Thursday, June 6, 2013

LEO TUBURUDIKE NA KIODA KUTOKA KWETU LIULI KARIBUNI!!!


Liuli ni moja ya vijiji ambacho kipo kando ya ziwa Nyasa ni maarufu kwa hospitali na jiwe hili hapa chini ...pia kahitoria kidogo juu ya hili jiwe na mji wa Liuli..

Jiwe la Pomonda

Miongoni mwa miji muhimu katika wilaya ya Nyasa ni mji wa Liuli. Mji huu unayo bandari muhimu ambayo hutumiwa na meli zinazofanya safari katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. meli za Mv Iringa na Mv Songea zimekuwa zikitia nanga katika bandari hiyo ikiwa ni sehemu ya kukuza uchumi, usafirishaji bidhaa na kadhalika.
Katika rekodi za kihistoria kuna mengi ya kukumbukwa katika mji wa Liuli, lakini jambo muhimu ni kuwepo kwa Jiwe hilo ambalo linalinganishwa na sura ya binadamu. Ukkchunguza jiwe hilo utaona linafanana kidogo au kuwa na maumbile fulani yenye sura ya binadamu.
Ni historia nzuri na tamu kwa wakazi wa nyasa na vitongoji vyake. Jiwe hilo lipo karibu kabisa na Bandari ya Liuli ambapo kila abiria au msafiri yeyote anapotumia bandari hiyo ataweza kuliona. Ni moja ya vivutio vya Utalii katika mji wa Liuli. KARIBUNI WATALII, KARIBUNI LIULI kujionea mengineyo.

3 comments:

MTU KWAO said...

Ukweli utamu wa utamaduni na nyimbo na hata mavazi ,ngoma ,na mambo ya mila na desturi ni kitu cha kukupa furaha kama ukiona ngoma nyingi za kiafrika hasa hapa kwetu utapenda na kufurahia umahiri wa kucheza na tabasamu analokuwa nalo mleta ujumbe kweli mimi binafsi napenda muziki wa asili yaani ngoma
che jiah

ray njau said...

Utamaduni ni kioo cha jamii husika.

Yasinta Ngonyani said...

MTU KWAO..AMA KWELI MTU KWAO..hakuna kitu kizuri kama ngoma za asili lakini naona siku hizi watu wengi wanadhalau miziki ya asili na kutaka hii ya kisasa.

Kaka Ray:::hasa umenena..Ahsanteni kakazangu...DUMISHA LILILO LAKO NA ACHA LISILO LAKO.