Thursday, August 30, 2012

KUHESHIMU BENDERA YA TAIFA!!!!!!

Nimekaa hapa nikajikuta naimba huu wimbo je wewe unaukumbuka? Ungana nami katika kumbukumbu hii haya moja,mbili, tatu..............

1. Bendera ta Tanzania, ndiyo ya kujivunia,
Ilianza kupepea, mwaka sitini na moja,
Hapo inashuhudia, tunavyojitegemea,
       Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.

2. Siku ya tarehe tisa, saa sita kamili,
                         Mwezi wa kumi na mbili, yalikuwa mambo sasa,
                    Mlima Kilimanjaro, bendera yetu hutwekwa,
                Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.

3. Rangi kijanikiwiti, yaonyesha mbuga zetu,
     Manjano ndiyo madini, yaliyo uchumi wetu,
    Buluu huonyrsha maji, yaliyo nchini mwetu,
Nyeusi ni yetu sisi, Waafrika asilia
Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.

4. Bendera yetu mwanana, yajulikana bayana,
Duniani twatukuka, katu hatuwi mateka,
   Bendera yapeperuka, Uchina na Amerika,
Wala haitatatuka, na juani kuchujuka,
  Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.
.......................................................................................................................
Kama sikosei ilikuwa darasa la sita au la saba

10 comments:

Anonymous said...

Yasinta, tunashukuru kutupeleka Tanzania tena. Kwa kweli tunajuvunia kwa rangi nzuri za bendera yetu zenye kuleta mana halisi/kamili kama zinavyoimbwa kwenye huo wimbo. Mungu ibariki Tanzania nchi yenye amani.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina! Ahsante,,,kweli Mungu ibariki Tanzania yetu!!!

Salehe Msanda said...

Hongera
Kwa kuutukuza utanzania,Ni wachache wanaoheshimu bendera pamoja na kuwa ni moja ya kilelelezo cha Taifa letu. Kizazi kipya cha Tz hakioni umuhimu wa bendera ya Taifa,ni nadara sana kuwaona vijana wanasimama wakati bendera ya Taifa inashushwa au kupandishwa. Kwa kifupi kuna kasi ya ajabu ya kusahau historia ya Tanzania ilikotoka na umuhimu wa kuheshimu historia yetu.
Kazi kweli kweli

Unknown said...

Asante

Unknown said...

Hii ilikuwa darasa LA 5

Unknown said...

Asante sana Yasinta, binafsi nimefurahi kuupata wimbo huu,niliuimba mwaka 1974,ila naona kama ubeti wa pili haujakamilika,kuna mistari miwili kabla ya mstari wa mwisho

jasmetp said...

Sasa hivi Cambridge system inachukua utanzania wetu. Hawajui history Wala geography ya Tanzania. Ni mashaka matupu

jasmetp said...

Yasinta, ubeti wa kwanza na WA pili kuna mstari unaopungua. Rejea tena kwenye vitabu. Hata mie naupenda sana. Nakumbuka klabu yangu iliuimba pale Shree Hindu Mandal primary school na kushika nadasi ya pili. Ilipendeza sana

Anonymous said...

Asante Yasinta. Nimeanza kufundisha wanafunzi wangu. Sasa ule uberi was pili unanichanganya. Nisaidie kukumbuka

Unknown said...

Yap nakumbuka nilikuwa darasa la tatu kipindi vitatu vinabadilishwa na kuanza kutumika vitabu vya Ben& Company.Hakika vitabu hivi vilikuwa vizuri na kweli vilitufundisha uzalendo.Hongera sana ndugu.