Monday, June 17, 2013

LEO TUANZE JUMATATU NA KUANGALIA SHULE HIZI ZA KATA YA WINO TARAFA YA MADABA WILAYANI SONGEA!!!

Ifinga ni kijiji ambacho kipo kata ya Wino kutoka barabara kubwa kama inavyoonyesha kwenye kibao ni km 48. Kijiji hiki kinajulikana sana kwa kilimo cha mpunga na machungwa...Mwaka 1992 tulifanya safari mpaka Ifinga tulichukua chumvi nasi tulipata machungwa mengi sana . Kijiji hiki wanakula sana wali hakuna ugali. Ninachoshangaa mwaka ule kulikuwa hakuna hata shule sasa leo napita hapa naona kibao Ifinga Matumbi Secondary school..nikaona ni lazima nipige picha..najiuliza sijui ni maendeleo au ili mradi kila kijiji kiwe na shule?
Kwa sababu mwanzo kulikuwa na shule yetu hii  Wilima ndiyo ilikuwa ya kata. Lakini nayo sasa imeendelea na kuwa High school. Nakumbuka mengi sana kuhusu shule hii....Wilima Sekondari. Kuna nyingi kumbukumbu zinazowahusu watu wengi...Jumatata njema....

4 comments:

ray njau said...

Elimu ni bahari,haina mwisho na ni ufunguo wa maisha.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray ni kweli..Lakini je kuna walimu kutosha au ndo kuwa na shule tu? nimewaza tu kwa sauti jamani

Mija Shija Sayi said...

Kwa upande wangu naona ni afadhali iwepo hata kama haina waalimu kabisa, hii inaonyesha japo kuna matumaini ya watu kutaka elimu. Sasa inakuwa ni kazi kwao kufanya bidii ya kupata waalimu.

Ni hayo tu Head Prefect.

ray njau said...

Elimu kwanzaaaaaaaaaaaaaaaa!!