Tuesday, June 4, 2013

MILA NA DESTURI:- NI WAZO LA LEO KUTOKA KWA DIARY YANGU....EBU SOMA HAPA CHINI!!!

Katika pitapita zangu kila siku nakutana na mengi sana katika blog nyingi na hivi karibuni nilikuwa nimepita hapa na nikakutana na WAZO la mwanablog mwenzetu nimelipenda wazo lake nami nikaona si mbaya kama nikaleweka hapa ili kueneza wazo lake.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WAZO LA LEO: Mila na desturi zipo, na tumezikuta kwa wazee wetu, zipo nyingi, na nyingi hatuzijui tena kwa vile huenda hazikuwezekana kutekelezeka. Lakini kuna mambo mengi mazuri tumeyapuuzia, na kwa kufanya hivyo tumejikuta tukipata taabu sana,…nachukia kwa mfano wa kutafuta mchumba, kabla mtu hajaoa au kuolewa, wazee wetu walikuwa wakihakikisha kuwa mke au mume wa kuoa au kuolewa anatafutwa kwa kufanyika uchunguzi wa kina kwenye familia anayotoka…ni ni hekima yake, ni kuwa kwa kumpata mume au mke bora ni kwa ajili ya kizai bora, na matokeo yake ni kuwa na familia bora na hili litaweza kujenga taifa lenye amani, hili tumelipuuza, na matokea yake ndio haya..
Pia wazee wetu walikuwa wakiangalia kuwa huyo anayeolewa au kuoa, hana matatizo yoyote ya kiafya au ya kurithi, au tabia za kishirikina, au tabia zozote mbaya…haya yalikuwepo na ukiyachunguza kwa makini utayaona kuwa yalikuwa na faida zake, lakini huenda haya na mengine mengi hayapo tena tumeyapuuza.
Wazo langu la leo. Zipo mila nzuri, tuzifuate, na kama zipo mila potofu, tuziache, au tuziboreshe ziwe bora zaidi, lakini tusisahau kabisa mila na desturi zetu zenye hekima ndani, na kukimbilia mila na desturi za wenzetu,….kwanini tupuuze mila zetu, ….huo ndio utamaduni wetu na anayeacha utamduni wake ni mtumwa.
NIWATAKIENI JUMANNE NJEMA NA KILA MTAKALOTENDA LIWE NJEMA...UJUMBE TUPENDANE....KAPULYA WENU

11 comments:

emuthree said...

Tupo pamoja ndugu wangu

Yasinta Ngonyani said...

emu-three!
Kabisa pamoja daima.
Mila zetu... kuchaguliwa mchumba hii huwa mara nyingi inajitokeza katika jamii. Lakini binafsi pia napinga kidogo kwanini wazazi wanichagulie mchumba wampendao wao? Je? ni wao au mimi nitaishi na huyu mchumba? kwa sababu binadamu tumeachana kwa kupenda. ndiyo sikatai, inawezekana lakini ni lazima pia liwepo penzi si kuishi na mtu ambaye hata humpendi. Ila wakati mwingine huwa tunapenda sana kuoga mila za wengine na kuacha mila zetu za asili..TUACHE KUIGA JAMANI.

Justin Kasyome said...

Mim nadhani kuchaguliwa mchumba lilikuwa jambo jema sana na lingefaa hadi sasa ila kwa ulimwengu wa sasa ni ngumu sana maana tayari kuna utandawazi na tumetawanyika kutoka sehmu moja (mahameni!) Suala waliolkuwa wanangalia wazee wa zamani upende wa afya, sasa linachukuliwa moja tu la UKIMWI, ndio maana kuna utaraatibu wa kupima kwanza kabla ya ndoa!

sam mbogo said...

kwa wakati huo wazazi walikuwa sahihi kukuchagulia mchumba,kwani sababu zao kwa wakati ule zilikuwa sahihi.sasa hivi tumezidi kihelehele wakati mwingine tukijichagulia wenyewe tunajikuta tunalala mika,hivyo kwangu mimi kutafuta mwenzi wako ,nimuhimu kujuwana kwanza,hatakama umetafutiwa,umetafuta ni bora kwanza kila mtu alizike/ridhike na huyo mtarajiwa wake. kaka s.

Mija Shija Sayi said...

Naungana na M-3 upo juu kaka yangu! Hata kipindi kile nadhani pamoja na kwamba tulikuwa tukitafutiwa lakini nadhani tulikuwa tunashikirikishwa ili kuanza kumpenda na mapema.

Lakini tukiangalia kiundani hadi sasa hivi bado ni kama tunachaguliwa kiaina... Maana unapompeleka kumtambulisha mchumba mara nyingi wazazi huanza kudadisi hiyo familia na kama ikiwa na matatizo wazazi hugoma kumwoza au kuoa huko..

@Kaka S, Vipi siku moja Kili akuletee mjukuu wa Osama aseme ndo anataka kumwoa?? hahahahahahaaaa...

Pamoja daima....

SAm mbogo said...

Kama mimi baba yake sikuchaguliwa mke na mtu,ila mazingira ndo yalinisaidia kupata mke,na ukizingatia sikukurupuka,na akili yangu ilikuwa timamu,siwezi kumkataa mjukuu wa osama ilimradi uosama wake siyoKATIKA JENETIKS kwa ushauri na mazungumuzo yatatawala ili chaguo lake likamilike.ila snto mkataza asilani. halafu wewe Mija !! je na wewe mmoja wa mabinti zako akataka kuolewa na mmoja wa wajukuu wa MZEE MANDELA. KAKA S.

ISSACK CHE JIAH said...

Ni wazi kusema kuwa mila na desturi za wakati ule zimepitwa na wakati ,tukubali tusikubali majuzi nilisema juu ya mtandao wa simu kwa sasa huwezi kumzuwia mtoto wangu kuolewa na mtoto wa osama wala wa mandela kwani utakuta watu wanapokutana kwenye fesibuku je utawazuwia ,niliongea juu ya dada yangu aliyeolewa enzi hizo na picha tofauti na miaka hii,tuache kukumbatia mila za zamani kwani utakuwa tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele tuwe na siku njema
CHE Jiah

Mija Shija Sayi said...

Asante kaka S kwa jibu lako. Nimependa sana uliposema ilimradi uosama wake usiwe kwenye JENETIKS, Nadahani hii ndio sababu kubwa ya wazazi wetu enzi zile kuchagulia watoto wao wachumba...(kuangalia kwanza mtoto wao anakwenda kujiunga na watu wenye JENETIKS za namna gani.)

Kuhusu mwanangu kuleta Mjukuu wa mzee Mandela, eeebwanaee... hizo dua kwanza naomba zitimie aisee..nitafurahi sana kuletewa mkwe kutoka kwa mzee Madiba maana wana JENETIKS za UANAHARAKATI kama DA'MIja hapa..LOL!!

Ila pia nitamshauri ahakikishe amempenda mume na si JINA..

Ni hayo tu kwa sasa...

ray njau said...

vema!!

Yasinta Ngonyani said...

Inspiration stories! KWANZA karibu tena hapa kibarazani...kutafutiwa mchumba ni safi lakini pia unahitaji kumpenda sio wazazi wampende je ni wao wataishi naye?..

Mija..kazi ipo sasa...

Kaka S:-)

Kaka ISSACK CHE JIAH! dunia hii:-)

Mija :-)

Kaka Ray: ni vema haswa:-)

Salehe Msanda said...

Ni wazo jema sana kutukuza mila zetu.Yanayotokea sasa hivi ikiwa na malalamiko ya kumomonyoka kwa maadili katika jamii
ni kutokana na kuacha kuzingatia masuala ya mila,desturi na utamaduni wetu.
Ukiondoa mfano wa suala la kuoa/kupata mchumba kulikuwa n suala la malezi katika rika mbalimbali zikitanguliwa na Usimamizi uliokuwa unaongozwa na bibi na babu kwa watoto wadogo kwa kusimuliwa hadithi nyakati za jioni na usiku.
Lengo lilikuwa kutuonyesha umuhimu wa kuwa pamoja kama familia na kuwekewa misingi ya kutimiza majukumu ya kila rika.
sasa hivi bibi na babu wa watoto wetu ni Tv ,Magazeti ya Udaku na radio Fm. Kazi kwelikweli.
Kwa kukumbushana suala hili tunaweza kuisaidia jamii kujali masuala ya msingi ya malezi ya vijana na hata kama si kurudisha utaratibu wa jando na unyango basi itafutwe namna bora au ya wakati huu ili kuwa na utaratibu wa kuwa na malezi yenye mwelekeoo unaoleweka.
Kila la kheri.