Saturday, March 17, 2012

MWONEKANO MPYA WA KAPULYA....

Hapa ilikuwa mwaka huu 2012/5/1 nilipopiga picha hii nikiwa nimesuka nywele za kimasai ......
...na hapa ni leo nimefumua zile nywele za kimasai na sasa nipo naturel /yaaani na nywele zangu nilizozaliwa nazo. Watoto wangu wameshangaa kwani nilifumua zile rasta minywele yangu ilikuwa mirefu si kawaida baada ya kuosha zikashiling/rudi na kuwa fupi...Yakajia maswali umenyoa mama?...ila wote wamependa mwonekano wangu mpya . Je wewe unayeangalia ni mwonekano upi unaupenda niendelee nao? JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA :-)

14 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

Rafiki mbogo unauona ugomvi huo anauanza dada yangu? mimi sijtoe maoni mpaka wewe useme kwani mtani wako dada yako anataka kwenda kwenye mashindano ya urembo leo hii jumamosi sasa fanya haraka kumpa jibu ajiandae pe salamu mimi dada ninzachosema ni kuwa nakutakia mashindano mema
Che Jiah

ray njau said...

Muonekano asilia ni maridhawa bila madhara.Wikiendi njema kibarazani.

Mija Shija Sayi said...

Muonekano asilia nao unakupendeza kumbe.. Safi sana.

Umependeza zaidi bila umasai

ISSACK CHE JIAH said...

VIPI Mbogo hujaamka MKWE wangu? mwanagu Rachel Isaac hajakuamsha? Nawe mwanangu Rachel amka toa maoni yako shangazi yako Yasinta anataka kwenda kwenye mashindano ya warembo anataka ushauri wako tao maoni yako mwache huyo mkwe wangu mbogo aendelee kulala mpe maziwa ya ng'ombe anywe akiamka atatoa maoni yake
mimisiwezi kumshauri Dada yangu kuwa anaonkana amependeza au la ila napenda anonekane kama alivyozaliwa pale nyumbani Ruhuwiko
Dada chagua uasilia kama upendavyo kula vitu vya asili
Che Jiah

Yasinta Ngonyani said...

Yaani nimecheka mpaka basi tu..huu wala si ugomvi na wala si kutaka kugombea shindanno la urembo...isipokuwa ni muonekano wa asili yaaani mimi kama mimi...ila niwachekeshe kidogo hapa jana jioni Kijana Erik kaniangalia na akasema mama, unaonekana mzee bila rasta...

Anonymous said...

yaani hapo umependeza sana huyo mwanao anakudanganya wala hujazeeka ,umependeza hasa nywele kipilipili bwana asikudanganye mtu sio hayo mauzi unayajaza kichwani

sam mbogo said...

Haya njomba nachukuru chana, maana baaaa! bwana wewe che Jiah, huyu chemwali Rachel amakweli nakuchukulu kwa kuniachia tulikuwa vile tukicheza likasaula chonde chonde! bwana weweee!. Da Yasinta kiukweli hatua ulio chukua ni bubkubwa safi na uamuzi huo si mchezo unataka moyo.sasa kipengere cha kupendeza, au hujapendeza ni hatua nyingine. kinacho fuata ni matunzo najinsi unavyo taka ziwe,ukitaka ziwe virasta vidogo dogo unaweza kupendeza pia,wewe fanya majaribio nahizo nywele za asili utapata mtindo ambao utakufaa .ila ukitaka nikusaidie nitafute. kaka s.

ray njau said...

Vivyo hivyo natamani wanawake wajipambe kwa mavazi yenye mpangilio mzuri, pamoja na kiasi na utimamu wa akili, si kwa mitindo ya kusuka nywele na dhahabu au lulu au mavazi yaliyo ghali sana,bali kwa njia inayowafaa wanawake wanaodai kumheshimu Mungu, yaani, kupitia matendo mema. _1Timotheo 2:9,10.

Simon Kitururu said...

Jumamosi njema! ... na umependeza!

Rachel Siwa said...

Umependeza sana MWALI WEWE!!!Duhh tumekuwa wengi na Nywele hizi sasa,Jana nilipita blog moja nikakuta wametuua/kutucheka,sanifu Eti ukiwa na nywele hizo/hizi Unatofauti na baba yako!haaahahaha!

@baba yangu Isaack Che nimeamka hahahhhaha maziwa ya Ngo'mbe na bili hizi baba?

Hahhaahahhaha bwanawewe baa Sam mwana wa Mbogo!!!!

@da'Yasinta Erik anawasiwasi hahahhaha.

Fadhy Mtanga said...

Umetoka chicha ile mbaya. nimelipenda pozi la hiyo picha ya chini. safi sana da Yasinta.

Seleman Awadh said...

mwonekano wako ni mzuri sana ila ungesokota dred za asili ungependeza na ukifanya hivyo naomba unitumie picha maana i lke u!

Sara Chitunda said...

mi napenda uonekane kama picha ya pili ambayo umefumua kwani umpendeza sana.

obat telat bulan said...

obat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing cytotec