawake walikaribishwa kusikiliza Sheria iliposomwa, na hilo liliwapa fursa za kujifunza. (Kumbukumbu la Torati 31:12; Nehemia 8:2, 8) Pia, walizoezwa kushiriki katika migawo fulani ya ibada ya hadharani. Kwa mfano, inaelekea wanawake fulani walifanya “utumishi uliopangwa” kwenye hema la kukutania, huku wengine wakishiriki katika kikundi cha waimbaji kilichokuwa pia na wanaume.—Kutoka 38:8; 1 Mambo ya Nyakati 25:5, 6.
Wanawake wengi walikuwa na ujuzi na ustadi uliohitajiwa ili kufanya biashara na kupata faida. (Methali 31:24) Kinyume na tamaduni katika mataifa mengine siku hizo, ambako baba peke yake ndiye aliyewafundisha wanawe, akina mama Waisraeli walishiriki kuwafundisha watoto wao wa kiume mpaka walipokuwa watu wazima. (Methali 31:1) Bila shaka, wanawake katika Israeli la kale walikuwa wenye elimu.
3. Walistahiwa na kuheshimiwa. Zile Amri Kumi zilisema hivi waziwazi: “Mheshimu baba yako na mama yako.” (Kutoka 20:12) Katika methali za Mfalme Solomoni mwenye hekima, tunasoma hivi: “Mwanangu, sikiliza nidhamu ya baba yako, wala usiiache sheria ya mama yako.”—Methali 1:8.
Sheria ilitia ndani maagizo mengi kuhusu jinsi watu ambao hawajaoana walipaswa kutendeana, na hivyo kuwaheshimu wanawake. (Mambo ya Walawi 18:6, 9; Kumbukumbu la Torati 22:25, 26) Mume mzuri alipaswa kufikiria uwezo wa kimwili na kimaumbile wa mke wake.—Mambo ya Walawi 18:19.
4. Haki ya kulindwa. Katika Neno lake, Yehova anajirejelea kuwa “baba ya wavulana wasio na baba na mwamuzi wa wajane.” Kwa maneno mengine, alikuwa Mlinzi wa wale ambao haki zao hazikulindwa na baba au mume. (Zaburi 68:5; Kumbukumbu la Torati 10:17, 18) Hivyo, pindi moja mjane fulani wa nabii alipotendewa isivyo haki na mkopeshaji, Yehova aliingilia kati na kufanya muujiza ili yule mjane alipe deni lake na kudumisha heshima yake.—2 Wafalme 4:1-7.