Thursday, August 16, 2012

NYUMBANI NI NYUMBANI:- HAPA NI TASWIRA YA PERAMIHO!!!

Kwa vile jana tulikuwa tumeshafika Songea mjini. Nimeona tuendelee  leo  na kuangalia taswira ya hapa Peramiho kwetu. Hapa kuna huduma nyingi sana kama wengi mnavyojua, HOSPITALI, DUKA LA VITABU/MAGAZETI na bila kusahau  kuna bonge la KANISA pia SEMINARI pia unaweza kupata vyakula vya aina mbalimbali....ALHAMIS NJEMA!!!!

7 comments:

ray njau said...

Asante sana kwa taswira ya nyumbani kwenye ardhi ya wazaa chema.
Hakika baraka ni kwa matiti matamu uliyonyonya na mikono salama iliyokulea.
"Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani".
Salamu!!

ISSACK CHE JIAH said...

ASANTE SANA DADA KWA KWELI WIKI HII UMETUKUMBUKA SANA NA KULE KUNYUMBA HAPO LIPOKELA ,NKAKO,KITAI ,LIKONDE, LIPUMPUMBA ,NA KULE LITEMBO HIVI KWELI WIKI IJAYO UTUELEZE KWANINI MAJINA HAYA YANAANZA NA LI NA YALE YA NAMABENGO, NAMBOLE, NANDEMBO,NTYANGIMBOLE,NKAKO,.LEO UPO PIRAMIHO UMETUELEZA MAANDHARI KWA MBALI TUNATAKA TUONE LIVE MIUNDO MBINU YAKE KWANI KAMA HALI NI ILEILE YA MWAKA 1980 PERAMIHO NAPO HAPABADILIKI? AU KWA VILE NI ENEO LA WATU MISHENI UKWELI JANA NILICHUKIA KUSIKIA KUWA STANDI ILE NILIYOTEREMKA MWAKA 80 MPAKA LEO IPO VILE KUNA RAFIKI ZANGU WENGI TULIOJENGA ULE UWANJA WA MAJMAJI KAMA HUJUWI MWANANGU RECHEL MIAKA ILE TULIKUWA TUNAPELEKWA KUJITOLEA PALE KUSAIDIA KUUJENGA ULE UWANJA TUKIWA SHULE,WEWE MUDA HUO SIJAKUZAA WALA KUFIKIRIA KAMA UTAKUWEPO SONGEA ILIKUWA HALI NGUMU SI SONGEA TUU BALI HALI YA KANDA ILE YOTE ILA KWASASA MIKOA ILE YA KUSINI INAPENDEZA MIMI NASEMA UKWELI KUNA UNAFUU LAKINI UKINIAMBIA PERAMIHO NA SONGEA STAND IPO VILEVILE HAPO NIMECHOKA YASINTA ASANTE KWA KUTUSTUA KUNA MTU MMOJA ANAITWA KAPINGA NILISOMANAE ILA ALIKUWA MBELE YANGU NILISIKIA KAMA AMEKUWA ASKOFU KANISA MMOJA KULE HIVI NYIE MAKASISI NA MAASKOFU MNAFANYA NINI JARIBUNI KUPIGANIA MAENDELEO JAMANIII MWANANGU RECHEL MSALIMIE MCHUMBA WAKO MBOGO SIJAMSIKIA MUDA AU AMEZAMA NA MELI ZILE ZA ZANZIBAR ILE YA NUNGWI?
KWAHERI DADA NAENDA NJE YA OFISI NIKIRUDI NAOMBA MCHANGO WENU MHAGAMA ,MBOGO,RAY NJAU,RECHEL WA ISSACK MWANAGU HEBU LETENI MCHANGO NAWE YASINTA TUNATAKA KUJUA MAJINA YA MIJI HII KWANINI YANAANZA NA HIVYO
CHE JIAH

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante kwa yote na nitafikisha salamu kwa walezi wangu.

Kaka wa mimi ISSACK CHE JIAH! nashukuru kama umepata kumbukumbu ya kunyumba. Kwa kweli kuhusu kama Peramiho kumebadilika si sana kidogo na mwaka jana nilipokuwa kule sasa kutoka pale njia panda ya kwenda Likuyufusi mpaka mlangoni hospitali kuna rami sasa. Kwangu naona ni jambo nzuri sana maana usafiri unakuwa wa haraka zaidi ukizingatia wagonjwa wanaingia kila dakika. Kuhusu kwa nini majina yanaanza na LI nitafanya uchunguzi na kama kuna mmoja anajua naomba msaada...Maana hapa kama umenistua nilikaa hapa nikiwa nawaza hivi kwa hili jina PERAMIHO lina maana gani? Nikawa nimeligawa PERA-MIHO nikawa natafakari PERA ni tunda na MIHO kwa kingoni ni macho. Je? ndio kusema maana yake NI PERAMIHO NI PERA LA MACHO? jibu sijapata kwa hiyo nalo nalifanyia kazi ...ahsante kwa wazo zuri...

Emmanuel Mhagama said...

Hapo kwenye majina mie mgeni kidogo, kwanza sikuwahi kuwaza juu ya hilo.
Kwa habari ya Peramiho, sina hakika mnapajua kiasi gani maana mie hapo ndo kunyumba. Wakati Songea pamebaki kama palivyokuwa, Peramiho habari ni tofauti sana; PAMECHAKAA KULIKO MAELEZO. Kilichonoga kwa sasa ni ile lami iliyofika hadi mlangoni, vinginevyo, mimi ninayeijua Peramiho ya miaka ya tisini nikipaangalia sasa machozi yananilengalenga.

Rachel Siwa said...

Haahaah baba Isaac, Mbogo yupo Bongo na da'Mija huko wanakula vitu Fresh!!!

Kuhusu Majina ngoja nami nijifunzie hapo baba,sielewi kwa kwanini.

Asante da'Kadala[Yasinta] kwa matukio ya Nyumbani, usije ukalia tuu kwa kukumbuka ya Nyumbani.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama! Ulichosema ni kweli kabisa. mie huwa nasikitika nikifika stendi ya peramiho ni fujo tu hakuna stendi ni kusimama tu pale na pale.....kwa kweli bado tupo nyumaaa.

Kachiki wewe subiri tu nifanye utafiti wangu wa majina. Kulia pia ni safi kwani kunakufanya uzidi kukumbuka na kupenda ulikotoka...

Anonymous said...

mbona hapo umenikumbusha nilipokuwa vacation huko mwezi wa kwanza mwaka huu unanifanya nikumbuke msemo wa mwalimu wangu wa geographicalkuwa EAST OR WEST HOME IS BEST sasa pasipokuwa bora nyumbani kwako kutakuwa wapi huku tuhemeako? wala sikubaliani kuzitukukuza hizi sehemu za kufikia - nabambu mbawala