Tuesday, July 3, 2012

UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!



Leo kabla ya kusema neno baya, mfikiria mtu ambaye hanawezi kusema.
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu ambaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mno amekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendesha gari lako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni mchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako yako. Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!! 

11 comments:

Interestedtips said...

kwakweli maisha ni zawadi..tunahukumu sana na kulalamika sana...tunatupa chakula ovyo tukijidai tumeshiba au kimetukinai tukisahau ambao hawapati hicho chakula.....ujumbe mzuri sasa dada

Usengwile????

ray njau said...

Wewe ukisema cha nini na mwenzio wanasema Mungu wangu nitakipata lini?Ukisema sitaki hiki siyo kitamu na na mwenzio anasema kwa uchungu wake huo mimi nipeni.Wewe ukiomba viatu na mwenzio anaomba miguu.
--------------------------------
Nenda, ukale chakula chako kwa kushangilia na kunywa divai yako kwa moyo mchangamfu, kwa sababu tayari Mungu wa kweli amependezwa na kazi zako.Katika kila pindi, mavazi yako na yawe meupe, wala kichwa chako kisikose mafuta. Furahia maisha pamoja na mke unayempenda siku zote za maisha yako yaliyo ya ubatili ambayo umepewa na Yeye chini ya jua, siku zote za hali yako iliyo ya ubatili, kwa maana hilo ndilo fungu lako maishani na katika kazi yako ngumu unayoifanya kwa bidii chini ya jua._Mhubiri 9:7-9
===============================

Yasinta Ngonyani said...

Ester! mimi nakwamba kuna watu wanatupa chakula kila siku na tena kingi mpaka huruma yaani...watu wana mivitu na halafu hawatumii wakati wengine wanahitaji

Kaka Ray! yaani basi tu binadamu hatuna shukrani na wala hatutosheki

EDNA said...

Mdada umenena mweeeh!

Mija Shija Sayi said...

Kweli tupu ndugu yangu... tumezidi kulalama bila kufikiri.

nyahbingi worrior. said...

kweli,maisha ni zawadi.

ray njau said...

@Yasita;
Tafadhali tafakari ni uhifadhi maneno haya:
Basi Yehova akaona kuwa ubaya wa mwanadamu ulikuwa mwingi duniani na kila mwelekeo wa fikira za moyo wake ulikuwa mbaya tu wakati wote. Yehova akajuta kwamba amewafanya wanadamu duniani, naye akaumia moyoni mwake.Kwa hiyo Yehova akasema: “Nitawafutilia mbali kutoka usoni pa nchi wanadamu ambao nimeumba, mwanadamu na mnyama wa kufugwa, na mnyama anayetembea na kiumbe kinachoruka cha mbinguni, kwa sababu ninajuta kwamba nimevifanya.”Lakini Noa akapata kibali machoni pa Yehova.
_Mwanzo 6:5-8

Yasinta Ngonyani said...

Edna wa mlongo wangu! Ulongise bé!
Dada mkuu Mija! hakuna kitu tulidhikanacho...Binadamu sisi..
nyahbingi! Yaani haswaaa na halafu tukumbuke katika maisha tunaishi mara moja tu...
Kaka Ray! Ahsante nitafanya kama ulivyoniomba ...yaani kutafakari.

ray njau said...

@Hakika wewe ni mwanazuoni mahiri na makini katika tansia ya habari na elimu kwa jamii.Blogu ni gazeti kama magazeti mengine tunayaona mitaani kwetu.Tofauti ni namna ujumbe unavyowasilishwa kwa wadau na jamii kwa ujumla.Blogu inawasilisha ujumbe na taarifa zake kupitia njia ya elektroniki.Hii ni changamoto kwa wamiliki wote wa blogu kuendelea kuwasilisha kwa jamii kile kitu ambacho kwa kweli ndiyo matarajio ya jamii.Nampongeza sana Yasinta kwa kuendelea kuwekeza muda wake katika kuienzi lugha ya Kiswahili akiwa huko ughaibuni.Kupitia mada hii nimejifunza umuhumu wa kuchagua picha inayofanana na mada husika ili ibebe taswira ya ujumbe uliopo ndani ya mada husika.Picha iliyotumika ni sahihi kabisa nami nahitimisha kwa pongezi na shukrani nyingi kwa Yasinta na wasaidizi wake katika blogu( mama maisha blog) ya maisha na mafanikio.

Anonymous said...

Binadamu hatosheki. Tamaa mbele, mauti nyuma!

obat penggugur said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat cytotec