Wednesday, March 21, 2012

UTAFITI: KUNYONYESHA HUZUIA KANSA YA MATITI KWA ASILIMIA 25-60

Tusiacha kunyonyesha vichanga wetu jamani


Mara nyingi nimekuwa najiuliza hivi kwa nini akina mama hapa niishipo hawapendi kunyonyesha watoto wao. Utakuta mtoto ana miezi mitatu amekwisha achishwa kunyonya. Anapewa hii mipira (kidanganyio) kutwa nzima kisa eti akima mama wanaogopa matiti yao yatakuwa kama "chapati"....kwa mimi wala sielewi kabisa . Ebu soma hii makala hapa chini.......
Ambayo nimeipata kutoka kwa kaka Matondo nikaona si mbaya kama tukijikumbusha na pengine kuna waliokosa kuisoma. SI WOTE TUNAKUMBUKA NI JUMATANO NI KIPENGELE CHA MARUDIO
----------------------------------------------------------------------------------------------
Mbali na ukweli kwamba kunyonyesha ndiyo chanzo cha lishe bora kabisa kwa mtoto, wanasayansi sasa wanadai kwamba kunyonyesha pia kunaweza kupunguza uwezekano wa mama kupata kansa ya matiti kwa asilimia 25 hadi 60.

Hizi ni habari njema kwa akina mama wa Afrika ambao kimsingi huchukulia kunyonyesha kama mojawapo ya wajibu wao baada ya kupata mtoto. Pengine hii inaweza kuwa ndiyo sababu iliyofanya saratani ya matiti isijidhihirishe sana Afrika.

Wasiwasi wangu ni juu ya kizazi kipya ambacho kinaiga mambo ya Kimagharibi kwa pupa. Nimeshasikia kwamba mabinti wengi sasa hawana hamu tena ya kunyonyesha vichanga vyao wakichelea kuharibu matiti na miili yao. Ukijumlisha na vitu vingine vinavyoingia Afrika vikiwemo vyakula vilivyolimwa "kisayansi", madawa na mabadiliko mazima ya mfumo wetu wa maisha, sitashangaa kama kansa itafumuka na kuwa ugonjwa wa kawaida tu muda si mrefu ujao. Hili likitokea, atakayefaidika bila shaka ni makampuni ya madawa ya nchi za Kimagharibi - na naamini kwamba hiki ndicho wanachotaka. Tuweni waangalifu na tuache mambo ya kuiga vitu kiholela bila kuelewa hasa kiini chake.Ukitaka kusoma zaidi gonga hapa. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE!!!!!

14 comments:

Simon Kitururu said...

Mmmh! Ila kuhusu hizi tafiti haki ya nani -kila ikuambiayo kula hata machungwa kuna faida kuna tafiti nyingine itakuambia kula machungwa kutakuua. Nawaza tu kwa sauti wakati nikifikiria jinsi tafiti mbali mbali zinipavyo majibu tofauti na yote yasemekana ni KWELI!:-( Ila titi lililotuna lina sumaku zake kimtuno - na hii nasema bila kudharau titi chapati kwakuwa mie ni mtu wa chuchu na chuchu ikituna tu vizuri mie nafarijika!!:-(

sam mbogo said...

Kwa asili watanzania niwatu wakuwa wanakumbushwa kila mara.nahii pamoja nakuwa yaweza kuwa nikazi ya serikali kwa pamoja na viongozi,watu/akina mama inabidi waambiwe tena nakiongozi mkuu/muhusika kuwa wanyonyeshe watoto,kwa muda mrefu kama inavyo takiwa. na sikweli kuwa watu wa magharibi hawanyonyeshi hapana wananyosha sana tu.hawa dada zetu niushamba tu hakuna walijuwalo juu ya usemi huu kuwa wazungu huwa hawanyonyeshi.wazungu hawanyonyeshi hadharani ila wananyonyesha.ukikuta hanyeshi ujuwe kunatatizo la kitaalamu.wanasahau kuwa nyumbani maranyingi ugonjwa wa marelia unawapata sana watoto,sasa kama mtoto hanyonyeshwi vizuri na mama atapata wapi kinga ya mwili? lazima itoke kwa mama kutokana na maziwa anayo nyonya,wananikera hao wanao kataakunyonyesha bila sababu ya msingi ,eti wanaogopa maziwa yao kua chapati kwenda zako/zenu chapati huliwa vilvile!? siyo kila kitu msikiacho cha ulaya ni bora acheni hizo,na kweli mkicheza mikansa itawaumbua.pia msikimbilie kuwapa maziwa ya kopo,kuwa nauwezo siyosababu kwamba mtoto hata bado hajafika wakati wa kutumia maziwa hayo ,nazaidi maziwa yenyewe kiafya/kitaalamu hamjuwi madhara yake,acheni bwana mnaudhi.bongo kuna kila kitu,mtoto akifikia muda wa kuanza kua mpe vitu vya nyumbani,viazi,matunsa ,uji,nk utakuta sikuhizi eti nawao wananunua vyakula vya watoto vya chupa/kopo, upuuzi huo mnawanyima watoto vya kula bora vya nymbani.ukija kwenye pampasi!!!? ndo usiseme kila mtu bongo pambasi nepi ni za kizamani.sikilizeni siyo kila mtoto akishazaliwa anavaa hizo mnazo ita pampasi,kuna nepi kwanza halafu nepi yenyewe yaweza kuwa nguo laini,kama kanga iliyotumika,wengi wenu mnajuwa hili ila ushamba tu .kuweni makini na pampasi zina tofautia viwango pia nahali ya hewa bongo ni joto sasa unakuta mtoto kavalishwa hiyo kishapiga puu!!? we achatu. badirikeni dada zangu. mambo taratibu msikurupuke.kaka s.

sam mbogo said...

Mkuu Kitruru,nakubaliana nawe kuhusu hizi tafiti,kiukweli nyingi zina changanya hasa hizi za kuhusu vyakula.sasa hivi tunaambiwa nyama nyekundu mbaya sana,sasa wale wazee wetu wa kisukuma,kimasai nyama wanakula kwa sana ,na wamasai kwa kusikia sina uhakika ni hili huwa hawali samaki.kwa maana hiyo nikuwa makini na kuwa na nidhamu na maisha yako kwa ujumla. Uchokozi-sasa mzee wa chuchu inakuwa je mkianza nyanganyana chuchu ya mama na mwanao!!? ila mwanamke akiwa chapati doh!!!!!? kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Kama kawaidi WaTanzania/waafrika tunavyopenda kuiga. Kinachonishangaza kwanini tusiige mambo yanayoleta maendeleo?..kama walivyosema waliotangulia kwanini usimnyonyeshe mtoto na badala yake unampa hicho kidanganyio..hakika kama watu tungejua ni vipi maziwa ya mama yalivyo kinga kwa mtoto..nikiwa kama mama nimenyonyesha wanangu na wameepuka na malazi mengi sana. Naweza nikasema wale walionyonyesha wanao miezi mitatu na mimi niliyenyonyesha miaka 2-3 matiti yao ni chapati zaidi kuliko yangu..

Kaka Simon nimefurahisha sana .."chuchu ikituna"
Na kaka sam leo umepasua safi sana ngoja tuone akina dada watasema nini....

ray njau said...

Ni tafiti maridhawa zenye tija kwa umma.

Rachel Siwa said...

Mmmm hii mada ya leoleo!!Asante da'Yasinta kwa kuleta hii mada, pia kaka wa mimi Kitururu a.k.a Mzee wa chuchu, duh Che Bwana wee Sam, Umeleta elimu tosha pia hapa,Mimi nimejifunza sana kupitia nyie,bila kukusahu kaka Ray.Kuongezea tuu si kila wafanyavyo Wazungu ni kizuri kwako, labda wao wanafanya kwa sababu muhimu, kulingana na Mazingira yao au Tamaduni zao.GEZAGEZA YAMSHINDA MUINGEREZA!!!!

Simon Kitururu said...

@Dada Rachel: Haki ya nani hizi chuchu sijachoka kuzinyonya na zikituna -MIE kwangu faraja KIBONGE!

Rachel Siwa said...

Hahahahaha kaka wa Mimi Kitururu,Fanya mambo ndugu yangu uwe nazo/umiliki zakwako kaka yangu,ili usihangaike!lakini unajua wengine hawana chuchu mpaka hawawezi kunyonyesha?

Simon Kitururu said...

Hivi kunawasio na CHUCHU? Hii ni kitimoto unayo nipa ambayo sijawahi kukutananayo!:-(@Dada Rachel

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! unataka kusema kuna watu hawana kabisa chuchu? Mimi najuavyo/nielewavyo watu wote wana chuchu...lakini zile zitoazo maziwa ni za mwanamke tu. AU?

Anonymous said...

yaani watu kuiga halafu ulimbukeni,kuna jamaa yangu mtoto anamwezitu eti maziwa ya kopo na wakati mamaya mtoto yuko fiti,ili waonekane wanavijisenti ndio wanajidai kununu hayo maziwa sasa mimi ushamba wa namna hiyo huwa sipendi nikawambia mtamuumiza mtoto hivivitu maziwa ya kopo sio mazuri kama mamamtu hana matatizo nikaonekana ni ninawaonea wivu kwa vile wana vijisenti lakini mtoto kilasiku anaumwa,mara tumbo,mara mafua mimi aaa naangalia wanavyopata tabu kwakujisababishia wao wenyewe...........na kama mama ananyonyesha usipokuwa makini na ile chuchu inavyotuna mhhhhhhhh.....usishangae mama ataendelea kunyonyesha kila baada ya miezi sita....???!!!nampa pole mzee wa mawazo....

ray njau said...

Hakika yabarikiwe matiti tuliyonya na mikono salama iliyotulea hadi tukaweza kukutana hapa kibarazani kwa binti Nangonyani kipenzi cha wadau wa maisha na mafanikio.
-------------------------------------
Binti Nangonyani kauliza swali au kahoji uumbaji wa Mungu,hakika mimi sipati mwelekeo kamili.Labda wanazuoni mahiri na makini katika tasnia ya sayansi ya maumbile na jinsia waibuke majibu yao.
-----------------------------------
Mimi najuavyo/nielewavyo watu wote wana chuchu...lakini zile zitoazo maziwa ni za mwanamke tu. AU?_Yasinta Ngonyani a.k.a Kapulya.
----------------------------------

ray njau said...

"HAKIKA YABARIKIWE MATITI TULIYONYONYA NA MIKONO SALAMA ILIYOTUPATIA MALEZI NA MAADILI MEMA"

Seleman Awadh said...

mimi kwa mtizamo wagu akina mama wa sasa hivi hawataki kukubali kwamba wao ni akina mama kwa sababu mtu umeshakubali kuzaa lazima pia ukubali kuitwa mama tofauti na ulivyokuwa msichana na pia kuachana na mambo aliyokuwa akifanya wakati wa usichana,lakini vinginevyo hali itaendelea kuwa mbaya endapo akina mama hawatajikubali na kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo & kuachana na dhana kwamba akinyonyesha matiti yatalala,kwani mama ni mama tu na msichana atabaki kuwa msichana kwa wakati huo ambao atakuwa ni msichana.asante!