Thursday, August 9, 2012

FIKRA/WAZO LA LEO:- UTOFAUTI WA BINADAMU JINSI ULIVYO!!


Nimekuwa nikifikiri sana jinsi binadamu tulivyo tofauti. Sio kimaumbile tu LA HASHA. Bali  ni kiMATENDO, kiMAWAZO/kiFIKRA na  kiTABIA. Kwa mfano: Kuwa na ile tabia ya UMIMI/kijionea huruma, yaani mtu anajua amefanya kosa, lakini hata hivyo anaona wewe aliyekutendea unamwonea tu.Anataka uwe upande wake.
Halafu hii ya kuwa na HASIRA ZA HARAKA ambazo watu wengi inakuwa ngumu kusamehe hata kitu kiwe kidogo kwako kinakuwa kikubwa. Sababu kubwa wanakuwa wameumizwa sana na yule aliyemuumiza mwenzake anaona si umizo/maumivu. Lakini kuna wengine ni wepesi sana kusamehe hata iweje sasa sijui wanasamehe kweli au?
SWALI LANGU ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku:- Je? kama wote tungekuwa hivyo dunia hii ingekuwa? Na Je? kundi lipi ni jema?

2 comments:

Anonymous said...

hakika leo umenigusa sana na mada yako dada yasinta sina kawaida ya kuchangia ila huwa na somaga tu mada zakom na comment za watu lakini leo imenibidi ni changie maana hii mada utadhani ya kwangu kweli mimi mwenyewe hapa nilipo kuna mtu tena ni ndugu yangu wa damu kwake kukutendea mabaya sio ishu lakini wewe ukija kumkosea aidha kwa bahati mbaya au kwa makusudi kweke haliishi hata ukitaka usuluusho hataki anakinyongo,kiburi,ubinafsi,dharau yoote yakwake,anaweza akakukosea yeye lakini anakujeuzia kibao ya kwamba wewe ndiye uliye mkosea na mimi ni mwepesi sana wakumsamehe mtu hata kama hajaniomba msamaha maana najua hii dunia tunapita tu tumekuja duniani hatuna kitu na tunaondoka bila ya kitu ss tunagombania vya dunia ambavyo tutaviacha tu kama tulivyovikuta mimi sijuii watu wengine wanjiona vipi na wenzao wengine hujiona bora kuliko wenzie wao ni wakuonewa huruma tu posipo kujali wenzie wanahitaji huru kama wao hakika dada yasinta kuna watu wa aina hii tena sana tu

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu usiye na jina. Bahati mbaya hajataja jina lako ila sio mbaya sana..Nimeyapenda maoni yako sana tu,,Basi naona tumshukuru Mungu kwa kutuumba watu tofauti maana angeumba wote wa aina moja wanaopenda kusahau haraka yaliyotokea kwa kuomba radhi au kinyume chake ingekuwa hakuna maana ..Au labda ingekuwa safi sijui maana kila kitu kingekuwa sawa... Ahsante kwa maoni na karibu tena..