Friday, August 17, 2012

KUMBUKUMBU:- LEO NI MIAKA NANE (8) KAMILI TANGU MAMA YETU ALANA NGONYANI ATUTOKE!!

KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka nane sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana,  sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!

Na ndiyo maana hii siku sitaisahau maishani mwangu..ilikuwa saa kumi jioni nimetoka kazini na nilikuwa nimepanga muda huo waandishi wa habari wa gazeti la habari mpya za kanisa "Kyrknytt" waje wanipige picha. Kwasababu nilikuwa muhusika mkuu katika gazeti hilo. Ilikuwa mada kuhusi wamisionari wa Peramiho/Songea. Walikuwa na bahati sana wanamaliza tu kupiga zile picha na simu inalia/ita na ndiyo tukapewa habari kuwa mama yetu mpenzi hatunaye tena. Ndiyo maana hili gazeti/picha hii ni kumbukumbu kubwa sana kwangu.
NITAKUKUMBUKA NA KUKUPENDA DAIMA MAMA!!

19 comments:

Rachel Siwa said...

Ulale kwa Amani mama Ngonyani.Poleni sana wapendwa.

Anonymous said...

poleni kwa kumkosa mama

Anonymous said...

mola amrehemu mama yetu na ampuzishe kwa amani na tuzidi kumuombea ili naye utukumbuke ktk ufalme wa mbunguni - hee dada nangonyani kumbe wawanini sana na nyina waku yaani hii picha wala huulizi - nabambu mbawala

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki/rachel!Ahsante kwa kutufariji.

Usiye na jina! Ahsante sana.

Bambu Mbawala! Sala yako ni faraja kubwa sana..ahsante sana. Ahsanti kwa kuwona niwaningini na nyina wangu...

Yasinta Ngonyani said...

Mama! kila wakati nilikuwa nawaza kamwe hutatuacha. Nilikuwa tunataka uwe/ubaki nasi. Lakini yote ni mapenzi ya Mungu. Inanibidi nianze kuzoea. sikuoni kimwili na kushiriki wakati mzuri pamoja.
Kila wakati naiona sura yako katika mawazo yangu, kila wakati najisikia wema wako katika nafsi yangu. Daima nitakukumbuka nitaendelea kutunza upendo wako ndani ya moyo wangu milele. Nitakupenda daima mama!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Apumzike kwa amani!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Apumzike kwa amani!

Rafikio wa hiari said...

Yasinta mama yu pamoja nawe daima!
Wale tunaowapenda kamwe hawapotei kabisa....
bado tupo nao kwa mambo mengi sana tena maalum,
kwa kupitia ndoto walizotuachia,
mazuri walioongeza kwenye maisha yetu,
maneno ya busara ambayo kamwe hayatatutoka
na la muhimu kumbukumbu ambayo daima haita ondoka!
Kwa hiyo rafiki yangu mpendwa wa hiari,
Mama yupo pamoja na wewe daima,
Kwa maana upendo wake upo nanyi daima!
Raha ya milele umpe ee Bwana
na Mwanga wa milele umuangazie,
Mama yetu astarehe kwa amani!
Amina

erik said...

pumzika kwa amani bibi

Camilla said...

Sisi tulikupenda, lakini mungu alikupenda zaidi <3

Interestedtips said...

POLENI SANA WAPENDWA....NAJUA MNAPATA UCUNGU SANA...TENA ULIKUWA UNAFANANA NAYE.....MUNGU AENDELEE KUMLAZA MAHALI PEMA PEPONI ....AMEN

www.malkiory.com said...

Pole Yasinta. Mola awape faraja.

MARKUS MPANGALA said...

Mwenyezi mungu anatambua ya kuwa dunia hii tumekuja na tutalazimika kuondoka. nasi rafiki zako tunatambua kuwa wewe ni muhimu kwetu na sina shaka tutakuwa nawe daima katika shida na furaha zetu duniani. upendo wetu dumu daima

Emmanuel Mhagama said...

Kuna wimbo mmoja walikuwa wanaimba zamani kwenye misiba, sina hakika kama bado unaimbwa. Unasema hivi "Duniani matembezi, sisi sote wasafiri. Tunapandwa ardhini kama mbegu mashambani". Hao waliotunga huo wimbo waliishia njiani, wametukosesha neno muhimu la matumaini. Maandiko Matakatifu yanasema hivi "Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo" (Wafilipi 3:20) Hii ni safari ya kila mmoja.
Hata hivyo hii picha imenikumbusha mbali sana. Kama vile nilimwona jana. May Your Soul Rest in Peace Mama.

Anonymous said...

pepa dada tawoa njila yitu yiyoyo ila tipishana pa kulongolela tu na tutazidi kuwaombea muwe na umoja uliojaa upendo na amani ktk familia yenu - nabambu mbawala

Giancarlo said...

La mamma la persona più bella che ci sia, e resterà sempre nel nostro cuore!! buona serata...ciao

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni sana wote kwa kuwa nasi kwa siku ya jana. Mwenyezi Mungu na azidi kuwapa upendo na ushirikiano kwa wakati wa raha na taabu. Mbarikiwe sana.ruksa kuendelea....

EDNA said...

Pole sana kwa kumpoteza mama.Mungu na akupe nguvu na ujasiri ili uweze kuuhimili upweke.

penina Simon said...

Duh she was so cute, hope tutaonana nae paradiso.