Sunday, June 9, 2013

NI DOMINIKA/JUMAPILI YA 10 YA MWAKA C...NA TUANGALIE/TUSOME HESHIMA YA MWANAMKE NA WITO WAKE!!!

"Mwanamke kama Mama na mlezi wa kwanza wa mwanadamu ana haki ya pekee kabla ya mwanamume. Umama kwa upande wa utu na maadili unaonyesha uwezo wa mwanamke wa kuumba ulivyo muhimu sana ambao unadhihirisha wito wa pekee na ni changamoto ya pekee inayomchochea mwanamume na ubaba wake"
"Heshima ya mwanamke hutegemea utaratibu wa upendo, nao ni hasa utaratibu wa haki na wa kupendana..."
"Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!" Yesu akajibi, "Barabara; lakini heru yake zaidi yule aliyelisikia neno la Mungu na kulishika"

4 comments:

Anonymous said...

Hakuna kama MaMa! By Salumu

Justin Kasyome said...

kweli, mama ni mama!

Justin Kasyome said...

kweli, mama ni mama!

ray njau said...

Nitamfanyia msaidizi.—Mwa. 2:18. ===================================
Bila shaka, mke atahitaji kujidhabihu ili amuunge mkono kwa bidii mume wake kupitia maneno na matendo yake. Lakini anajua kwamba mume wake anaposhiriki kwa bidii katika shughuli za kiroho anaisaidia familia yote kukaa macho kiroho. Si rahisi kwa mke kuweka mfano mzuri katika kumuunga mkono mume wake wakati anapofanya uamuzi ambao mke hakubaliani nao. Hata wakati huo, mke anaonyesha “roho ya utulivu na ya upole” na kushirikiana naye ili uamuzi wake ufanikiwe. (1 Pet. 3:4) Mke mwema anajaribu kuiga mifano mizuri ya wanawake waliomwogopa Mungu nyakati za kale, kama vile, Sara, Ruthu, Abigaili, na Maria, mama ya Yesu. (1 Pet. 3:5, 6) Pia, anawaiga wanawake wenye umri mkubwa leo “wenye tabia ya kumhofu Mungu.” (Tito 2:3, 4) Kwa kumpenda na kumheshimu mume wake, mwanamke ambaye ni mfano mzuri anachangia sana hali njema ya familia nzima. Nyumba yake ni mahali salama na penye kustarehesha. Mwanamume wa kiroho anamthamini sana mke anayemuunga mkono!—Met. 18:22