Friday, June 28, 2013

NIWATAKIENI IJUMAA HII YA MWISHO WA MWEZI KWA MLO HUU...MAKANDE!!!

Karibuni tujumuike na mlo huu wa makande/ngánde/makandi..au sijui wewe kwa lugha yako unasemaje..Nimeona si vibaya kama Ijumaa hii ya mwisho wa mwezi huu tukimaliza kwa mlo huu mzito.Ijumaa njema na mwisho wa juma uwe mwema kwa wote.

17 comments:

emuthree said...

Mhh, hapo umenifikisha home!

Unknown said...

Usangi hiyo naiona mbele yangu, kishukuri chedi.

Unknown said...

Usangi hiyoo, kishukuri

ray njau said...

Watani zangu wapare shughuli imempata mwenyewe au???????????

Yasinta Ngonyani said...

emu-three!! nafurahi kama nimekufikisha kunyumba.
Nancy!..kwanza karibu sana kibarani..na ahsante
Kaka Ray..:-)kumbe ni chakula muhimu cha wapare? mimi nilikuwa najua hasa kule ubenani na upangwani...

Amina mnzava said...

Dada yani hapo nipo nyumbani yani umenitamanisha sana

Yasinta Ngonyani said...

Amina....karibu ...au je huwezi kuandaa unajua vyakula vingine huwa tunasahau tupo na ugali kila siku..

ray njau said...

Watani zangu wapare hizo ni pure ja spesheli avae!

Amina mnzava said...

Ahsate dada yote haya nikujiendekeza tunasahau vakula vaasili eti mpaka uende nyumbani ndio ule tena kwa mwaka mara moja ngoja nianze kudumisha mila

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray...hiyo lugha imenishinda wapare labda wanisaidie
Amina! Ni kweli lazima kudumisha mila nipo tayari kuwa pamoja nawe.

Unknown said...

Pure ja spesheli avae, me mwnyw mpare ila hapo cjamsoma vyema, unajua dada ngoja nkwambie kitu yaani wapare tupo magroup mng kweli nahis hicho kipare ni cha same na nlichosema mm (kishukuri chedi)yaani makande mazuri hicho ni cha usangi dadaangi dadaangu.

Unknown said...

Asante nshakaribia dadaangu.

Nicky Mwangoka said...

Safi sana wanikumbuka mbeya Milima ya Uporoto kabisa. Nimesahau email yako nataka nikutumie habari fulani unitafsirie


ray njau said...

Hiyo pure ni kutoka kule Same.

Yasinta Ngonyani said...

Nancy! nimekuelewa na kama umekaribia basi nasema tena karibu sana.
Kaka Nicky! nafurahi kama umepata kumbukumbu ya milima ya Uporoto..Kuhusu email jaribu kuangalia tena utaipata
Ahsante kaka Ray..naona wote Nancy na mimi na wengine tumepeta jibu.

ray njau said...

Havache thana Mcheku Yasinta!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Wasukuma haya tunaita MASANGU...LOL !!!