Monday, September 17, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA IIJUMAA YANGU/WIKIENDI YANGU PAMOJA NA WAFANYAKAZI WENZANGU!!!

 Kula pilau au kujisikia upo Afrika/Tanzania si lazima uwe Afrika /Tanzania.Ijumaa ya tarehe 14/9/2012 nikaamua kuwaalika wafanyakazi wenzangu kuja nyumbani kwangu. Nao wakaja na mambo yakawa kama muonvyo. Niliwaomba wabadili nguo na wavae kiafrika nao hawakusita. kama muonavyo hapa chini.
 Hapa ni maandalizi ya kuaandaa pilau/chakula yanaanza
 Baadhi ya wageni wamewasili
 Tupo mezani tunalichapa pilau kwa raha zote
 Msosi na hadithi zinaendelea ,......kila kitu kilikuwepo
Mpishi na mwenyeji anaonekana hapa pia ...maana ndiye alikuwa mpiga picha za hapo juu



Na mwisho akatokea mpiga picha na tukapiga picha ya pamoja. Waliokaa chini kwanza Yasinta, anayefuatia ni Marlene, waliosimama nyuma yangu ni Pernilla, anayefuatia mwenye batiki ni Ylva na halafu Elizabeth na mwisho ni Maria. Nilifurahi sana kuwa walikubali kuvaaa nguo zangu angalia utadhani walipima wao:-) Na jioni ikaishia hapa. Hakika kwangu na kwa wo pia tulikuwa na siku nzuri sana naweza nikasema tulikuwa nusu ya Afrika/Tanzania. JUMATATU NJEMA.

16 comments:

Rachel Siwa said...

Kweli ukijithamini utathaminiwa, Inapenda sana da'Kadala, Mtu kwao@

batamwa said...

vipi dada Yasinta Marlene ameolewa?kama bado basi nifanyie mpango

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki! Ahsante ndugu wangu..nakuambia hii siku ilikuwa moja ya siku ambazo nilikuwa na furaha sana.
Batamwa! Bahati mbaya umechelewa Marlene ameolewa na ana mtoto tayari. Ila ntamwambia:-)

ray njau said...

@Yasinta;
Hongereni sana kwa tafrija ya ubunifu iliyohanikizwa na upendo mchangamfu kutoka katika sakafu za mioyo yenu.Hakika hiki ni kitu adimu katika orodha ya vitu adimu.

Anonymous said...

hiyo inaitwa B2A...BACK TO AFRICA... nimepipenda sana hiyo sister Yasinta.. du..wazungu wa watu na host mmependazaje? mavazi yetu mazuri sana..ila mmoja hapo kama hana furaha, kulikoni wifi? hahahahahahaha (shangtazi ya Camilla huyo!

sam mbogo said...

mmependeza,na nguoza kitz safi. mwanamke vitenge!? kaka s

Emmanuel Mhagama said...

Viko vitu vya kawaida sana ambavyo vinaweza kufanya mtu akayafurahia maisha na kila nukta ya uhai ikawa na maana. Huu siyo tu ubunifu, lakini ishara za wazi za UPENDO ambao hauhesabu gharama. Hapa kwetu TZ ili uwape watu pilau lazima kwanza uwachangishe halafu ndo uwaite kuja kula pilau, tena huku ukihakikisha kwamba katika vile walivyochanga, kuna vingine vingine vinabaki kwa ajili ya watoto wako. Huo ni upendo au wizi? Unawezeja kuwapenda watu kwa gharama zao wenyewe. Hapo umewapenda au umejipenda? Dada Yasinta naamini hawa wazungu wa watu hukuwachangisha. Kama vile haitoshi, ukawagawia na vitenge vyako wajimwage navyo. WHAT A WONDERFUL LOVE.

isaackin said...

safi sana hii na wenyewe wamependeeza na hayo mabatiki kama wamezaliwa nayo vile

Anonymous said...

yasinta endelea na moyo huu wa kujitoa, umetoa mavazi na vyakula.Mungu akuzidishie pale ulipotoa na akubariki sana.Nimependa huo ubunifu, keep it up.

Mija Shija Sayi said...

Baaaaab kubwa Ysinta!! Mimi sina hata la kusema.

Nimeikagua sana nyumba yako yaani ni Utanzania mtindo mmoja...nimekipenda kitambaa cha meza.

Hongera sana dada mkuu..

John Mwaipopo said...

umebarikiwa mkono utoao kuliko mkono upokeao

gadiel mgonja said...

wooooou! fantastic! mbona umealika weupe tu jaman,dah! hilo bonge la msos.duh kumbe wazungu wanapendeza sana wakivaa kiafrica! ahsante kwa kututangazia utamadun wa muafrica.gud day dadaa.

Penina Simon said...

Nimewapenda mno hawa ladies, kwanza walivyovaa inaonyesha upendo wao kwetu, hv nani aliwashonea hizo vitenge? na wamependezaje jamani!!!!!, wafikishie salaam zangu, i love u all, mwaaa mwaa mwaa,

Yasinta Ngonyani said...

Shukrani kwa wote na salamu nyingi sana kutoka kwa hao akina dada. Siku hii kwa kweli ilinifanye nijione nipo nyumbani kabisa. Napenda kuwashukuru sana akina dada hawa kwa kuifanya siku hii ikawa ni kati ya siku ambazi sitazisahau maishani. Ilikuwa safi kwa kweli kuwa Tanzania/Afrika ndogo:-)

ray njau said...

‘Upendo huvumilia mambo yote. Upendo haushindwi kamwe. ’—1 KOR. 13:7, 8.
=================================================================
Mambo mengi yameandikwa na kuchapishwa kuhusu upendo. Sifa hiyo imetukuzwa na kutungiwa nyimbo za mahaba. Upendo ni uhitaji wa msingi wa wanadamu. Lakini mara nyingi vitabu na sinema zimeonyesha hadithi za uwongo kuhusu upendo, na kuna habari nyingi kama hizo zinazouzwa kwa wingi. Hata hivyo, inasikitisha kwamba watu wengi hawampendi kikweli Mungu na jirani yao. Tunaona mambo ambayo Biblia ilitabiri kwamba yangetukia katika siku hizi za mwisho. Watu ‘wanajipenda wenyewe, wanapenda pesa, wanapenda raha badala ya kumpenda Mungu.’—2 Tim. 3:1-5.
==============================================================
Nafsi yenye ukarimu hiyo yenyewe itanoneshwa,naye anayenywesha wengine kwa ukarimu yeye mwenyewe pia atanyweshwa kwa ukarimu,_Methali 11:25

batamwa said...

asante dada Yasinta ninasubiri jibu kwa hamu sana lolote lile