Tuesday, June 25, 2013

MATESO KATIKA NDOA/MAHUSIANO....KUFUJWA KWENYE NDOA NI NINI?Ifuatayo ni habari ya mwanamke ambaye aliwahi kuja kwangu kwa ushauri kuhusu ndoa yeke: Mama Kotilda Mkatah aliolewa mwaka 1980 na mume msomi aliyekuwa na wadhifa mkubwa kwenye taasisi moja ya fedha ya serikali.
Ndoa hii ilifungwa kwa sababu, Kotlida hakuwa na njia, lakini anasema, tangu wakiwa kwenye uchumba, alikuwa tayari na wasiwasi kama ndoa yao ingekuwa ni ya amani. Anasema, wakati bado wachumba, huyo bwana aliwahi kumpiga kibao kwenye kituo cha UDA kwa kosa la kuchelewa kufika kituoni kama walivyokuwa wamekubaliana.
Ndoa ilikuwa ni ya mateso makubwa hata kabla haijafungwa, Mwezi mmoja baada ya ndoa, mume alimwachia mkewe kazi kwa kwenda kufanya fujo ofisini kwa bosi wake kwa madai kuwa bosi huyo alikuwa na uhusiano na mkewe. Kotilda alianza kuishi kwa masharti. Hakuna kutoka, hata kwenda kwa jirani bila kuomba ruhusu na kutoa maelezo marefu kwa nini aende huko.
Kusimangwa, kukosolewa, kuitwa mjinga na mbumbumbu, ikaanza kuwa ni sehemu ya maisha ya mama huyu. Hali iliendelea hivi na kotilda akawa anajiambia, kuna siku hali itabadilika. Lakini, kwa bahati mbaya, hali haikubadilika. Wakati anakuja kwangu, alikuwa ameshaanza kuamini kwamba ni kweli alikuwa anastahili kutendewa vile na mumewe.
Huku ndiko tunakoita kufujwa. Mpenzi mmoja anapomuumiza mwingine kwa kauli zake au kimwili, mara kwa mara, tunasema hapo kuna kufujana.
Mpenzi mmoja anapokuwa na mamlaka aliyojipa dhidi ya uhuru na haki ya mwenzake, tunasema hapoimekuwa kufujana. mara nyingi, wanaofuja ni wanaume. Miongoni mwa matatizo ya ndoa ambayo mtu hashauriwi kuendelea kuyavumilia ni kufujwa. Ndoa ya kufujwa kuna maumivu makubwa ya hisia na mwili.
Ni vizuri hata hivyo, nikasema kwamba, neno kufuja ni mimi ambaye nimelibuni keelezea hali hii, ambapo mtu mwingine angeweza kuita mateso katika ndoa, kuonewa katika ndoa au kutumia istilahi yoyote.
Nimeipenda habari hii nikaona si mbaya nanyi wenzangu msome kwani tusinyimane elimu.
Chanzo: kitabu cha Mapenzi kuchipua na kunyauka na marehemu Munga Tehenan.

6 comments:

Justin Kasyome said...

Mh! Asante kwa elimu hiyo, ili hata sisi tulio nje ya ndoa tujifunze namna ya kuingia kwenye ndoa iliyo bora! Kama ingekuwa mimi, tangu kipigo cha kwanza ningeteleza!

ray njau said...

Kutamaushwa—“Sikutarajia Hali Hii”

“Nilipoolewa na Jim,” asema Rose, “nilitarajia tungekuwa na mapenzi kama ya malkia na mfalme mwenye kuvutia katika hadithi moja—mahaba kemkemu, wororo tele na kutendeana kwa fadhili.” Lakini, baada ya kitambo kidogo, “mfalme” wa Rose akawa havutii tena. “Hatimaye alinitamausha sana,” yeye asema.

Sinema, vitabu, na nyimbo zinazopendwa na wengi hutoa maoni yasiyo halisi kuhusu upendo. Wanapokuwa wakichumbiana, huenda mwanamume na mwanamke wakahisi kwamba mataraja yao yametimia; lakini baada ya miaka fulani katika maisha ya ndoa, wanakata kauli kwamba hiyo ilikuwa ni ndoto tu! Maisha ya ndoa yasiposhabihi yale yanayosimuliwa katika riwaya za mahaba, wengi huona ndoa yao haiwezi kufaulu kabisa.

Pasipo shaka, matazamio fulani katika ndoa yanafaa kabisa. Kwa mfano, inafaa kutazamia upendo, ufikirio na utegemezo kutoka kwa mwenzi wa ndoa. Na bado, huenda hata matazamio hayo yasitimizwe. “Nahisi kana kwamba sijaolewa,” asema Meena, msichana mchanga aliyeolewa karibuni huko India. “Najihisi nikiwa mpweke na hakuna anayenijali.”

emu-three said...

Ndoa ni hazina isiyothaminika, na kama tungelijua hivyo, katu tusingeibeza.

Tatizo ni kuwa ,ni nini maana ya ndoa, na tufanye nini kwenye ndoa,haijulikani.
Ipo siku niliuliza kwanini ukitaka kuwa docta unausomea udocta, sasa kwanini kwenye ndoa ukitaka kuwa mwanandoa hatuusomei `undoa' tunaingia kichwa kichwa..

Hatutaki kujifunza kwanza kabla ya kuingia kwenye hiki kisiwa cha baraka cha ndoa,kama tungelijifunza tukafahamu mitaa ya ndoa, ramani ilivyo, na mpangilioa wake, katu hatungelipotea.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka zangu...ahsanteni sama. Justin wala usiogope...ray kakangu mfano mziti Usengwili. Emu-3...hakika umenena kwanini hakuna shule ya Ndoa? Au kwa nini kukimbilia kuoana kabla kujuana?

Mfalme Mrope said...

Ndoa ndoano na kuishi ni kusikilizana. Bahati mbaya sana ndoa nyingi ziko katika hali ya taabani na wajuao ni walioko katika ndoa hizo. Habari njema ni kwamba hakuna awezaye kuwatatulia matatizo yenu bali ninyi wenyewe. Ni vema kuamshana usingizini pale pasipo na maelewano. Tatizo kubwa nilionalo mimi ni pale mmojawapo anapokosa upeo wa kuona lipi ni baya na lisilompendeza mwenza. Hali hii kwakweli ni hatari kwa ndoa na mara nyingi huelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi...Ni mawazo tu...

sam mbogo said...

Kuolewa amakuowa, nikitu kizuri sanaaa. ubaya ama uzuri unakuja wakati tendo hilo la kuowana lisha fanyika!!? kila mtu mume au mke anajuwa aliko mpata mwenzi wake,na miongoni mwenu mnajuwa nini kiliwafanya au kuwasukuma muowane. kiukweli wa tu hukurupuka katika maamuzi ya kuowa amakuolewa inabidi kujipanga vizuri.haya yote tuna yo jadiri sasa ni matokeo ya kutokuwa makini na maamuzi yetu ya awali. mfano mtu kisha onyesha dalili za kukupiga kibao ama kakupiga kabisa ,lakini bado uamkubali akuowe,ukitegemea atabadirika, kumbe ndo unakuwa umeji palia mkaa. ushauri wangu kama ndoa inakusumbuwa na unakiri kabisa huwezi kuvumilia au hamuwezi kuelewana tena toka ndani ya ndowa,anza upya kwani kwa wana wake,zamani walikuwa wanaogopa kurudishwa kwa wazazi,lakini sikuhizi mwanamke akiachika hasemi naenda kwa wazazi utamsikia akisea siwezi kushindwa kuishi,hapo ujuwe anaweza kusimama ka ma yeye .kaka s