NI KAZI YA DADA CAMILLA 2013
hapa pia ni kazi ya mikono ya dada/binti Camilla mwaka 2012
na siyo Dada/Binti Camilla tu hata Kaka/kijana Erik naye anaweza ni kazi ya mikono yake mwaka jana 2012
..Na mwaka huu 2013 tena jana amekuja na hii..Hakika kama mama mzazi nimefurahi sana kwa jinsi mikono yao ilivyofanya kazi nzuri. Sina haja ya kununu mito ya mapambo wanangu wananisaidia...Nina haki ya kusema naona FAHARI sana kwa kweli......proud/stolt. ALHAMIS NJEMA KWA WOTE:-)
7 comments:
Ni fahari watoto kujifunza kazi za mikono kama ujuzi wa ziada dhidi ya masomo ya kawaida wanayofundishwa shuleni. Kwa mifano hiyo ya kazi zao nzuri ni dhahiri kuwa wanaweza. VIPAJI NA VIPAWA VYA WATOTO VIKIENDELEZWA NI URITHI MKUBWA KWA WATOTO KUJIWEZESHA WENYEWE PALE WATAKAPOKUWA WAKUBWA.
Mmh...mmh!! Hawa watoto wanakoelekea utakuja tuambia...
Hongereni sana kwa kazi nzuri za mikono yenu..
God bless..
Yan nimeipenda hiyo tupo pamoja mpendwa
Kazi za Nyumbani za Kila Siku kwa Ajili ya Watoto
================================
“Wazazi wa leo wenye shughuli nyingi huwa walegevu kuhusu kusaidiwa kazi za nyumbani na watoto wao,” laripoti The Toronto Star. Ijapokuwa kazi za kila siku “hazitawahi kuwa jambo la kutangulizwa na watoto,” asema Jane Nelsen, mwandishi wa Positive Discipline, kazi hizo “huwafanya watu wajitegemee na kujistahi.” Kulingana na uchunguzi katika gazeti Child, kazi fulani halisi za kila siku katika nyumba kwa ajili ya watoto wenye umri wa kati ya miaka miwili hadi mitatu zingeweza kutia ndani kuokota vichezeo na vilevile kuweka nguo chafu ndani ya kikapu. Watoto walio na umri wa kati ya miaka mitatu hadi mitano wanaweza kupanga meza, kupeleka vyombo kwenye beseni ya kuoshea vyombo, na kusafisha mahali wanapochezea. Wale walio na umri wa kati ya miaka 5 hadi 9 wanaweza kujitandikia vitanda vyao, kuokota majani, na kung’oa magugu, ilhali walio na umri wa kati ya miaka 9 hadi 12 wanaweza kufanya kazi kama vile kuosha na kukausha vyombo, kutupa takataka, kukata nyasi, na kufagia mkeka. Nelsen aongezea kwamba “kunakuwa na matokeo mazuri unapowawekea muda wa kumaliza kazi hizo.”
kaka Said, dada mkuu msaidizi, emu.3 na kaka ´Ray..ahsanteni sana ,,,yani wamenipunguzi ghalama ya kununu mito ta kupamba nyumba najisikia fahari sana. Namshukuru Mungu pia walimu wao.
Kazi nzuri sana Mungu aendelee kubariki kazi za mikono yenu..
Nimerudi tena. Jamani hii sanaa haiishi hamu kuangalia.
Post a Comment