Thursday, June 27, 2013

LEO TUANGALIA NENO WIVU....

WIVU:- Ni hali au tabia ya mtu kusononeka au kukasirika kwa muda mtu amuonapo mpenzi au rafiki yake ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine. Hii ni tafsiri ya KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU.
Na hapa sasa nilikuwa namsikia marehemu mama yangu akiimba wimbo huu alikuwa mpenzi sana wa zilipendwa utadhani yeye ndio alikuwa redio:

Wivu ukizidi nyumbani mapenzi yanapungua,
Wivu usio na maana waleta hasara,
Umefanya kitu gani bibi umemkataza kufanya kazi
Ati sababu achelewa nyumbani.

Sikumbuki ni nani aliimba nilikuwa msichana mdogo kiasi kwamba hata sikujua neno wivu maana yake ni nini. Inasemekana ni muhimu kuwa na kumwenea umpendaye, Maana mapenzi bila wivu si mapenzi. Kwamba haiwezekani mtu ukae tu, vitu vinatendeka mbele ya macho yako ambavyo vyaweza kukutia mashaka na wewe ukakaa tu bila kuona wivu. Huo ni ubinadamu kwani binadamu tuna silka ya wanyama, huwa tunaweka maeneo yetu alama kama wanyama ili wasiingiliwe na wengine.Hii yote ni kuonyesha wivu.......!!!Wengine wanasema wivu sina ila roho inauma...Je roho ikiuma sio ndio wivu???

6 comments:

Mfalme Mrope said...

Penye moto pakifuka moshi hiyo ni kawaida...penye penzi pakifuka wivu mnashangaaaaa!!! Wivu ni kinga ya mapenzi dada... ila wivu ukizidi mwe! inakuwa karaha tupu...

ray njau said...

Wivu una pande mbili:
1.Chanya
2.Hasi.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka mrope! Ndo hapo sasa halafu pia kuna wivu mzuri na mbaya......yaani kumwonea mtu wivu wa maendeleo hui mzuri. Ila ulewa kumtakia mwenzako mabaya huo mbaya

Justin Kasyome said...

inategemeana na aina ya wivu kweli, ila unapomwonea wivu mwenzio hadi anapopigwa simu kwa mfano na mfanyakazi mwenzeke wa jinsia tofauti na yake, huo ndi wivu mbaya maana utamfanya akose amani ya mawasiliano!

Nancy Msangi said...

Da hii mada imenigusa kweli dada naomba pia ushauri wako me mahusiano yamenishinda kabisa wanaume sitaki hata kuwasikia, cjui nifanyaje dada

Nancy Msangi said...

Da hii nada imenigusa Sana dada mm sipendi kbs wanaume yaani nawachukia basi tu